binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
This is fair, wanawake tumezidi kusemwa jamani wakati kaka zetu kina mdukuzi nao hawako nyuma 😂😂Hamna mistake mbaya hasa kuithaminisha ngono kwa hela na ndio maana mapenzi siku hizi yamekosa maana kabisa.
Mabinti wanaforce wapate wenye hela na wapo tayari hata kuharibu ndoa ya mwanamke mwenzake kwa kutembea na mme wa mtu.Ukija kwa vijana wa kiume siku hizi kuna wimbi la vijana wanaodate na mishangazi ili mradi wapate fedha na hata kijana akitaka kuoa nae analenga (mwanamke mwenye fedha).Wazazi nao nyumbani kila siku wanawambia vijana wao tuletee mtu wa maana,huyo wa maana sio eti mtulivu, mwenye heshima au mcha Mungu bali ni mtu wenye fedha.
So sababu ya fedha mapenzi siku hizi hayana maana, ndio maana uvumilivu hamna na badhi ya ndoa nyingi za siku hizi zimepoteza maana.
Swali langu kila mtu anamtaka mwenye hela, sisi tusio na hela tuende wapi?