mbona gari imetoka nje ya nchi na unatumia, mbona simu inatoka nje ya nchi na unatumia, umevaa nguo? Kutoka wapi? Lakini hujanibu swali langu au hulitaki
We jamaa, mbona umeng'ang'ania kusema tulikua Kima? Hivi ni
Nani amekwambia nadharia ya evolution ndiyo nadharia pekee kwenye sayansi. Jifunze, nadharia zipo nyingi.
Haya najibu maswali yako:
1. Maada na nishati zimewekwa na nani?
Jibu: hakuna ajuae. Ndiyo sababu watu wakaamua kuunda mifumo ya imani wakitegemea pengine aliyeviweka yupo na wanaweza kuwasiliana nae.
2. Tukifa hizo maada zinatupa nini?
Jibu: hapa cha zaidi ni kukupa elimu sababu huelewi hata umeuliza nini. Nikuelimishe kuwa hewa, mwili wako na vyakula unavyokula vyote ni maada.
Wewe hapo ulipo ni maada kuanzia vidole, ubongo hadi nywele.
3. Kwanini wengine wagonjwa wengine wazima, wanene,wembamba n.k?
Jibu: miili yetu na miili ya viumbe hai yote inafata DNA zetu.
Ugonjwa na afya ni hali tofauti za mwili.
Kuna muda ukifika utakufa kwasababu seli zako za mwili zinakufa.
4. Kwanini kusiwe na usiku tu bila mchana?
Jibu: Hii ni physics. Ulisoma physics ya advance. Tunaweza kuanza na mjadala wa astronomy, mimi sioni shida.
5. Mbona gari, simu na nguo vimetoka nje ya nchi na natumia?
Jibu: Sijakwambia kutumia vitu toka nje ya nchi si sahihi, la hasha.
Tamaduni, elimu na bidhaa toka kwa wengine si kitu kibaya.
Busara ni kutambua kipi ni mantiki na kipi si mantiki.
Sijasema usisome vitabu, kusoma vitabu ndiyo mwanzo wa maarifa.
Nnachokataa ni wewe kusoma kitabu kimoja tu cha dini na kuamua na kukifata bila kuchunguza upate mantiki na uthibitisho.