Alicho kipost Julius Mtatiro kuhusu wazazi wenye watoto wanaosoma shule za English Mediums

Shule zetu za serikali msiziite Kayumba nyie mabwege, km hmna uzalendo ondokeni ktk ardhi yetu. Mbona UDSM, UDOM, SUA, MZUMBE IFM, IAA n.k hamziiti Kayumba? Mapumbavu sn nyie makenge
Tunaziita kayumba, kwa sababu ya huduma duni, usijiite mzalendo kwa vile huna pesa, Samia, na mawaziri wake nani anasomesha mtoto st kayumba? Usilinganishe shule ya secondary na chuo kikuu/college,
Shule ya skondsri mpo 60 darasani, chuo kikuu mnakuwa 20!, na, chuo kikuu kule kuna "lecturing sio teaching"
Umaskini sio kigezo cha uzalendo, hv kwa vijana kuna mzalendo kama Diamond, je watoto wake wanasoma st kayumba?uzuri wa shule za kisasa,mtoto anakuwa exposed kwa Mambo mengi, ambsyo wa st kayumba atakutana nayo chuo kikuu,
Shule za serikali maslahi ni duni, na waalimu wanaona Bora liende!
Kama, taasisi, za, serikali kama, ttcl,na airtz zipo hovyo, tena huko kuna mishahara minono, je huko primary na, secondary kupoje kwenye mishahara mbuzi!
 
Bora ungeandika kiswahili au kikwenu naona hata lugha ya watu nayo inakutekenya

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Utajiri ni kusoma kutumia lugha ya waingereza? We bado uko kwenye ukoloni wa mwingereza. Hata vichaa waingereza wanaongea kiingereza.
Mtoa hoja ameandika challenge kama kukosa MKOPO na mwisho kaandika Majukumu ya mzazi kuwa mengi kwa wakati mmoja.(soma tena thread).

Hizi alizotoa ni factor za KIUCHUMI. Logic yake ndani ni UMASIKINI na UOGA. Na wala sio Ubora wa Elimu. Ila anafikiri ni Gharama.

NCHI NZIMA bado tuko kwenye UKOLONI(hata wewe ukiwepo), ndio maana Elimu ya Sekondari hadi PhD inatolewa kwa Lugha ya Kiingereza.

Hivyo nashangaa wewe unaona mtoto kusoma Primary kwa lugha ya Kiingereza ni Ukoloni, ila huku level zingine kusoma Kiingereza sio Ukoloni?

Alitakiwa kuleta hoja za Msingi na sio kuleta hoja za KIMASIKINI. Nani alimwambia watu wanataka hio Mikopo?
 
Maneno ya mkosaji haya kupanga ni kuchagua haijalishi matokeo au wapi tutaishia
 
huyo mtoa hoja mwenyewe wanaye wanasoma english medium na wakati wa vikao vya wazazi yeye ndo wakwanza kujifaragua na udiisii wake ili wamuone wa maana, kimsingi hakuna eneo ambalo tunahitaji kuweka nguvu kubwa kama kusomesha watoto, ukitaka kujua tanzania hatujui kitu angalia levels za elimu kwa wenzetu wa kenya na pia hata hustling zao huku duniani, huwezi kukuta nchi ambayo hakuna mkenya wala mnigeria ,hawa wote hawakuogopa shule wala kiingereza, angalia hata graduates kutoka nchi hizo ni mamilioni ukilinganisha na bongo, na kikubwa hawashangai na furasa wanakomaa kweli kweli.
 
Kwa maisha ya Sasa kumpeleka mtoto English medium kuna changamoto Sana kuna watoto wanaanzia ushoga huko na mifano tunaiona mitaani Cha pili unapoteza pesa nyingi mwisho wa siku mtoto anamaliza hamna ajira Cha tatu maisha hayana mwalimu juhudi zako ndio zitakuwa muamuzi wa maisha yako Cha nne unaingia karama kubwa huku ukijua unaenda kukopa kwenye mabenki na vikoba mtoto anarudi masomoni anaanza kugombania Mandazi asubui na wadogo zake hitimisho elimu sio ufunguo wa maisha elimu inakusaidia kuchambua Mambo lakini haiwezi kukupa utajiri
 
Uongo nenda uswahilini Sasa. Hivi Kuna zile shule za chekechekea English Medium za uswahilini vitoto vinaongea kingereza kimenyooka hasa
Sembuse primary ambako masomo yote anasoma kiingereza kuanzia darasa la kwanza Hadi la saba kasoro somo la kiswahili tu .muongo wewe
 
Mzee una maono ya mbali sana...wanunulie viwanja ,wajengee mijengo yao,wakimaliza wakute maisha yamenyooka sio ya kuanzia zero tena.
 
Huyo atakuwa kilaza tu. Tumesoma primary za govt darasa moja lilikuwa na wanafunzi zaidi ya 100. Tulifaulu wote kabla ya ujio wa hizi mnazoziita private schools, tulikuwa tukitema yai vizuri tu,gvt sec schools tumesoma kidato kilikuwa ma zaidi ya wanafunzi 500... tulitoboa mpk chuo kikuu miaka hiyo. Mtaala ndio ule ule wa NECTA tofauti ni lugha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…