Akili ya BMW kwenye Magari

Hii paragraph ya mwisho, Wajapan wa JF wapo kwenye kikao kirefu. Wanapanga kukuita waende wakakuhoji na wewe.
 
Unaponunua gari angalia mahitaji yako. Usifuate mkumbo, Kuna watu wanasifia walichonacho hata kama wanateseka.

Pia, gari inaweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja ikawa ya kijinga kwa mtu mwingine.
 
Najua wapenzi wa BM wanaweza nishambulia ila haya ni maoni yangu:

Kama unahitaji luxury, speed ni sawa tu. Ila kama ww ni mtu ambaye wakati mwingine unasafiri na unapoenda ni offroad ni gari ya kijinga. Toyota LC LX ni option swadakta kwa mtu wa aina hii japo bei ni kubwa. Mm huwa naona kluger ni gari zuri kuliko X series yoyote kwa mazingira yetu.

Binafsi bora nikanunua LC LX used mkononi kwa mtanzania tena namba A iwapo ina hali nzuri kuliko kununua BM x series yoyote mpya.
 
Sawa baki na maoni yako mkuu unataka kusema ni bora uwe na gari ya miaka 15 nyuma kuliko X 4 ya 2022 sawa sawa Mkuu...
 
Boss wangu, X4 ya 2022 na LC lx ya 2007 nachukua lc ya 2007 tena isiwe mpya wala. Mkononi mwako wewe mtanzania kama itakuwa na hali nzuri hata iwe namba B sijui A.
Yap hiyo gari vijijini inaaminiwa sana Mkuu hapo umechanganya mada kwa gari ya kazi na ya kutokea sijui kama hiyo ya 2022 ipo Tanzania ingawaje niliziona mbili Arusha za 2020..na daslm kadhaa za 2020 kushuka chini hivyo vyuma ni balaa mimi nipo na LC ndio nazibeba sana kwa ajili ya kukata bodi kuziweka au kuwauzia makampuni ya utalii ila pana mawe kama Audi Q series kama hiyo 5,BMW aisee hayo madude yasikie tuu..yana confort sana pamoja na balance ya kutosha..
 
Ni kweli. Ndo maana nilisema unaponunua gari angalia matumizi yako. Mambo kama kipato chako, utalitumia kwenye mazingira gani, mafundi, spea, alternative iwapo lina hitilafu ndo yakuongoze kufanya maamuzi.
 
Jamaa yangu hapa kariakoo alikuwa na Toyota crown athlete akauza akanunua BMW 320i huwa anaisifia Sana BMW yake kwenye handling na balance.
Nimeshindwa kujua inakuaje crown inapishana kwenye balancing na BMW yenye engine ndogo kama 320
 
Usifananishe BMW 320i na vitu vya ajabu ajab, hasa ukute 320i GT ... mwanawane ni motoo
 
Isiwe tu kama ya Mad Max , unatembea na kidumu cha coolant.. hasa upate za kuanzia 2014 kuja juu..
Za 2014 kuja juu ushuru tu shikamoo. Hapo tunaongelea base model mfano 320i.

Ukitaka performance model je.

Jiulize kwann E90 zipo nyingi ila F30 za kuhesabia? Yaani mjini ukikutana na 3 series 10 basi 9 ni E90 au unaweza kuta zote 10 ni E90.
 
Jamaa yangu hapa kariakoo alikuwa na Toyota crown athlete akauza akanunua BMW 320i huwa anaisifia Sana BMW yake kwenye handling na balance.
Nimeshindwa kujua inakuaje crown inapishana kwenye balancing na BMW yenye engine ndogo kama 320
Hapo nahisi sababu ni small size ya 3 series.. Suspension system..
 
Za 2014 kuja juu ushuru tu shikamoo. Hapo tunaongelea base model mfano 320i.

Ukitaka performance model je.

Jiulize kwann E90 zipo nyingi ila F30 za kuhesabia? Yaani mjini ukikutana na 3 series 10 basi 9 ni E90 au unaweza kuta zote 10 ni E90.

Mkuu hebu tuambie kidogo utofauti wa E90 vs F30

Tupe summary review tupate mwanga asee
 
Mkuu hebu tuambie kidogo utofauti wa E90 vs F30

Tupe summary review tupate mwanga asee
Niliwahi kuandika humu ngoja nikutafutie link tajiri. Uzuri nimemiliki yote ila F30 kwa muda mfupi sana ila E90 na E46 kwa zaidi ya miaka 3 each.
 
Mkuu hebu tuambie kidogo utofauti wa E90 vs F30

Tupe summary review tupate mwanga asee
 
Asante mkuu
Ngoja nipate madini
Napenda sana elimu ya magari [emoji122]
 
Kitu ambacho hujui ni kuwa; sio kwamba watu hawajui magari mazuri na Imara
Tatizo watu wengi hasa Africa wapo kwenye rank ya security needs na kwa kiasi kwenye social needs, na maanisha kipato chao kinatosha kuwazia kumiliki usafiri.
Suala la kumiliki usafiri wa aina gani hapo unaongelea kama 7% kwani hapo unaongelea wanaojiweza vizuri na wenye usafiri tayari hivyo wana choice ya kuamua wanunue gari tena liwe la Brand gani
 
Mkuu hebu tuambie kidogo utofauti wa E90 vs F30

Tupe summary review tupate mwanga asee
Hivyo ni vizazi viwili tofauti.,

hata engines zake kwa sehemu kubwa hazishei.

e90 au f30 au G20 siyo specific gari fulani. Ila ni collective names kwa kizazi fulani za magari.

mfano 320i ya e90 ina engine ya N46B20 au N43B20. N43 ni direct injection wakati n46 ni kawaida.

320i ya f30 inakuja na engine ya N20 au B48. Zote ni twin scroll turbo charged, Direct injection. Na zinazalisha power kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…