Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata (CCM) ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mkewe

Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata (CCM) ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mkewe

Kuua mtu kisa amekusaliti ni ushamba mkuu. Unalazimishaje mtu akupende au aendelee kukupenda? Kwanini usitafute mtu mwingine?
Unatakiwa kuelewa kwamba kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na kitu kinachomkwaza au kumtia hasira.

Kwa mfano mimi nikiwa na hasira huwa nakaa kimya, japo kwa asili yangu ni mkimya ila nikiwa na hasira nakuwa mkimya zaidi. Nimeji experience mara kadhaa nikiwa na hasira halafu nikisema ni react, huwa na react violently halafu baadaye naishia kujuta, kwa hiyo nikachagua option ya ku stay calm ili kuruhusu mwanaharamu apite.
 
No, sometimes unakuta ni misunderstanding ndogo tu imetokea hasa kwenye kupishana kauli, unasema nimzabe kofi moja kumbe ndo kwaheri, hayo majuto yake sasa ndo huja baada ya tukio.
Kwanini umzabe mtu kofi? Hadi leo hii kuna watu hawajui kama kofi la mwanaume linaweza kuua? Mwanaume anaemzaba mwanamke kofi anatafuta kwenda jela aisee .
 
Angepotezea tu,

Mie wa kwangu alipozingua 2024 nilimwambia mapema,kuwa ukilala ndani ya nyumba hii nakuchoma moto

Na kweli nilinunua petroli Lita 10,nikawatoa watoto wote nikahamisha vitu vichache

Usiku huo alijiongeza

Hakulala ndani,alilala kwa marafiki zake na kesho akakimbilia Mwanza

Akupindua sana,wiki moja baadae akaanza KAZI ya ubaamedi

Na mpaka Sasa ni baamedi

Nina mwanamke mwingine,na sasa ni mjamzito

Na maisha yanasonga
Kwahiyo ulitaka kumuua mke wako ?
 
Ukiona mwenzio anakuzingua na kukutia hasira,kaa mbali nae hata kwa muda mfupi,toa hizo hasira ulizonazo. Akiwa na tabia zisizovumilika eg dharau, usaliti,unyanyasaji, vunja ndoa kila mtu aishi kwa amani.

Usisikilize maneno ya ndugu, familia, kiongozi wa dini etc anaekwambia" vumilia"unavumilia shida ambazo ziko nje ya uwezo wetu wanadamu eg kuumwa au uchumi kuyumba,hauvumilii ujinga wa mtu anaoufanya kwa makusudi.

Ukute wanandoa walikuwa na migogoro ya muda mrefu ambayo ilibidi waachane ila wakaendelea kukaa pamoja matokeo yake mwanaume akashindwa kucontrol hisia zake ndo yakamfika hayo na nina uhakika hata yeye sasahivi anajutia alichofanya.

Ni hivi: Ukiona red flags, haijalishi uko kwenye uchumba au ndoa, KIMBIIIA, RUUUUN.
 
Huu ni ujinga tulio aminishwa na tukajaa aiseee.... ndoa sio jela mazee
Wakristo wa huku Afrika ndo huwa wanaambiana wavumilie ujinga,huko mambele wanaambiwa kabisa " separate" hata kwa muda mfupi.

Tena wanawake ndo kabisa wanafundishwa mume akikupiga hata kofi usilale nyumba anayolala yeye siku hiyo.

Waafrika tamaduni zetu za kuvumilia unyanyasaji tumeziingiza hadi kwenye dini, nchi nyingine hayo mafundisho ya kuvumilia upumbavu hayapo hata kwenye dini.
 
Kwamba mwanaume akifanya uzinzi ni sawa? Sasa huo uzinzi kwanini anafanya na mwanamke kama hatufanani?

Ili tuone tofauti wasicheat na wanawake. Je, inawezekana?
Mwanaume anafanya uzinzi na nani? na mwanaume mwenzake au? Kama mwanaume kufanya uzinzi ni sawa basi hata mwanamke anaefanya uzinzi na huyo mwanaume nae hana makosa.

Haiingii akilini mwanaume na mwanamke washirikiane kuzini halafu mmoja ahukumiwe na mmoja aonekane hana hatia.

Kama mume wa mtu akichepuka ni sawa, basi na mke akichepuka na mume wa mwanamke mwingine iwe sawa maana mume wa mtu akichepuka hamna shida.
 
Mwanaume anafanya uzinzi na nani? na mwanaume mwenzake au? Kama mwanaume kufanya uzinzi ni sawa basi hata mwanamke anaefanya uzinzi na huyo mwanaume nae hana makosa. Haiingii akilini mwanaume na mwanamke washirikiane kuzini halafu mmoja ahukumiwe na mmoja aonekane hana hatia. Kama mume wa mtu akichepuka ni sawa,basi na mke akichepuka na mume wa mwanamke mwingine iwe sawa maana mume wa mtu akichepuka hamna shida.
Exactly, sio mmoja aonekane mkosefu na kutetewa kwa kisingizio cha binadamu hatufanani..!! Huo ni ujinga wa hali ya juu.

Wote ni wazinzi na wote wanastahili kukemewa..!!
 
Exactly, sio mmoja aonekane mkosefu na kutetewa kwa kisingizio cha binadamu hatufanani..!! Huo ni ujinga wa hali ya juu.

Wote ni wazinzi na wote wanastahili kukemewa..!!
Wanaume wa Tanzania hawataki kusikia hii point,wao mwanaume akichepuka ni sawa lakini mwanamke aliyechepuka na huyo mwanaume kakosea. Nachanganyikiwa jamanii😂😂😂.
 
Back
Top Bottom