Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Naendelea kuwaonya vijana wa kitanzania, msikubali kuvunjwa miguu au kuumizwa kwa namna yoyote ile mkiwapambania wanasiasa wa taifa lenu. Kama umeamua kupambana, pambania kile unachoamini na sio mwanasiasa.

Wanasiasa wa Tanzania ni wachumia tumbo,hawajui itikadi na hawana itikadi. Wanatafuta ugali, ndio maana wataungana na kuwa wamoja pale ugali wao utakapojaribiwa.

Haya,bado wengine wengi wataendelea kuwavunja moyo kwakuwa mliwapambania.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Coment hii kaione kajamaa kamoja humu kanaitwa Mmawia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika vitu vilinifurahisha ni Lowassa na Sumaye kurudi CCM, na leo furaha yangu imezidi marudufu baada ya kusikia huyu domo zege naye kahamia CCM.

Nitafurahi kama Mbowe naye ataachia uwenyekiti wa CHADEMA, maana yeye ndio alileta hizi taka ngumu ndani ya CHADEMA.
Si tulikuwa tukiwaambia mnatuita buku 7

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaja tume huru ya uchaguzi wana ccm woote wanatetemeka kwa hofu
Mpaka Oktoba? Pitia kwenye vituo vya kujiandikisha hivi sasa uone kama kuna hao wanachama wake wapo. Halafu ukitaka kujua hakuwa na watu bali aliwakuta kuwe na tume huru ya uchaguzi kisha uje utoe mrejesho.

In God we Trust
 
Mungu ananjia nyingi Sana za kuwafunua watu wakwamishaji wa mambo ya watu wengini
Chadema katoweni fungu la 10 kanisani muumshukuru Mungu kwa mashinji na kundi lake kuuondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemaliza kila kitu
Utayari wa ccm ameuona baada ya kutemwa ukatibu mkuu? Kazi kweli kweli! Awe mkweli tu kwamba ameona chadema hana ulaji tena! Ilikuwaje akawa ansubiria kuteuliwa tena? Akawadanganye wajinga wenzie akina pole pole!
Screenshot_20200218-153854.jpeg


In God we Trust
 
Mbowe hakustahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, yeye ndio msimamizi na muongozaji wa hawa viongozi wasaka madaraka ndani ya CHADEMA. Tulipiga kelele sana kuwa hakupaswa kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm ili hili kosa lake lipatiwe ufumbuzi na sura tofauti.

Ni nani alikuwa hajui kuwa Mashinji hakuwa kiongozi sahihi wa CHADEMA hasa kwa cheo cha ukatibu Mkuu? Kama katibu mkuu ambaye alikuwa mtendaji mkuu anaondoka chamani na kusema kuwa amegundua cdm haina mpango wa kuletea wananchi maendeleo, hapo mwenyekiti anaendelea kukaa ili iweje?
Nakuelewa sana tindo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kahamia CCM leo.
Mzee Mwinyi hakukosea aliposema "Sote ni CCM ile ile ila sisi ni CCM A na wao (CHADEMA) ni CCM B".

Ukweli ni kwamba CDM ni "chaka" la kutulizia akili la wana CCM wanaokasirishwa na maamuzi ya chama; hasira zikiwaisha wanarejea kwao.

CDM bado ina kazi kubwa ya kuwajenga kiitikadi na kudumisha makada wake. Nadhani wakiachana na itikadi potofu za "mpinzani wa kweli atatoka CCM" na "kubadili gia angani" watafika mbali sana.
Lakini kwa bahati nzuri au mbaya, wakati wana CDM hawajitambui, wana CCM wanatambua udhaifu wao na kuutumia vizuri.

Mathalani, Mzee Lowassa aliwalaghai kwa kauli mbiu ya "CCM siyo mama yangu wala siyo baba yangu" na Mzee Sumaye naye aliwapumbaza kwa "Naenda CHADEMA kujenga upinzani imara".
 
Ninaongea kwa kugonga meza....' kwanza kitendo cha kumfitini katibu wetu mkuu Dr Slaa!'.. mwishowe atajikuta katibu mkuu wake ni mkewe.
Maana sasa Cdm imebaki katika sura ya kifamilia na kishikaji.
Wameuua upinzani wa maana, umebakia upinzani wa ruzuku!

Sent using Jamii Forums mobile app
CHADEMA bado haijatetereka,waliohama wote hakuna aliyekulia ndani ya CHADEMA! Wote ni wageni tu so wasepe chama kibaki clean!Bado CHADEMA kuna hazina kubwa ya viongozi!
 
Another comprehensive repudiation of Chairman Mbowe's epic failure at the helm of CHADEMA. May well be the last nail in the coffin of the party.
 
Back
Top Bottom