Ali Kiba anadai kila mtu kazaliwa Muislamu na kwamba Wakristo wote ni watu waliobadili dini

Ali Kiba anadai kila mtu kazaliwa Muislamu na kwamba Wakristo wote ni watu waliobadili dini

Hivi logic ipi unayo iongelea wewe ? Maana naona unalitumia vibaya sana hili tamko. Tukikuomba uelezee unacho maanisha kwa kuzingatia misingi ya logic najua hutaweza sasa sijui kwanini unakurupuka katika matumizi ya maneno ?

Naomba utumie logic unayoijua wewe kututhibitishia ya kuwa Dini ni ubunifu wa mtu na uonyeshe usahihi wako.

Ni kama zilivyo logic ya vitu vingine ambavyo unakubaliana nazo kuwa ni ubunifu wa watu

Kama ilivyo kwa mziki na vitu vingine ambavyo vimebuniwa
 
Yupo sawa kulingana na Imani yake kwanini wewe ulitaka akusemee Imani yako?
 
Habari za mola zinafundishika na kukaririka kama ilivyo kwa habari zingine kama panya mabaka aliyemvisha paka kengele, na habari ya pazi aliyebebwa kichwa chini miguu juu na jogoo

Nimezipata habari za Allah na ndio maana niko hapa nilipo, na hata hapa utaendelea kuziweka lakini haita saidia

Vipi, we hujazipata habari za Yesu kubatizwa na kwamba yeye ndio njia ya kweli na uzima?

Kwasababu umezipata, vipi umesha okoka?

Unasubiria nini?

Hazina ushawishi eti?

Basi hali ni hivyo hivyo hata kwenye habari za allah kwa wengine wasio husika na imani hiyo
Very intelligent 👍🏿🙌🏿
 
Shida ya Ali Kiba ni kusema kile kilichoandikwa kwa mujibu wa imani ya UISLAM??

UISLAM mafundisho yake yapo wazi kuwa kila mtu huzaliwa akiwa Muislam na NDIO maana hatuwapeleki watoto kwa masheikh misikitini wawape dini....kwa sababu kila tunazaliwa tukiwa waislam tayari inabaki kusoma muongozo wa kuja halali na Haramu .

Na wewe una haki ya kutaja unachoamini kuwa mtu huwa Mkristo pale tu anapobatizwa...over wala hakuna haja ya mijadala mirefu.
Vipi kuhusu wachina, wajapan, wazungu na wahindi na wao walizaliwa waislam maana sionagi kama wana muda na huo msemo wenu.
 
Yupo sawa kulingana na Imani yake kwanini wewe ulitaka akusemee Imani yako?
Kama imani yako inafundisha usipomuabudu Zahanary una matatizo ya akili. Hutakiwi kuwatangazia wengine kuwa wana matatizo ya akili sababu tu hawamuabudu Zahanary.
Inabidi uangalie nini uanaandika kwa uma( uchuje).
 
Siwezi kumjua muanzilishi lakini haina maana kuwa halijabuniwa na watu/mtu

Zipo sababu nyingi za mimi kuto kumjua

Kuna wabubifu wengi wanaopenda kuwa anonymous

Hata wewe natumaini unakubali neno pombe lilibuniwa na watu/mtu lakini sidhani kama unamjua huyo mbunifu
Nimecheka sana, sasa unajuaje kama hilo limebuniwa ?

Kutokumjua kwako muanzilishi ni ishara ya kuwa hukijui unacho kiongelea, hili katika elimu tunasema ni uzushi. Kadhalika suala la kutomjua muanzilishi katika elimu ya uhakiki wa habari, habari hiyo inaingia katika habari ya kutokufanyiwa kazi mpaka pale kutakapo patikana maelezo sahihi na yenye ithibati ya kuyapa nguvu mapokezi hayo ya muanzolishi asiye julikana.

Sababu zako hata zikiwa elfu hazina nguvu sababu hazija kidhi vigezo vya uzani katika marejeo, zaidi ya wasi wasi na kutokujua kwako unacho kijadili.

Si katika hili, sababu jaribu kuanishia jambo na usilinganishe jambo hili la dini na habari za watunzi wa visasili. Suala la dini haliingii katika huu mfano, sababu ni mfumo wa maisha na ni elimu na maarifa ya kurithishana kizazi mpaka kizazi kingine.

Unaposema neno Pombe limebuniwa mfano wako hauingii katika suala la dini la dini, yaani unaleta ulinganyo usio linganywa. Jaribu kuweka mifano hai.
 
uislamu maana yake ni,kumtii mungu na kufuata amri zake,yaani kujiweka chini ya mnyazi mungu,
automatically ukizaliwa peke yako ukaachwa kisiwani peke yako utajikuta tu unajiweja mikononi mwa sir God,,wala haihitaji kuhubiriwa
Dunia ina watu bilioni 7 waislamu wapo bilioni 1 na nusu, hao waliobaki bilioni 5 na nusu sio waislamu na kuna wengine hata maana ya neno uislamu hawajui.
 
Nimezipata habari za Allah na ndio maana niko hapa nilipo, na hata hapa utaendelea kuziweka lakini haita saidia
Usikimbie hoja kijana maelezo yangu yako wazi sana, umezipata habari za Allah ukiwa tayari upo katika fikra mfu, na ukawa huwezi kuhoji kwa usahihi sababu umekaririshwa namna ya kufikiria kama walivyo fikiria waio kutangulia.

Lengo siyo kusaidia bali lengo nikuweka ukweli wa mambo jinsi ulivyo, kwahiyo ni juu yako kufanyia kazi au kuyaacha hapa hapa. Kwahiyo hili lisikuumize kichwa.
Habari za mola zinafundishika na kukaririka kama ilivyo kwa habari zingine kama panya mabaka aliyemvisha paka kengele, na habari ya pazi aliyebebwa kichwa chini miguu juu na jogoo
Hii si hoja, vingapi vya hovyo vinafundishika kijana ? Mangapi katika Sayansi umesoma na ni uongo mpaka kesho ?

Swali langu la msingi ni wewe uonyeshe ukweli wa unachokiandika.
Vipi, we hujazipata habari za Yesu kubatizwa na kwamba yeye ndio njia ya kweli na uzima?
Tunarudi katika msingi, kuna kauli moja huwa tunaitumia sana inasema hivi "Kila mmoja hudai Laila ni wake, lakini tukimuuliza Laila anakana".

Baada ya kupata habari huwa tunarudi kuzihakiki habari hizo kama alivyo tuelekeza Allah aliye juu ya kuwa "Mnapoijiwa na habari kutoka kwa fasiki, basi zichunguzeni". Hili najua ya kuwa hujawahi kutumia muda wako kuchunguza habari za dini zinazo kufikia zaidi ya kuhoji kitoto. Kwahiyo mimi nilipozipata habari za Ukristo na Yesu nikazichunguza na nikapata hitimisho lililo sahihi.
Kwasababu umezipata, vipi umesha okoka?

Unasubiria nini?
Hazina ukweli kwa ushahidi wa kiakili, kihistoria na ushahidi wa kimazingira. Hili wewe nakupa miaka mia, huwezi kuthibitisha ya kuwa Dini, mathalani ya Uislamu ilibuniwa na mtu, kwa njia yoyote ile.
Hazina ushawishi eti?
Zina ushawishi ila hazina asili inayofika mpaka kwa Yesu.

Basi hali ni hivyo hivyo hata kwenye habari za allah kwa wengine wasio husika na imani hiyo
Kwahiyo hapa tayari umehitimisha, bila kuonyesha mchakato wa kielimu zaidi ya makisio, kwa mtindo huu lazima useme tu Mola hayupo, yaani unafikia hitimisho juu juu sana.
 
Ni kama zilivyo logic ya vitu vingine ambavyo unakubaliana nazo kuwa ni ubunifu wa watu

Kama ilivyo kwa mziki na vitu vingine ambavyo vimebuniwa
Jibu swali nililo kuuliza, au hujui ya kuwa katika logic kuna mchakato hufatwa mpaka kufikia hitimisho ?

Sasa pita humo ufikie hitimisho ulilo liweka hapa. Mambo si mepesi kama unavyo yaona.

Mimi nakubaliana navyo si kwa kutumia misingi ya logic sababu najua logic haina uwezo huo. Sasa usinilinganishe mimi na wewe katika kufikiri na kufikia hitimisho mimi ni njia zangu.
 
Nimecheka sana, sasa unajuaje kama hilo limebuniwa ?

Kutokumjua kwako muanzilishi ni ishara ya kuwa hukijui unacho kiongelea, hili katika elimu tunasema ni uzushi. Kadhalika suala la kutomjua muanzilishi katika elimu ya uhakiki wa habari, habari hiyo inaingia katika habari ya kutokufanyiwa kazi mpaka pale kutakapo patikana maelezo sahihi na yenye ithibati ya kuyapa nguvu mapokezi hayo ya muanzolishi asiye julikana.

Sababu zako hata zikiwa elfu hazina nguvu sababu hazija kidhi vigezo vya uzani katika marejeo, zaidi ya wasi wasi na kutokujua kwako unacho kijadili.

Si katika hili, sababu jaribu kuanishia jambo na usilinganishe jambo hili la dini na habari za watunzi wa visasili. Suala la dini haliingii katika huu mfano, sababu ni mfumo wa maisha na ni elimu na maarifa ya kurithishana kizazi mpaka kizazi kingine.

Unaposema neno Pombe limebuniwa mfano wako hauingii katika suala la dini la dini, yaani unaleta ulinganyo usio linganywa. Jaribu kuweka mifano hai.
Nimekupa hoja hapo ya kuonesha mazingira gani yanaweza kusababisha ushindwe kumjua mbunifu

Sio kila mtu anapenda kuwekwa public

Sio kila neno lilitotungwa linaweza kunulikana na wote

Chukulia mfano wa hapa hapa bongo kuna maneno recently mangapi ambayo yanabuniwa na watu na yanatumika kila siku ila haijulikani mtunzi?

Neno demu, msela, mrume, vishoka, kudanga nk.

Maeno hayo bila shaka ushawahi yasikia na unaelewa yakitajwa yana maanisha nini na si ajabu miongoni mwa maneno hayo hata wewe unayatumia

Vipi unabisha kwamba maneno hayo hayajabuniwa na watu?

Bila shaka huwezi kubisha

Vipi unawajua waliobuni hayo maneno ni kina nani?

Huwajui eeh?

Sasa kama utashindwa kujua mbunifu wa maneno ya miaka ya karibuni utawezaje kujua maneno ambayo yana miaka elfu?

Sasa kama utataka kulazimisha hapa kwamba kila neno lazima liwe na muundaji na asipo julikana basi neno hilo lilikuwepo na halina chanzo itabidi uniambie nani mtunzi wa neno Mziki, Kilimo, nk. Kitu ambacho najua huwezi

Kama huwezi kujua inventors wa hayo maneno basi huna authority ya kupinga hoja yangu kwa kigezo cha kutomjua mbunifu wa neno DINI
 
UISLAM HUU AMBAO ULIANZISHWA NA MA JESUITS WA VATICAN KWA KUMPA MOHAMAD KAZI MAALUMU???
Ni kweli kabisa.

Watu hawajui mana hawasomi vitabu vya dini za mwanzo.

Dola la Rumi lilikua na Wasomi na watu waliokua na uwezo mkubwa sana wa kupanga mambo ya miaka mingi na kuigawa Dunia ili waitawale.

Biblia iligawanywa Kwa mahitaji ya Eneo. Korani ni kitabu kilichozaliwa na Biblia ndio maana wakristo hasa wakatoliki hawababaiki kabisa na Masharif machache yaliyopo ndani ya Koran yanayoweza kukaririwa na mtu Kwa kichwa TU hata mtu asiyemjua kusoma Wala kuandika. Lakini huwezi ukakariri Chuo kizima Cha Biblia Ile ya Kikatoliki iliyojaza vitabu vya dini zote.

Mfano : Wajerumani walipokubali mafundisho ya Martini Luther waliondoa baadhi ya vitabu vilivyokuwa na misimamo mikali ya kisiasa ili kuondao Imani Kali ambayo ingeweza kuzaa uasi Tena.

Ukisoma Hadithi za Mtume muhamad karibu zote zimeandikwa kwenye vitabu vilivyoondolewa kwenye Biblia Moja wapo kati ya Ile ya Kiothodox au Kikatoliki.
Mapadri wa mwanzo walimfundisha sana Muhamadi na akajua vitabu vingine vya dini ndio maana akawa na uwezo mkubwa wa kutoa ufafanuzi kupitia mafundisho ya vitabu vya dini ya Kikatoliki na Kiothodox. Mission yake ikarejea kwenye Torati ya Mussa ili akomboe Dola la Kiarabu.

Yani Kweli Mfipa kule Namanyere ambaye hajui kusoma Kiarabu na korani ni Muislam Kwa sababu TU hajabatizwa?

Tangu enzi za Muhamad palikua na watu waliokua ni wazushi wanaojua kutunga maneno ya uongo na kufanya rehearsal majukwaani Kwa kuhutubia propaganda za uongo ili kufanikisha mambo yao ya kisiasa na kijamii.

Ili uwe Muislam ni lazima useme Shahadu!!
Hakuna Mola anayepaswa kuabudiwa ila Allah na mjumbe wake ni Muhamad.
Sasa mmasai kazaliwa kule Ngorongoro na kuishi na Twiga wapi amekua kuwa Mjumbe Mwenyezi Mungu ni Mohamad. ?

Waafrika wanaamini TU na kumeza kila kitu kilicholetwa na Mzungu au Muarabu.

Sio watu wote ni kizazi Cha Ibrahimu!!
Ibrahimu alikua na ndugu zake ambao pia walikua na wajukuu na vizazi mpaka Leo. Kwa hiyo Waislam wa Burundi na Congo ,Kigoma na Tabora kujifanya eti nao ni vijukuu vya motume wanajidanganya?
Wakristo wao wako wazi kuwa ni wajukuu wa Ibrahimu sio Kwa kuzaliwa Bali wa kiroho. Kwa hiyo hapo hakuna kurithi dini Bali kukiri na kuamini Mwenyewe. Hulka ya dhambi kama uchoyo ,hasira , chuki ,tamaa ndiyo inarithiwa kutoka Kwa Adamu lakini dini na Imani ni falsafa na dhana ya mtu anayofuata yeye Mwenyewe au jamii.
 
1. Hakuna atakaye andamana eti mkristo kasema alizaliwa akiwa mkristo... Bali tutamuuliza. Je ubatizo ni kwa ajili GANI??

2. Kwa mafundisho ya Uislamu kila mtu anayezaliwa huzaliwa akiwa ni Muislamu ndio maana Waislamu hawawapeleki watoto wao Misikitini kuwabatiza, maana ukishambatiza tu tayari umeshamuondolea uhuru wake aliozaliwa nao ambo ni Uislamu....

Qur'an 30: 30. Basi elekeza uso wako kwenye Dini yenye kujiengua na upotofu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui..

Umbile la VIUMBE WOTE NI UISLAM....HUO UYESU UMEUPATA WAPI??
Ili dunia iwe mahali salama pa kuishi ninyi watu mnatakiwa kupuuzwa, tena mpuunzwe kweli kweli. Sorry not sorry; kupuuzwa sio tusi, simply ni watu kuacha kushughulika na ninyi na kuwaacha mfanye mseme mnayoyakusudia.

Binafsi mijadala ya kidini naiogopa sana.
 
8Usikimbie hoja kijana maelezo yangu yako wazi sana, umezipata habari za Allah ukiwa tayari upo katika fikra mfu, na ukawa huwezi kuhoji kwa usahihi sababu umekaririshwa namna ya kufikiria kama walivyo fikiria waio kutangulia.
Kuna namna gani nzuri na iliyo bora ya kuhoji zaidi ya kudai uthibitisho?

Mara ngapi humu mmeshindwa kuthibitisha hizi habari?

Au nikupe nafasi ujaribu bahati yako leo pengine hapo kati kati umepata majibu sahihi?

Haya thibitisha Allah yupo
Lengo siyo kusaidia bali lengo nikuweka ukweli wa mambo jinsi ulivyo, kwahiyo ni juu yako kufanyia kazi au kuyaacha hapa hapa. Kwahiyo hili lisikuumize kichwa.
Weka huo ukweli wote tuuone

Ila uo ukweli usiwe na sura ya kihuni maana nitaukataa licha ya kwamba ulishtanguliza self defense
Hii si hoja, vingapi vya hovyo vinafundishika kijana ? Mangapi katika Sayansi umesoma na ni uongo mpaka kesho ?
Uongo wa sayansi au kitu kingine chochote hau justify uongo wa habari za quran uonekane ni ukweli

Umekutwa unaendesha gari rough na hauna leseni, unachukuliwa hatua kwa kutozwa faini we unaanza kusema "Sipaswi kulipa faini kwa kuendesha gari hovyo. Kuna watu wengine wengi mtaani ambao ni wahalifu hatari na wabakaji, na polisi wanapaswa kuwa wanawafukuza, sio kumsumbua raia mzuri anayelipa ushuru kama mimi"

”Kwa kweli, wahalifu mbaya zaidi wapo, lakini hiyo ni suala jingine! Hoja ya msingi yaliyopo ni (1) je, ni kweli uliendesha kwa uzembe, na (2) anapaswa kulipa faini kwa hiyo?

Swali langu la msingi ni wewe uonyeshe ukweli wa unachokiandika.

Tunarudi katika msingi, kuna kauli moja huwa tunaitumia sana inasema hivi "Kila mmoja hudai Laila ni wake, lakini tukimuuliza Laila anakana".

Baada ya kupata habari huwa tunarudi kuzihakiki habari hizo kama alivyo tuelekeza Allah aliye juu ya kuwa "Mnapoijiwa na habari kutoka kwa fasiki, basi zichunguzeni". Hili najua ya kuwa hujawahi kutumia muda wako kuchunguza habari za dini zinazo kufikia zaidi ya kuhoji kitoto. Kwahiyo mimi nilipozipata habari za Ukristo na Yesu nikazichunguza na nikapata hitimisho lililo sahihi.
Its funny

Kwa hiyo wewe vigezo ulivyotumia kupinga mafundisho ya Yesu ilikuwa ni kitabu cha Quran ambacho kinapingana mafundisho ya biblia?

Halafu hoja ya kusema Allah aliyejuu inatakiwa kutumika baada ya kuthibitisha kua hayo maandiko ni kweli ya kwake

Kwani huna habari kua hata kauli ya kusema "huwezi kwenda kwa baba pasipo mimi" ilinukuliwa na Yesu?

Kwa maana hiyo nitakuwa sahihi kusema unakubali kua nukuu hiyo ni maneno halisi ya Yesu?

Kama hukubali kwanini wewe uone ni simple kwa wengine kukubali nukuu unazodai kua ni za Allah?
Hazina ukweli kwa ushahidi wa kiakili, kihistoria na ushahidi wa kimazingira.
Kumbe pamoja na habari kuandikwa kwenye vitabu na kudaiwa vimeandikwa na Mungu lakini bado umevipinga na kuona uzushi

Tunaona kumbe hoja ya kusema vitabu vimeandikwa na Mungu ni kauli ya kilaghai, inawezekana hata hicho kitabu unachokiamini na wewe ni mwendelezo ule ule katika sura tofauti

Inawezekana kabisa kua Quran ni the same thing kama biblia tu kua vyote ni vitabu vya kizushi japokuwa vina nadiwa kuwa ni vitabu vya Mungu
Hili wewe nakupa miaka mia, huwezi kuthibitisha ya kuwa Dini, mathalani ya Uislamu ilibuniwa na mtu, kwa njia yoyote ile.
Wewe nikupe miaka mingapi ya kuthibitisha mbunifu wa maneno haya "demu, wakishua, muziki, disco vumbi, kudanga, kanga moko, "nk.

Miaka 500 itakutosha au michache?

Zina ushawishi ila hazina asili inayofika mpaka kwa Yesu.
Kwa kuzingatia source gani?
Kwahiyo hapa tayari umehitimisha, bila kuonyesha mchakato wa kielimu zaidi ya makisio, kwa mtindo huu lazima useme tu Mola hayupo, yaani unafikia hitimisho juu juu sana.
Kwa hiyo chenye makisio tafsiri yake ni kitu cha uongo?

Quran imeandika Allah alimuumba adam

Tuambie ni tarehe gani ya mwezi gani na mwaka gani ili kuonesha upekee wa Quran kwa kuwa specific

Au tuambie ni lini kwa kutaja saa, tarehe, mwezi, na mwaka ikiwezekana hata majira ya msimu kama ni kifuku au kiangazi tujue muhamad alikwea buraq kwenda anga za juu

Kuna maneno kua Quran imetabili mambo ambayo yanatokea miaka hii tangu iandikwe

Tupe hizo aya ambazo zitaonesha tarehe, mwezi, mwaka, siku, na saa ya tukio ambalo lilitabiriwa kutokea ili kuonesha haikukisia
 
Jibu swali nililo kuuliza, au hujui ya kuwa katika logic kuna mchakato hufatwa mpaka kufikia hitimisho ?

Sasa pita humo ufikie hitimisho ulilo liweka hapa. Mambo si mepesi kama unavyo yaona.

Mimi nakubaliana navyo si kwa kutumia misingi ya logic sababu najua logic haina uwezo huo. Sasa usinilinganishe mimi na wewe katika kufikiri na kufikia hitimisho mimi ni njia zangu.
Unakubaliana navyo kwa namna gani?

Kwamba havina muundaji?
 
Utawasikia mashabiki wa Kiba wakimsifu eti ni mcha Mungu,mwana bongofleva ni mcha mungu?Waislamu bhana!mtu akishakua na kibaragashia,kanzu tundevu na salamu za hapa na pale kwa kiarabu tayari anapewa jina la ostadh dah!
 
Back
Top Bottom