Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

Sawa sikatai watu wamefanya kazi, hali iliopo sasa ni kwamba ufanisi sio ule uliokuwepo zama zile. Uzalendo hakuna hilo sijui utaliteteaje. Kazi inaenda na matokeo ila kwa hapa tulipofikia ni dhahiri kazi za mikataba zingeongeza tija. Uzembe unaofanyika serikalini huwezi kuukuta kwenye kampuni binafsi. Utajiuliza ni kwanini? Jibu liko wazi
 
Na kwa kuongezea tulitakiwa tuwe mbali mno ila sababu ya kukumbatiana na kuoneana aibu ndio tupo hapa tulipo. Wenzetu tulioanza nao safari wakajizatiti hatuwagusi kimaendeleo😂
 
Pension ya nini mtoto kaajiriwa na 23 akifika 28 anaachia ofisi hapo unalipwa penshen gani na bado umri mdogo? Kwani wanaopiga kazi kwenye NGO wanalipwaga pension wale baada ya contract ya miaka 5
Unamaanisha makato ya kwenda kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii yasiwepo na hiyo iwe moja kati ya condition za utaratibu huo wa ajira?
Vinginevyo tuondoe neno 'Kustaafishwa'.
Kwa utaratibu wa elimu yetu ni nadra sana kukuta mtoto anaanza kazi rasmi akiwa na 23 years.
 
Bado mleta maada ana hoja kukuzidi wewe mtaalamu wa x,, rays
 
Tatizo lililopo ni la kimfumo, ata wewe ukipewa hiyo nafasi hutoweza kufanya chochote. Utapiga kelele kwa sababu uko nje ya mfumo, ila ukishaingia nawe unakuwa ni wale wale.
 
Na wanapokufa hao wenye uzoefu huwa tunafanyaje?
 
sasa ndugu nikuulize,

Deni la bodi ya mikopo atalipa nani kama nikiajiriwa kwa miaka 10 tu?

Kwa kweli ukipewa kitengo cha kutunga sera za uchumi na Siasa utatenguliwa mapema sana
Na mimi mwenye miaka kibao tangu nile hela za heslib nan ananilipia hayo madeni yangu huko maana sijaajiliwa na sina huo mpango tena
 
Tatizo lililopo ni la kimfumo, ata wewe ukipewa hiyo nafasi hutoweza kufanya chochote. Utapiga kelele kwa sababu uko nje ya mfumo, ila ukishaingia nawe unakuwa ni wale wale.
Mtu mmoja hawezi kubadilisha System ila tunapoelekea kinachoendelea sasa hakitaendelea kesho.., Kuna mifumo mingi ilikuwepo Utumwa, Ukabaila na sasa hivi Ubepari ambao kutokana n teknolojia na hakuna uhitaji wa nguvu kazi na wenyewe utakufa kifo cha kawaida..., Uhitaji wa ajira zenye Ujira ni mkubwa kuliko Supply..., Na huwezi kusema kwamba huwezi kufanya cha kufanya wakati unachukua Kodi za watu na wewe kazi yako ni kuhakikisha welfare ya hawa watu....

Kwahio what is currently available is not fit for purpose....
 
Yana mwisho.
 
Kwani ukifanya kazi hiyo miaka kumi ukapata mtaji unashindwa kuendelea ku produce?
 
Kama mabadiliko yatachukua miaka 50 au 100 ijayo ambapo sisi hatuta kuwepo, kwa nini mabadiliko yafanyike?

Unatakiwa ujue, binadamu ni mbinafsi sana; na asipowekewa mifumo thabiti ataendelea kuwanyonya wengine.​
 
Kwahiyo madaktari ningwa wote wae wakufunzi ili Hali huko vyuobi wakufunzi wapo, aise hii akili ya wapi mkuu
 
Kama mabadiliko yatachukua miaka 50 au 100 ijayo ambapo sisi hatuta kuwepo, kwa nini mabadiliko yafanyike?

Unatakiwa ujue, binadamu ni mbinafsi sana; na asipowekewa mifumo thabiti ataendelea kuwanyonya wengine.​
Miaka 50 mpaka 100 ? Hapa juzi tu Gen Z Kenya wamelianzisha..., na sasa hivi wamepoa ila hakuna kilichobadilika hivyo ni kwamba wameweka pause..., Na huku Bongo hawa ambao wapo kindergarten sasa hivi (na Gen Alpha) siku wakiingia mtaani unategemea nini kitatokea..., Ushaona hata mfano wa huyu mleta uzi badala ya kupeleka chuki kwa watunga Sera anapeleka chuki wa walalahoi na wabangaizaji wenzake (sababu hata wao wanachopata hakikidhi mahitaji)

Extreme Poverty anywhere is a threat to Society Everywhere....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…