Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazo wahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Hivyo kasema Wanapaswa kutoka nje Zinapojadiliwa Wizara Zisizoihusu Zanzibar.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Hivi huyu jamaa hawa Wazanzibar walimkoseaga nini??
Maana ye kila siku ni bifu nao tu
 
Safi sana kessy wape asa vidonge vyao, wajinga ndo waliwao kinachowapa kuungangania muungano nkitu gani
 
ni lini Zanzibar walisema wanataka Muungano na Watanganyika ?
nashangaa Nyerere alivyokimbilia Zanzibar kufunga mkataba wa Muungano..
Mmesahau mlivyokua mkiingia Zanzibar kununua bidhaa ?
sasahivi hela za bandari ya Zanzibar mkusanye nyinyi, utalii mkusanye nyinyi, foreign exchange kutoka Zanzibar mkusanye nyinyi , misaada ya UN, FIFA iishie kwenu..
makusanyo hayo kutoka Zanzibar mnaingiza kwenye mfuko wa Muungano kuendesha miradi ya bara na Zanzibar kuambulia mazombie ya askari kutoka bara ili kuwadhibiti...
mmeizuia Zanzibar hata kujiunga na OIC ili isinufaike..
MBONA HAMUITISHI REFERENDUM ili Wazanzibar waamue kama wana hata shauku ya kuungana na machogo.
Katiba ya Warioba ndio jibu. Hata wabunge wa CCM wanalijua, ila kwa uoga wao walishangilia kura ya wazi huku hawaipendi. Mungu yupo tutaelewana karibuni
 
Hivi huyu jamaa hawa Wazanzibar walimkoseaga nini??
Maana ye kila siku ni bifu nao tu
Kuna dada yake alikaa uke wenza na mwanamke wakizanzibari.
Ndio maana anamsaidia dadaake kulia wivu.
Nashukuru Makamba kamkataa huko nyuma nimesema aina ya ruhusa sheria ya kuruhusu aina ya kupata viongozi aina kesy ni tatizo.
Kiongozi hajui hata katiba ya chama chake wala itikadi na misimamo ya chama chake sijui ni kiongozi waaina gani huyu.
 
Kessy anawaambia ukweli, ahsante sana. Tumechoka
Nani wamechoka wabara au wa-zanzibari ? wa-znz ambao munawapandikizia mpaka raisi? ambao mnawanyima uhuru wa kuchagua hata kiongozi wamtakae ? ambao wakiamua kuchagua kiongozi wanaeamini atawatoa katika janga na unyonge wa kutawaliwa na mkoloni mweusi munawaletea jeshi na kuwababikiza kesi za uwongo ? amboa hawana haki yoyote ya kujiamulia mambo yao bila ya ridhaa ya serikali ya tanganyika? nani hasa kachoka hapa?
 
ni lini Zanzibar walisema wanataka Muungano na Watanganyika ?
nashangaa Nyerere alivyokimbilia Zanzibar kufunga mkataba wa Muungano..
Mmesahau mlivyokua mkiingia Zanzibar kununua bidhaa ?
sasahivi hela za bandari ya Zanzibar mkusanye nyinyi, utalii mkusanye nyinyi, foreign exchange kutoka Zanzibar mkusanye nyinyi , misaada ya UN, FIFA iishie kwenu..
makusanyo hayo kutoka Zanzibar mnaingiza kwenye mfuko wa Muungano kuendesha miradi ya bara na Zanzibar kuambulia mazombie ya askari kutoka bara ili kuwadhibiti...
mmeizuia Zanzibar hata kujiunga na OIC ili isinufaike..
MBONA HAMUITISHI REFERENDUM ili Wazanzibar waamue kama wana hata shauku ya kuungana na machogo.

Maneno chungu nzima na malalamiko yasiyo na mshiko, hivi kati ya Rais Nyerere na Rais Karume nani alikuwa anataka waungane haraka haraka ili kujihakikishia usalama wake binafsi na nchi yake - jibu unalo.

Kama ujapata jibu nataka nikukumbushe kwamba bila ya msaada wa Mzalendo Baba wa Taifa basi Sultani Jamsheed angerudi Madarakani kiulaini na kuendeleza udhalimu wake wa kisultani - nyinyi mgemfanya nini kama angekuja na jeshi la kukodi, hilo hamlikumbuki.

Madai yote unayo lahumu Serikali ya muungano asilimia kubwa hayana mshiko, baadhi yenu mnataka kutafuta sababu ya kuvunja muungano - njama zenu zitagonga mwamba kutokana na Wazanzibar wengi kutounga mkono ndoto zenu za mchana.
 
Nadhani huyu ni mbunge wa tatu katika bunge hili kuwakemea wazanzibari- J. Makamba, Prof. Tibaikjuka na sasa huyu hapa. With fairness Tanz bara tumejitahidi kuwa kimya na kuwavumilia Wazanzibari, lakini kelele zao za hoja ya kuonewa zimekuwa too much. Nenda ofisi ubalozi wowote Tzn nchi za nje, wafanyakazi wengi ni Wazanzibari. Lakini kila siku tunasikia hoja ya kunyonywa. Let's call it quit.
 
Sioni mantiki yake wakati wenyewe ndio wanaoshupalia serikali mbili.
 
Mi sikuwahi kuwapenda wabunge wanaotokana na CCM kwa kuwa huwa hawajui kujenga hoja za maana zaidi ya kusubiri kuunga mkono hoja kwa kuegemea Chama chao kana kwamba Serikali inatumia mfumo wa kibunge (parliamentary system). Hata hivyo nimekuwa nikiliwazwa mara kwa mara kwa uropokaji mzuri wa Mbunge Kessy hasa dhidi 'ego' za wazanzibar ambao wanajidai wanataka uhuru baada ya kugunfua kuwa wana rasilimali ya mafuta. Go bhana Kessy utupe raha hata kidogo mana hatuwezi kuipata kwa wanaccm wenzako.
Hivi wanaolazimisha Muungani ni wanzanzibari au ni wabara?
 
Nani wamechoka wabara au wa-zanzibari ? wa-znz ambao munawapandikizia mpaka raisi? ambao mnawanyima uhuru wa kuchagua hata kiongozi wamtakae ? ambao wakiamua kuchagua kiongozi wanaeamini atawatoa katika janga na unyonge wa kutawaliwa na mkoloni mweusi munawaletea jeshi na kuwababikiza kesi za uwongo ? amboa hawana haki yoyote ya kujiamulia mambo yao bila ya ridhaa ya serikali ya tanganyika? nani hasa kachoka hapa?
Hao walioko madarakani huko znz ni Watanganyika?
 
Huyu mbunge ana asili ya Tipu Tipu. Hivyo ana ona uchungu nduguze wa Znz kuijidhalilisha na Tanganyika. Anafahamu vizuri sana kuwa hawa wamedhibitiwa.
Anacho fanya ni kujaribu kuwamsha hawa ccm znz ambao ni hawana hisia na znz zaidi ya kulinda maslahi ya matumbo yao.
Hii njia ani tumia kwa ujanja ..anawatia hasira dhidi ya Tanganyika...ili waaamke wadai chao...hivyo anafanya kwa ustadi kuwasaidia
Hapaana! anawaambia ukweli
Hao wznz wako Dodoma hawajui gharama za uwepo wao
Huku bara wanakuja Zaidi ya 80, BLW wapo 50.

Wanataka nafasi za ubalozi, hivi SMZ inachangia nini katika kuendesha balozi 21 zilizopo.

Kama wanataka nafasi za ubalozi, basi waombe kugharamia balozi watakazokuwa na balozi mzanzibar. Siyo watake vyeo wakimbie gharama

Kessy kaongea ukweli, mambo yasiyowahusu wanayaongelea yanawahusu nini?

Wanalalamika mgonjwa hakutibiwa na JMT, kwani wizara ya afya ni suala la muungano!

Wanadai nafasi za muungano sawa, hivi znz yenyewe inatoa ajira za muungano ngapi
Halafu wamejazana katika maeneo yasiyowahusu kama wizara zisizo za muungano

Wanataka mgao wa 4.5 wakati huo huo wanataka na kile kisicho cha muungano

Kessy kawaambia ukweli, wakati umefika tuwaambie ukweli.
Muungano ni gharama tushirikiane, si eneo la kuzalisha ajira au kutoa mafao kwa znz.

Znz ili iwe na heshima ni wakati sasa wakiongelea muungano wasidai tu watuambie na eneo gani wanasaidia. Tumechoka kusikia madai tuu hakuna mchango wowote

Hiyo 4.5 ni pato la Tanganyika, bado wanataka na inasikitisha wanataka kugawana sawa
Wakiambia wenzetu mnaleta nini mezani, wanakimbiaa. Utegemezi huu unachosha

Kwakweli afadhali amepatikana mwenye uchungu na kodi zetu

Watu milioni wanachukua sehemu kubwa sana ya kodi zetu. Hivi Dar na znz zina ulinganifu kwa jambo gani kiasi znz ipate takribani mara 20

Ahsante Kessy, Ahsante sana. Wakiwa Dodoma watulie na kusubiri watakacho zawadiwa,
 
Poleni wabunge kutoka znz hasa wa ccm
Huo ndio ukweli
CCM walivyo wa ajabu watadhani kwamba hii inawahusu CUF tu huko Zanzibari wanadhani wao ni wa bara hahahahhahahaaa hutawasikia wabunge wa ccm toka Zanzibar wakikemea hili badala yake wataungana na huyu mbunge yaani ccm Zanzibar wanachekesha sana
 
Huyu mbunge Kesy huwa anawaumbua sana kisiasa Wazanzibari.
Anatoboa yale ambayo ni dhahiri.
Sijaona mbunge wa CCM mwenye uthubutu wa kusema ukweli kama mheshimiwa Kessy. Tangu nimahamu sijawahi kumsikia akichangia pumba, siku zote pointi zake zina mantiki.

Nina imani mtu kama Kessy angekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano, migogoro ya muungano wetu ingepata ufumbuzi wa kudumu.
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazo wahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Hivyo kasema Wanapaswa kutoka nje Zinapojadiliwa Wizara Zisizoihusu Zanzibar.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Kwa kweli! Hivyo kwenye Bunge la Katiba alikuweko? Mchango wake ulikuwa je? Maana naona anachepuka kabisa kutoka kwenye msimamo wa wakubwa zake.
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazo wahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Hivyo kasema Wanapaswa kutoka nje Zinapojadiliwa Wizara Zisizoihusu Zanzibar.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Ha ha haaa huyu jamaa itakuwa walimnyima mkr huko visiwani
 
Hii ni Mara ya sita ndani ya miaka 4 tu Mbunge kessy anajitoa mhanga kueleza ukweli.
Wanaofahamu vizuri wanajua anachoongea ni sahihi ILA hawataki kumsikiliza au kumwelewa.
Naona naye ameanza kupamba hoja zake kwa maneno ya "kuudhi" Ili apate kusikika.
Ni kihoja kukuta Mbunge wa Zanzibar anahoji utendaji wa Wizara ambayo si ya Muungano.
Ipo siku ataeleweka.
ILA Kessy punguza maneno ya kuudhi
 
Hapaana! anawaambia ukweli
Hao wznz wako Dodoma hawajui gharama za uwepo wao
Huku bara wanakuja Zaidi ya 80, BLW wapo 50.

Wanataka nafasi za ubalozi, hivi SMZ inachangia nini katika kuendesha balozi 21 zilizopo.

Kama wanataka nafasi za ubalozi, basi waombe kugharamia balozi watakazokuwa na balozi mzanzibar. Siyo watake vyeo wakimbie gharama

Kessy kaongea ukweli, mambo yasiyowahusu wanayaongelea yanawahusu nini?

Wanalalamika mgonjwa hakutibiwa na JMT, kwani wizara ya afya ni suala la muungano!

Wanadai nafasi za muungano sawa, hivi znz yenyewe inatoa ajira za muungano ngapi
Halafu wamejazana katika maeneo yasiyowahusu kama wizara zisizo za muungano

Wanataka mgao wa 4.5 wakati huo huo wanataka na kile kisicho cha muungano

Kessy kawaambia ukweli, wakati umefika tuwaambie ukweli.
Muungano ni gharama tushirikiane, si eneo la kuzalisha ajira au kutoa mafao kwa znz.

Znz ili iwe na heshima ni wakati sasa wakiongelea muungano wasidai tu watuambie na eneo gani wanasaidia. Tumechoka kusikia madai tuu hakuna mchango wowote

Hiyo 4.5 ni pato la Tanganyika, bado wanataka na inasikitisha wanataka kugawana sawa
Wakiambia wenzetu mnaleta nini mezani, wanakimbiaa. Utegemezi huu unachosha

Kwakweli afadhali amepatikana mwenye uchungu na kodi zetu

Watu milioni wanachukua sehemu kubwa sana ya kodi zetu. Hivi Dar na znz zina ulinganifu kwa jambo gani kiasi znz ipate takribani mara 20

Ahsante Kessy, Ahsante sana. Wakiwa Dodoma watulie na kusubiri watakacho zawadiwa,

Kusema Znz hawachangi ni ujinga. Wao pia wanachamgia sana tu. Kuhudu mgawanyo upo kikatiba wamekubaliana na badi nchi hixi xipo mbili...ndio maana znz wanaendesha serikali yao na uchumi wao.
Ni ujinga mkubwa syi znz hawachangii ...ni upumbavu wa hali ya juu.
Idara zote za muungano fedha zinazokusanywa zinaingia hazina. Mfano wa hizo ni
Viza..hii inaingia bingo na hakuna mgao
Kodi za aviation licence hata zikisajiliwa znz
Posta
Simu . Hixi simu ndio zinaingiza mapato makubwa ..hixi fedha zake xote xinaingia muungano...makampuni ya simu yakilopa yanaingia hazina..sasa hata zile za znz wakitumia kodi zinakuja bara
Fedha za madini na gas ni ya muungano hivyo mnapouza vitalu kule znz frdha mna hukua bongo
Kodi sa customs
Vat yote
Wapemba kariakoo wapo hapa na wanachangia
Licence za mabenki
Licence za bima
Hizi zzote hata zikiwa kule visiwani fedha zinaingia bongo.hivyo wana changia vya kutosha ....ndio maana nikakwambia huyu ana asili ya kiarabu anafungua macho ccm znz waache uhjinga ...nchi yao inateketes kutetea muungano usio na maskahi
 
Ndugu yangu, wakati wa bunge la katiba, gavana wa benki kuu aliwahi kusema Zanzibar haichangii muungano. Hakuna mzanzibar aliyesimama kupinga hilo.

Pili, kutuambia wapemba karikoo wanachangia, kunatupa uvivu kujadiliana nawe
Hata hivyo tuna wajibu wa kutoa elimu ya umma. Makampuni ya simu yanachangia si kwasababu ya znz. Zantel si walikuwa znz nini kiliwahamisha? Lazima utambue ukubwa wa soko. Hayo mengine hayana sababu za kujibu maana ni ya kiwango chako, si chetu

Labda nikuambie usiyo yajua kidogo. Wizara zote za muungano znz haichangii hata senti.
Zanzibar haina bajeti za wizara za ulinzi na usalama ambazo ni kubwa ka taifa lolote
Wizara ya mambo ya ndani ambayo ni kubwa kwa taifa lolote
Wizara za muungano na taasisi za muungano

Zanzibar inapewa bajeti sapoti kutoka hazina Tanganyika. Hazina hiyo haina mchango wa znz
Znz inapewa 4.5 ya pato la Tanganyika, kwamba bila kufanya chochote pato la Tanganyika likiongezeka znz inapata mgao mnene.

Ukisikia mabilioni ya kodi yanakusanywa Tanganyika znz ina 4.5% yake hapo

Hao wabunge wanaokuja Dodoma, wanabeba mifuko tu.
Hawahudumiwi na SMZ. Gharama na huduma zao ni za Tanganyika.

Pamoja na mgao huo, tunasikia watapewa tena 4.5 6 ya benki kuu.
Hiyo nayo inategemea uchumi wa Tanganyika

Wanapewa asilimia za mikopo na misaada. Mikopo hiyo ni mzigo wa Tanganyika
Kwamba wanapewa mgao, hawajui deni wala ukubwa wake

Utashangaa Kodi za Tanganyika kupitia mfuko wa elimu HESLB zinafadhili wanafunzi wengi wa znz kuliko ZHESL. Wakati wanafunzi wa znz wakilazimika kurudisha mikopo ZHESL wanafunzi wa ZNZ waniopewa HESLB hawarudishi.

Kumbuka znz imeshapewa mgao wake, vipi ipewe tena HESLB za Bureee! bila kurudisha?

Na ni kwa hesabu au sababu gani inapaswa kupewa pesa hizo.

Kuhusu utumishi, ajira za muungano zinatengenezwa Tanganyika si znz.

Lakini pia kupitia Tanganyika wapo wznz ndani ya maeneo yasiyo ya muungano.
Kupewa mgao wa PAYE ni zawadi, znz haina ajira wanasaidiwa

Muhumi,wazanzibar wasiwe watu wa kudai tuu, tunataka kuwasikia wakichangiwa mawazo ya kuimarisha uchumi ambao wao ni wanufaika kuliko eneo lolote la JMT.

Tunataka wznz wawajibike kwa watu na taasisi zao.
ZHESL ichukue dhamana ya wanafunzi wake. Ada za taasisi zao zilipwe na SMZ.
SMZ ihudumiwe wabunge wake wakija Dodoma, na wasishiriki mambo yasiyowahusu

Lakini pia wakiongelea muungano hatupendi bla bla bla za vocha za simu.
Tunataka tuwasikie wakitueleza wao wanachangia nini katika muungano kwa namba

Wakitaka usawa wa mabalozi(hoja ya kitoto sana) basi waombe kuhudumia balozi hizo.
Si kutaka nafasi za ubalozi wasizojua gharama zake

Wznz wanataka na kudai kwasababu hawajui gharama za muungano, tunataka wawajibike kwa michango ya wazi si kusikia hoja za mabalozi

Hongera mbunge Kessy kwa kuwaambia ukweli mchana. Tumechoka jamani
 
Back
Top Bottom