dormant accont
Senior Member
- Jan 4, 2022
- 154
- 162
- Thread starter
- #361
Naona unachanganya vitu viwili hapa, uthibitisho(proof) na madai(claims).leo umenipa swali dogo sana, acha nikupe uthibitisho, quran 83-86) Mungu anasema hivi 'Na hiyo ndio hoja yetu tuliyompa Ibrahim juu ya watu wake, tunampandisha cheo tumtakae. Hakika Mola wako ni mwenye hikma wa yote, mjuzi wa yote. Na tukamtunukia is-haka, na yakub. Wote tukawahidi. Na nuh tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake daud, na sulaiman, na ayub, na yussuf, na mussa, na harun. Na hivyo ndivyo tulipavyo wafanyao ihsan. Na zakaria, na yahya, na issa na ilyas. Wote ni miongoni mwa swalihiina. Na ismail, na alyasa na yunus, na luti. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu'.
Quran (16-35) mtoto (issa) akasema, hakika mimi ni mtumwa wa M/Mungu. Amenipa kitabu, na amenifanya nabii'.
Quran (suratul imran), umeteremshiwa wewe, muhammad, hii quran yenye kukusanya ukweli wa misingi yote ya sharia ya mbinguni iliomo katika vitabu vilivyotangulia. Na hakika kabla ya quran M/Mungu alikwisha teremsha taurat kwa mussa, na injil kwa issa.
Unaponipa aya za kuran, unanipa madai ya waarabu kwamba mungu kawaambia nini.
Hayo ni madai ya waarabu kwamba mungu anataka tufanye nini.
Akili yako inabidi itambue utofauti kati ya uthibitisho na madai.