Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Mungu azilaze peponi roho za marehemu na awapatie nguvu wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu
 
Rip itakuwa mteremko mkali na uterezi gari ikavuta korongoni
 
Habari mbaya sana, poleni wazazi mm ni mmoja wa wazazi ambaye sipendi kabisa vi trip vya pamoja iwe ni kwa watu wazima au watoto i prefer private transport
Usipende kulaumu kila kitu. Pia ukiwa katka trip ya peke yako haikuhakikishii usalama kama unavyodhani,lolote laweza kumkuta yoyote mahali na wakati wowote kama una mungu muombe tu akunusuru na hayo mambo
 
Mungu wa huruma tumekukosea wapi? Poleni sana wazazi pamoja na wote waliopoteza wapendwa wao katika ajali hii! Pumziko la milele uwape Ee Bwana!
 
Niko njiani kuelekea Arusha. Nimefiwa na watoto wa kaka yangu wawili katika hiyo ajali. Mungu atupatie wepesi.
Pole Mkuu, Mungu na awafanyieni wepesi, na mkawe na safari njema.
 
Mungu awatie Nguvu wanafamilia wote waliopata Msiba ni Huzuni
 
Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.
Duh! Poleni sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…