Aliyeona mwezi wa Eid atushtue tujiandae

Aliyeona mwezi wa Eid atushtue tujiandae

Kwanza Mimi nakataa.
Tanzania Haina mufti Wala Haina shekhe mkuu.
Huyo ndugu ni Mufti wa BAKWATA na shekhe mkuu wao kwakuwa hapa Tanzania Kuna madhehebu na taasisi nyingi za kidini na kila taasisi Ina jina inalomtambulisha nalo kiongozi wake mkuu.
BAKWATA waliamua kutumia mufti na shekhe mkuu Kisha mashekhe wa mikoa , wilaya na Miata.
Taasisi nyingine hutumia majina kama mwenyekiti, katibu mkuu, amiri au mudiru hayo ni majina lakini majukumu hutegemea na katiba ya taasisi husika.
Pia kutumia neno shekhe mkuu wa Tanzania na mufti wa Tanzania Hilo jina Lina uongo mkubwa sana kwa sababu tunaposema Tanzania maana yake ni bara na visiwani!, Na inajulikana wazi kuwa kule Zanzibar I BAKWATA haipo kabisa Wala hawaruhusiwi kwenda kufanya jambo lolote kule kwa sababu kule Kuna mufti wa Zanzibar ambaye anateuliwa au kuaishwa na raisi wa Zanzibar na kina kadhi wa Zanzibar ambaye wote wawili kadhi na mufti na wasaidizi wao wanafanya kazichini ya wizara ya Sheria ya Zanzibar.
Nachomaanisha ni kwamba hili jina la BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA ni batili kwa sababu linaonyesha kwamba waislamu wa Zanzibar pia wapo chini ya BAKWATA wakati kule Zanzibar haiwaitambui BAKWATA kwa sababu wao wanazo taasisi za kidini zinazosimamiwa na serikali kwa ajili ya uislamu na waislamu wa Zanzibar tu.
Uongo mwingine ni kwamba unaposema kwamba " shekhe mkuu wa Tanzania au mufti wa Tanzania inaonyesha kama vile watanzania wote ni waislamu na Mufti au shekhe mkuu ndiye kiongozi wao.
Nasema hivyo kwa sababu pamoja na kwamba Tanzania inao manaswara wengi sijawahi kusikia cheo Cha askofu mkuu wa Tanzania, au padri mkuu wa Tanzania, mchungaji mkuu nk.
Badala yake utasikia askofu mkuu wa kabisa katoliki Jimbo KUU la dar, au askofu mkuu wa kabisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kkkt, askofu mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, anglikana, wasabato, nk.
Maswala ya askofu mkuu, au padri mkuu wa Tanzania hatujayasikia sasa haya ya kusema mufti na shekhe mkuu wa tz Yana msingi gani na anafanya kazi chini ya wizara gani?!
Sawa sawa ni kusema Mufti na shehe mkuu wa BAKWATA na siyo shehe wala mufti wa Tanzania!
 
kuna shekhe nimemwona pale mwenge mida ya saa 12 anatizama juu kama jogoo sijui kama aliokota kitu angani
 
Back
Top Bottom