Aliniacha kisa ex wake tena anataka kurudi kwangu

Aliniacha kisa ex wake tena anataka kurudi kwangu

Isunji dark

Member
Joined
Feb 22, 2019
Posts
9
Reaction score
9
Wakuu kwanza nikili nimetumia ID nyingine tofauti na ninayotumia.

Kuna dada ambaye nilikutana nae na tukawa katika mahusiano kumbe kipindi nimetoka kumtafuta alikua ameachana na huyo ex wake.

Sasa katika mahusiano yetu tulipendana sana yeye alionyesha kunijali japo sijui rohoni alikua ananiwazia nini, tumekaa katika uhusiano zaidi ya miezi sita bila ugomvi wowote.

Ila baada ya hapo nikaanza kuona tofauti nikamuuliza mbona unakuwa kama mbali shida nini akasema hapana na bahati mbaya baada ya siku kama nne mbeleni mimi ( wezi waliingia nako kaa waliruka fensi na kukaa ndani wakawa wananisubiri nirudi sababu walikua wanajua nafanya kazi za mobile money) na yeye siku nne hizo alikua na safari ya mikoani, nikampa taarifa kuwa nimeibiwa na wameniumiza .

Sasa kipindi naendelea kuuguza jeraha kama wiki tatu mbele nikakuta mesji,
yeye: upo poa
Mimi: nipo poa nambie
Yeye: safi nikwambie kitu ila usinune
Mimi: sawa nakusikiliza
Yeye: i m sorry naona kwangu mda wa kuolewa umefika so nataka kuolewa naomba nisameheme
Mimi:💔

Jana kanitafuta nikachati nae kumbe karudi alikokua yupo nyumbani kwao ambapo pia ni karibu na kazini kwangu, akaja maeneo ya kazi akawasalimia majirani wa pale kwangu hakuja alivotoka jana kanitumia meseji akaa kidogo akapiga simu naomba nisamehe turudiane nilikosea nimejifunza nisamehe sana mi nikamjibu nitakupigia, sasa wakuu nimwambiaje maana nina hasira sana japo alipiniacha sikuonyesha kama nina hasira nae sana nikawa namjibu kawaida sana ila ukweli niliumia sana.Baadhi ya meseji za nyuma na jana
Screenshot_20230803-172805_Messages.jpg
Screenshot_20230803-172356_Messages.jpg
Screenshot_20230803-172440_Messages.jpg
 
Naye akajongea kwa kasi akamfuata mzee baba, akafunga mikono yake kifuani kisha akafungua kinywa chake kumuuliza mzee baba "mzee baba, nilikuwa na mke, binti ya Mgazi kutoka huko usukumani, akaja akaniacha akaridiana na mwanaume wa ukoo wake lakini sasa anataka kunirudia.

Je, yanipasa nifanye nini?" Mzee baba akajibu "Amini nawaambia, amrudiaye ex wake anakitafuta kifo chake kwa mkono wake mwenyewe" kisha mzee baba akapita katikati ya kundi la watu akaenda zake.
 
Jana kanitafuta nikachati nae kumbe karudi alikokua yupo nyumbani kwao ambapo pia ni karibu na kazini kwangu, akaja maeneo ya kazi akawasalimia majirani wa pale kwangu hakuja alivotoka jana kanitumia meseji akaa kidogo akapiga simu naomba nisamehe turudiane nilikosea nimejifunza nisamehe sana mi nikamjibu nitakupigia, sasa wakuu nimwambiaje maana nina hasira sana japo alipiniacha sikuonyesha kama nina hasira nae sana nikawa namjibu kawaida sana ila ukweli niliumia sana.Baadhi ya meseji za nyuma na jana
Brother listen to me very careful, kwa nilivyozisoma hizo meseji kwa mukhtasari huyo ana mtu wake but sometimes huyo mtu wake anampotezea kwa hio anakosa wapi kwa kujishikiza sasa kwako atakuja sababu hana option Ila mtu wake akija anambeba kirahisi tu maana yake ni kwamba huyo ni mtu wa mtu mwingine sio mtu wako au niseme ni mpenzi wa Mwanaume mwingine sio mpenzi wako, kwa hio jiongeze au nasema UONGO my Cute Wife Kapeace Mamndenyi Leejay49
 
Ulikuwa una nini cha kumwambia tena?mbona convo yenu inaonekana mmeimaliza
Nimewahi ongea kwenye simu kuwa kama kaolewa ni yeye huko huko sita tengeneza ugomvi na bwana ake, hata ukisema mwisho leo kupiga simu sita piga tena
 
Brother listen to me very careful, kwa nilivyozisoma hizo meseji kwa mukhtasari huyo ana mtu wake but sometimes huyo mtu wake anampotezea kwa hio anakosa wapi kwa kujishikiza sasa kwako atakuja sababu hana option Ila mtu wake akija anambeba kirahisi tu maana yake ni kwamba huyo ni mtu wa mtu mwingine sio mtu wako au niseme ni mpenzi wa Mwanaume mwingine sio mpenzi wako, kwa hio jiongeze au nasema UONGO my Cute Wife Kapeace Mamndenyi Leejay49
Ndo iko hivyo
 
Mods wanazingua kinoma inamaana kila meseji zangu mpaka wa prove, nipo jukwani mda sana hata hii ID tangu 2019 nilikua situmii sasa mnaniwekaje option za hivo
 
Inaonekana bado unampenda sana na akirudi utampokea. Pole sana mkuu mapenzi ndivo yalivyo na mioyo yetu huwa inatusaliti sana.
Mwambie straight kwamba huyo Mwanamke ana mtu wake sasa kavurugana nae kwa muda tu kakosa option anajiweka kwake kwa kipindi kuna kitu hua mnakiita 'give it a time' to get some fresh air, sasa hicho kipindi kikipita jamaa anarudi kumchukua alafu yeye anaanza upya kusaga meno, hakuna mwanamke hapo aachane nae atafute mwingine km anabisha amchukue atakuja tena na ID nyingine kusimulia kisa kingine na SMS nyingine
 
Mwambie straight kwamba huyo Mwanamke ana mtu wake sasa kavurugana nae kwa muda tu kakosa option anajiweka kwake kwa kipindi kuna kitu hua mnakiita 'give ...
Ok nimekuelewa ukweli alinambia kua alikua na bwana wakazinguana harafu mi nilimkuta wakati yupo na depression baada ya hapo ndo kamrudia tena ila ninahasira nae sana nataka nimfanyie kitu ambacho hata sahau kwa sababu aliniachia maumivu nikasahau tena jana kaanzisha mengine
 
Back
Top Bottom