Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Kumbe CCM bado ni chama pumba kabisa kama wanajijua kuwa hakuna mwingine ndani yao anayeweza kmrithi Magufuli. Hoja hii iliwahi kutolewa wakati wa utawala wa Mwinyi ikafyekelewa mbali kabisa na maisha yakenda vizuri sana na huenda ndiyo maana leo tuna huyu Magufuli. Ukishaanza kubadili vifungu vya katiba kumfurahisha aliyeko madarakani leo, utaruhsu mwehu mmoja kubadilisha katiba yote na kusema yeye ni rais wa maisha. Aliyeingia madarakani kwa katiba fulani ataondoka kwa katiba hiyo hiyo hata kama kutakuwa na ammendments kwenye katiba hiyo, ammendements hizo hazitamuhusu yeye. demkrasi huagiza kuwa utatwala kulingana na katiba iliyokuweka madarakani, siyo iliyokuja baada ya wewe kuwa madarakani
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja ndugu watanzania tujipinge kisaikolojia kuwa muda wowote sheria inaweza badilishwa na kuongezewa muda wa uongozi wa Mh JPM. Mimi binafsi naunga hoja kwani kwa kipindi cha miaka mitano aliyokaa madarakani amefanya makubwa sana kwa hiyo naamini akipita muda wa kutosha atabadilisha sura ya tanzania na na nchi ya maziwa na asali wa watz wote sio watz wachache kama miaka iliyopita.
 

Attachments

  • 0CF9A1FE-89B5-44F7-A3C0-A01D913999FC.jpeg
    76.4 KB · Views: 5
  • B23C21B7-6663-4640-8C3A-A243689777D2.jpeg
    84.1 KB · Views: 5
Patachimbika
 
Acheni upuuzi akifa?
 
Ikiwa CCM ndio wataamua mwenyekiti wao alendelee kuwa JPM na mgombea wao aendelee kuwa JPM wewe unaumia nimi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…