Kupatikana kwa hatia kwa aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya kunarejesha upya yaliyotokea chini ya utawala wa awamu ya tano ambapo baadhi ya wataeule wa mwendazake walijiona miungu watu wasioweza kuguswa au kufanywa lolote. Mmojawapo wa hawa wateule ni Paul Makonda au Daudi Christian Bashite aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar. Wapo wanaosema ndiye alikuwa nyuma ya shambulizi dhidi ya Tundu Lissu na kupotea kwa baadhi ya watanzania. Je ni kweli kuwa Sabaya ndiye alifanya ujambazi peke yake wakati Makonda alitenda zaidi? Je ni lini Makonda atepewa haki yake kwa kushushiwa hukumu anayostahili? Leo tuanze na Makonda kujua ni lini mamlaka zitamnyang'anya uungu mtu wake? Tukimpata Makonda, tunaweza kuwajua hata wale watu waliojulikana kama watu wasiojulikana wakati wanajulikana?