...Najaribu kuwa free thinker! kwa miaka mingi nimekuwa nikisia Mzee Lowasa, Kinana na kwa hivi karibuni Kikwete ilifikia wakati kijana wa Kikwete huyu naibu waziri kila kituo kipya cha mafuta kilichofunguliwa ilisemekana ni chake! Loawassa aliwahi kuwapa challenge Chadema kipindi kile wamemshikia bango kuwa ni fisadi, aliwaomba kama kuna mwenye ushahidi aende mahakamani, huyu Kinana aliwahi shutumiwa na Mchungaji Msigwa kuwa meli yake ilikuwa imebeba mankotena ya meno ya tembo, Kinana akaenda mahakamani na mahakama ikaona Msigwa ameshindwa kuthibitisha madai yake na ikamuamuru alipe fidia, aliishia kumuomba radhi Mzee Kinanan hadharani! Sasa hizi tuhuma za ufisadi zina ukweli kiasi gani au ndio mambo ya kurithishana habari za kufikirika!