Wakuu Kwema!
Kuomba msamaha ni ushujaa, msamaha ni neno la kijeshi katika mapambano.
Unapomkosea mtu akawa na uchungu na wewe basi jua kuwa ipo siku yako, Kama sio wewe basi moja ya kizazi chako.
Upepo unavuma, wenye macho haya tuliyaona miaka mitatu minne iliyopita, tuliandika na kuonya hasa Wale waliojitia Wana nguvu ambazo kimsingi hawana,
Nilishawahi kuandika na Leo narudia, ukipewa Cheo chochote iwe ni Urais,Uwaziri, u-IGP au Cheo chochote kile usije ukadhani wewe ni Mkubwa, huna ukubwa wowote, huna lolote,
Siku zote mkubwa ni yule atendaye haki, apendaye maagizo ya Mungu, mwenye upendo, asiye na fitna na hila, asiyeua wala kumwaga damu za watu wasio na hatia.
Vile unavyotumia nguvu kuonea watu, na kuwatesa watu hasa wasio na hatia ndivyo hivyo hivyo Mungu atatumia nguvu kukuonea na kukutesa.
Vile watoto wa watu ulivyowaua na kuwaangamiza wanavyoteseka, ndivyo hivyo hivyo watoto wako na kizazi chako kitakavyo Tessa na MUNGU.
Kila siku nasema Mungu ni mwaminifu, ana Haki. Huwezi Tesa watu alafu ati uishi Kwa Raha, haijawahi tokea na kamwe haitatokea. Ni suala la muda tuu.
Mungu hajakupa Cheo ili utese watu, Ili uwadhulumu watu, ili uwavuruge watu wake.
Kaka yangu, Kama utanisikia naomba uzingatia haya, tafuta uliowakosea Kama wapo, uwaombe Radhi, Watafute Kwa muda wako,
Usiende kuomba Mungu msamaha, huko unaenda kupoteza muda wako, Mungu haombwagi Msamaha,
Upepo unavuma, bendera uelekeo unaenda mashariki.
Kaka yangu ni Bora Mungu akulipe wewe kwani wewe ndiye uliyekosea kuliko kukuacha wewe na kuhamishia kipigo kwenye kizazi chako.
Kaka yangu.
Bado hujachelewa. Tafuta uliowakosea uwaombe Radhi kuanzia mwakani 2022 mpaka 2025 utakuwa katika vita mbaya na Mungu Mkuu.
Nimekuambia mapema ili ujihami Kwa kuomba Msamaha Kwa uliowakosea ili Mungu aghairi.
Vinginevyo Mungu atakuwa mwaminifu kwako Kwa 100% kukutesa Kama ulivyofanya.
Mimi mdogo wako;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro