8Usikimbie hoja kijana maelezo yangu yako wazi sana, umezipata habari za Allah ukiwa tayari upo katika fikra mfu, na ukawa huwezi kuhoji kwa usahihi sababu umekaririshwa namna ya kufikiria kama walivyo fikiria waio kutangulia.
Kuna namna gani nzuri na iliyo bora ya kuhoji zaidi ya kudai uthibitisho?
Mara ngapi humu mmeshindwa kuthibitisha hizi habari?
Au nikupe nafasi ujaribu bahati yako leo pengine hapo kati kati umepata majibu sahihi?
Haya thibitisha Allah yupo
Lengo siyo kusaidia bali lengo nikuweka ukweli wa mambo jinsi ulivyo, kwahiyo ni juu yako kufanyia kazi au kuyaacha hapa hapa. Kwahiyo hili lisikuumize kichwa.
Weka huo ukweli wote tuuone
Ila uo ukweli usiwe na sura ya kihuni maana nitaukataa licha ya kwamba ulishtanguliza self defense
Hii si hoja, vingapi vya hovyo vinafundishika kijana ? Mangapi katika Sayansi umesoma na ni uongo mpaka kesho ?
Uongo wa sayansi au kitu kingine chochote hau justify uongo wa habari za quran uonekane ni ukweli
Umekutwa unaendesha gari rough na hauna leseni, unachukuliwa hatua kwa kutozwa faini we unaanza kusema "Sipaswi kulipa faini kwa kuendesha gari hovyo. Kuna watu wengine wengi mtaani ambao ni wahalifu hatari na wabakaji, na polisi wanapaswa kuwa wanawafukuza, sio kumsumbua raia mzuri anayelipa ushuru kama mimi"
”Kwa kweli, wahalifu mbaya zaidi wapo, lakini hiyo ni suala jingine! Hoja ya msingi yaliyopo ni (1) je, ni kweli uliendesha kwa uzembe, na (2) anapaswa kulipa faini kwa hiyo?
Swali langu la msingi ni wewe uonyeshe ukweli wa unachokiandika.
Tunarudi katika msingi, kuna kauli moja huwa tunaitumia sana inasema hivi "Kila mmoja hudai Laila ni wake, lakini tukimuuliza Laila anakana".
Baada ya kupata habari huwa tunarudi kuzihakiki habari hizo kama alivyo tuelekeza Allah aliye juu ya kuwa "Mnapoijiwa na habari kutoka kwa fasiki, basi zichunguzeni". Hili najua ya kuwa hujawahi kutumia muda wako kuchunguza habari za dini zinazo kufikia zaidi ya kuhoji kitoto. Kwahiyo mimi nilipozipata habari za Ukristo na Yesu nikazichunguza na nikapata hitimisho lililo sahihi.
Its funny
Kwa hiyo wewe vigezo ulivyotumia kupinga mafundisho ya Yesu ilikuwa ni kitabu cha Quran ambacho kinapingana mafundisho ya biblia?
Halafu hoja ya kusema Allah aliyejuu inatakiwa kutumika baada ya kuthibitisha kua hayo maandiko ni kweli ya kwake
Kwani huna habari kua hata kauli ya kusema "huwezi kwenda kwa baba pasipo mimi" ilinukuliwa na Yesu?
Kwa maana hiyo nitakuwa sahihi kusema unakubali kua nukuu hiyo ni maneno halisi ya Yesu?
Kama hukubali kwanini wewe uone ni simple kwa wengine kukubali nukuu unazodai kua ni za Allah?
Hazina ukweli kwa ushahidi wa kiakili, kihistoria na ushahidi wa kimazingira.
Kumbe pamoja na habari kuandikwa kwenye vitabu na kudaiwa vimeandikwa na Mungu lakini bado umevipinga na kuona uzushi
Tunaona kumbe hoja ya kusema vitabu vimeandikwa na Mungu ni kauli ya kilaghai, inawezekana hata hicho kitabu unachokiamini na wewe ni mwendelezo ule ule katika sura tofauti
Inawezekana kabisa kua Quran ni the same thing kama biblia tu kua vyote ni vitabu vya kizushi japokuwa vina nadiwa kuwa ni vitabu vya Mungu
Hili wewe nakupa miaka mia, huwezi kuthibitisha ya kuwa Dini, mathalani ya Uislamu ilibuniwa na mtu, kwa njia yoyote ile.
Wewe nikupe miaka mingapi ya kuthibitisha mbunifu wa maneno haya "demu, wakishua, muziki, disco vumbi, kudanga, kanga moko, "nk.
Miaka 500 itakutosha au michache?
Zina ushawishi ila hazina asili inayofika mpaka kwa Yesu.
Kwa kuzingatia source gani?
Kwahiyo hapa tayari umehitimisha, bila kuonyesha mchakato wa kielimu zaidi ya makisio, kwa mtindo huu lazima useme tu Mola hayupo, yaani unafikia hitimisho juu juu sana.
Kwa hiyo chenye makisio tafsiri yake ni kitu cha uongo?
Quran imeandika Allah alimuumba adam
Tuambie ni tarehe gani ya mwezi gani na mwaka gani ili kuonesha upekee wa Quran kwa kuwa specific
Au tuambie ni lini kwa kutaja saa, tarehe, mwezi, na mwaka ikiwezekana hata majira ya msimu kama ni kifuku au kiangazi tujue muhamad alikwea buraq kwenda anga za juu
Kuna maneno kua Quran imetabili mambo ambayo yanatokea miaka hii tangu iandikwe
Tupe hizo aya ambazo zitaonesha tarehe, mwezi, mwaka, siku, na saa ya tukio ambalo lilitabiriwa kutokea ili kuonesha haikukisia