Al-Jazeera ni TV ya ovyo, kwenye vita ya Israel vs Hamas hawasemi athari zinazotokea upande wa Hamas

Al-Jazeera ni TV ya ovyo, kwenye vita ya Israel vs Hamas hawasemi athari zinazotokea upande wa Hamas

Ukiwa muongo, pia uwe makini. Kwa muda wote vita hii imepiganwa hajafa wala kutangazwa wangapi wa Hamas wamekufa! Picha zinazorushwa ni za vitoto tuu na kidogo wanawake.

Cha ajabu ukiangalia TV hiyo hiyo, miili mingi ya maiti zilizokufa GAZA na iliyofunikwa kwenda kuzikwa ni ya watu wazima.

Propaganda zingine itumike na akili kidogo basi.
Fox,CNN,BBC ,Sky news zote hazipo upande wa Palestine na hicho anacho ripoti Al Jazeera ni robo tu yanayo tokea Palestina, zaidi ya robo tatu yanayo tokea Palestina haya ripotiwi na uzuri dunia imejua ukweli,kura UN zimepigwa mara tatu zaidi ya asilimia themanini wana msupport Mpalestina,mpaka kura za juzi Canada,Spain,Ireland nk kutoka Europe wanamsupport Palestina.
 
Hamas sio magaidi
Pia hakuna tv ama idhaa zinazokosa propaganda ziwe za west ama east wote lazma waangalie maslahi yao kwanza kabla ya maslahi yenu
Kwani hizo BBC CNN fox dw namfano wa hayo
Si walitangaza kwamba Iraq [emoji1131] kulikua na weapons of mass destruction vipi waliwahi kukuonesha
Hao hao si ndio walikua wanasema kwamba ukraine anashinda waliosema vita yake dhidi ya Russia sasa hv hata msaada wanafikiria kuikata
Nakupa tu faida walau aljazeera wanayotangaza 75% yanaweza kua na ukweli tena hasa yanayohusiana na kinachoendelea hapo ghaza
Unachanganya sana kauli za wanasiasa wa magharibi na taarifa zinazotolewa na media za magharibi. Fuatilia vizuri taarifa zilizokuwa zikitolewa na BBC na CNN kuhusu spinning iliyokuwa ikifanywa na utawala wa GW Bush (US) na ule wa Tony Blair (UK) kuhusu Saddam Hussein kuwa na silaha za maangamizi na ufadhili wa ugaidi. Ilikuja kuthibitika ni kweli Bush na Blair walidanganya. Kama nilivyosema, media ziliripoti viongozi hao walichosema zikachambua na kuona zina mapungufu kibao.

Aidha, majuzi wakati US wakiondoka Afghanistan, drone yao moja ikashambulia nyumba ya mfanyakazi wa shirika la misaada na kumuua pamoja na watu 10 wa familia yake. CIA wakadai wameua gaidi la ISIS likiwa mbioni kutekeleza shambulizi. CNN ndiyo ilikuwa TV ya kwanza kufichua ukweli kwamba wameua raia asiyekuwa na hatia na watoto wake. Baadaye serikali ya Biden ikakiri kosa na kuomba radhi na visingizio kibao. Ingekuwa hapa kwetu CNN ingeandamwa kwa kusaliti siri za jeshi.

Fuatilia vizuri media za West uone zinavyohoji ukweli toka serikali za nchi hizo. Soma details uone kazi iliyokamilika. Siyo vipande vya kushabikia. Wanajitahidi sana kuwa objective. Aljazeera nayo iko vizuri ingawa lengo lao hasa ni kuziba pengo wanaloona katika habari za mataifa ya kiarabu na hasa kuhusu wananchi wake.

Kuhusu Hamas kumbuka usemi wa: gaidi wa mtu mmoja ni mpigania uhuru wa mtu mwingine. Ni uamuzi na haki yako kuwaona Hamas si magaidi.
 
Hujasikia mpaka sasa Wapalestina 18,000 wameuliwa na mabomu ya mazayuni? Kati yao hao, watoto ni zaidi ya 10,000?

Twambie wewe, wajomba wa mungu wako wanatangazwa wapi vifo vyao?
Na mpaka mwisho wa mwezi huu tunazungumzia elfu ishirini na tano … mpka waseme… wameanzisha vita wasivyo viweza
 
Back
Top Bottom