Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Mkishindwana achaneni kwa amaniMahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imemhukumu aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto, Dominic Mushi (34) kunyongwa hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe kwa kumnyonga.
Mushi alimuua mkewe Diana Hugo Oktoba 14, 2024 eneo la Kinyerezi Kichangani, lililopo Wilaya ya Ilala.
View attachment 3646458
Diana ambaye alikuwa mfanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Airport, aliuawa kwa kunyongwa na mwili wake ulikutwa kitandani ukitoka damu puani, masikioni na mdomoni.
Katika maelezo ya onyo ya Mushi aliyoyatoa Kituo cha Polisi Stakishari, alidai kuwa kelele za kuomba msaada alizokuwa akizitoa mke wake siku hiyo usiku ilikuwa ni ndoto, kwani mke wake alikuwa na tabia ya kutoa usiku kwa sauti.
Uamuzi huo umetolewa Agosti 7 na Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube, aliyepewa mamlaka ya nyongeza kusikiliza kesi ya mauaji.
Hakimu Makube alisema upande wa mashtaka uliita mashahidi 15 na vielelezo sita kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa, huku mshtakiwa akiwa na shahidi mmoja, ambaye ni yeye mwenyewe.
Hata hivyo, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mahakama ilijiuliza maswali matatu, kwanza kama Diana amekufa kweli.
Pili, kama kweli amekufa, je kifo cha Diana ni cha asili au kimesababishwa na mtu.
"Jambo la tatu, kama mshtakiwa alikuwa na tatizo la afya ya akili, je tatizo hilo lilishughulikiwa ipasavyo kwa kutibiwa? au je limesababisha athari yoyote na kama alifanya tukio hilo, je alikuwa anajitambua? " Alisema Hakimu Makube na kuongeza;
"Mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, imejiridhisha kuwa Diana alikufa na kifo chake sio cha asili bali kilisababishwa na mtu (Mushi), baada ya kukabwa na kukosa hewa," alisema Hakimu
Alisema swali kubwa na la msingi ni kwamba mshtakiwa ndio aliyesabisha kifo cha mke wake na si vinginevyo, hasa baada ya shahidi wa nne na wa sita wa upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa Diana alipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani, lakini majirani walivyotoka na kwenda kumgongea mlango, mume wake alifungua na kuwamabia kuwa mke wake alikuwa anaota.
"Ushahidi unaonyesha kuwa mshtakiwa ndio alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu, pengine yeye ndio angetueleza Diana alifariki kwa tatizo gani" alisema Makube.
Akichambua baadhi ya ushahidi wa upande wa mashtaka, hakimu Makube alisema shahidi wa nne wa upande wa mashtaka, ambaye ni mlinzi wa nyumba hizo alisema kuwa alisikia Diana akiomba msaada na alipofika katika nyumba hiyo, Mushi alimwambia kuwa mke wake ana tatizo la kutoa.
Baada ya kupewa taarifa hiyo, mlinzi huyo alirudi katika eneo lake la ulinzi na baada ya muda Diana aliendelea kupiga kelele, aliomba msaada, hivyo aliamua kumpigia simu mpamgaji mwingine( shahidi wa sita) na kumueleza kuwa Diana anapiga kelele za kuomba msaada.
Mpangaji huyo aliongozana na mlinzi hadi katika nyumba ya Mushi na kugonga mlango, Mushi alifungua mlango na kusisitiza kuwa mke wake ana tatizo la kutoa, hivyo aliwataka majirani hao waondoke mlangoni kwake.
"Baada ya kupitia ushahidi, Mahakama inaona mazingira yote kuwa Diana aliuawa na aliyefanya mauaji haya sio mtu mwingine, bali ni mume wake," alisema Hakimu Makube na kuongeza;
"Kwa kuzingatia hilo, Mahakama inakutia hatiani Mushi kwa kosa la kuua na kwa kuwa adhabu kwa kosa hili ni moja tu, hivyo ni Mahakama inakuhukumu kunyongwa hadi kufa" alisema hakimu Makube
Mimi nimefanya maamuzi ya kumove on. Mke nimishamfuta ktk obolangata na mtima wangu