Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Uwiii nimesisimka sana kuisoma habari hii mbaya. Halafu nimepita hapo wiki jana tu. Wapumzike kwa amani, poleni wazazi na wanafamilia wote kwa janga hili.
 
Mungu awepe makazi mema watoto wasio na hatia hao, ila repoter sijaona maelezo ya chanzo cha ajali maana najua hakuna ajali isio na chanzo iwe uzembe au bahati mbaya
 
Poleni sana Mwalimu kuu na Shule yote Poleni kwa tukio hili la kusikitisha Mungu awalaze Marehemu wote Mahala pema ,jamii husika jipeni .moyo mkuu

Yote ya Mungu. Wapunzike kwa amani. R.I.P

Ni vema kufanya risk assessment kwa kila jambo.
 
Ajari kama hizo ni za kutatanisha tena arusha usiseme. 2012 pale makumira ukitoka chuo pale darajani kabla hujafika usa ilikuwa ni asubuhi mapema basi la ngorika na haice kuelekea dar lilitafuna watu sijawahi kuona almost wote walikufa tulivyofika mda huo huo police wanatoa maiti zilizokuwa kama nyama buchani hapakuwepo na damu hata kidogo.

Yule dereva alikufa vibaya sitosahau alivyokuwa anapiga kelele ajari ilikuwa ni asubuhi saa 1 hadi saa 4 asubuhi gari la kuvuta basi lilikuwa halijafika. Chuo kizima tulikwenda kuvuta ile basi walau dereva aokoke, tulivuta tukashindwa konda alioloka alikuwa anapiga kelele akimuita kwa jina chilo chiloo nakufaaa, mida ya saa nne na nusu gari la kunyanyua basi likafika likaanza kuvuta amenatia kwenye vyuma mara kunyanyua tu juu gafla likarudi chini likammalizia tulisogea karibu ila hakukua na damu jamani sijui kwann.

Wapumzike kwa amani.
 
Nimeangalia picha za bus linaonekana halijaumia sana. Yani usingetegemea vifo viwe vingi kiasi hicho kiasi kwamba nahisi kuna kitu kiko nyuma ya ajali hii ambacho sisi binadamu wa kawaida hatuwezi kukielewa.
Acha kuleta fikra shirikishi.
Watoto wetu wapumzike kwa amani wakiutazamia ufufuo.
 
Mungu awape nguvu na uvumilivu familia zote ktk wakati huu mgumu,Mungu zilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom