Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Kumbe CCM bado ni chama pumba kabisa kama wanajijua kuwa hakuna mwingine ndani yao anayeweza kmrithi Magufuli. Hoja hii iliwahi kutolewa wakati wa utawala wa Mwinyi ikafyekelewa mbali kabisa na maisha yakenda vizuri sana na huenda ndiyo maana leo tuna huyu Magufuli. Ukishaanza kubadili vifungu vya katiba kumfurahisha aliyeko madarakani leo, utaruhsu mwehu mmoja kubadilisha katiba yote na kusema yeye ni rais wa maisha. Aliyeingia madarakani kwa katiba fulani ataondoka kwa katiba hiyo hiyo hata kama kutakuwa na ammendments kwenye katiba hiyo, ammendements hizo hazitamuhusu yeye. demkrasi huagiza kuwa utatwala kulingana na katiba iliyokuweka madarakani, siyo iliyokuja baada ya wewe kuwa madarakani
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja ndugu watanzania tujipinge kisaikolojia kuwa muda wowote sheria inaweza badilishwa na kuongezewa muda wa uongozi wa Mh JPM. Mimi binafsi naunga hoja kwani kwa kipindi cha miaka mitano aliyokaa madarakani amefanya makubwa sana kwa hiyo naamini akipita muda wa kutosha atabadilisha sura ya tanzania na na nchi ya maziwa na asali wa watz wote sio watz wachache kama miaka iliyopita.
 

Attachments

  • 0CF9A1FE-89B5-44F7-A3C0-A01D913999FC.jpeg
    0CF9A1FE-89B5-44F7-A3C0-A01D913999FC.jpeg
    76.4 KB · Views: 5
  • B23C21B7-6663-4640-8C3A-A243689777D2.jpeg
    B23C21B7-6663-4640-8C3A-A243689777D2.jpeg
    84.1 KB · Views: 5
Patachimbika
ccm tangu uhuru imekuwa ikibadili marais kwa mafanikio wote wakiiacha nchi salama salimini.Ni nini kilichobadilika mpaka mnatuambia hamuoni mtu wa kumrithi Magu?Je ndio mwisho wa kufikiri kwenu?Ni nini kimetokea kwa chama hiki kikongwe mpaka watu wanasema hadharani bungeni kwamba hawaoni mtu wa kumrithi Magu ndani ya chama chao?Ni kweli au ni kikundi tu cha wabinafsi fulani ccm wanataka kumshawishi Magu kwa ajenda zao binafsi?Je,ccm ya leo si ile ya zamani?(yenye tunu kibao).Ccm ya leo haina candidates wa urais isipokuwa mtu mmoja tu?Kama ni hivyo mtuambie tuma sababu gani ya kuachia chama mufilisi kama hichi (kinachotegemea mtu mmoja) kiendelee kushika madaraka?Hamuoni chama chenu kilivyo hatari kwa ustawi wa taifa?(chama cha mtu mmoja)e.Si haya mnayompigia kelele Mbowe kila kukicha?(kwamba aachie madaraka ya chadema kwa watanzania wengine)?Sasa na nyie mnafanya nini hapo?Hivi watanzania mmekumbwa na uchizi wa aina gani lakini?Mbona ile jamii ya watu wenye uwezo wa "kawaida tuu"(si lazima uwe jinias) wa kufikiri inaondoka kwa kasi hivi?You know kama kuna jambo nampendea sana Magu ni hili,ameweza kuwabana watu hadi rangi halisi za kinafiki za watz zinaonekana.Hata wale tuliodhani ni wazito kumbe ni wepesi hivi!From Ally Keissy wa ccm,Edo Lowasa hadi Lijualikali wa chadema woote tumeona rangi zao halisi.Namshukuru sana Magu kwa hii legacy.Ametusaidia kujua rangi halisi za wabongo baada ya kuapply hii staili yake ya uongozi wa kibano kikali.Sasa watu tusiowadhania wanaimba mapambio ya ajabu!Inatusaidia katika kuchagua na vetting ya viongozi mbalimbaliNext time i think we will be careful because KUMBE MKO HIVI JAMAAANI![emoji34]
 
Kwa sasa hivi bado ni mapema kumuongezea Raisi Magufuli muda, kwa maoni yangu akikamilisha 2 000 MW, phase zote za Mwendokasi na SGR iwe imeshafika Dodoma/Manyoni hapo sasa kuna hoja kwamba asimamie na kukamilisha hivyo bado ingawaje anaelekea vizuri, ...
Acheni upuuzi akifa?
 
Spika...." Hata asipotaka tutamwongezea ... .Mh.Kesy nina imani sote tutarudi weka moyoni bunge lijalo tunamaliza..." mjengoni 9/6/20
Amefanikiwa kujenga hofu na kukidhiti chama.Ajabu karibu wabunge wote ccm wanatarajia hisani ya mkuu katika uteuzi.Ni aibu na fedheha wanavyomtukuza mkuu zaidi ya Muumba.
Ikiwa CCM ndio wataamua mwenyekiti wao alendelee kuwa JPM na mgombea wao aendelee kuwa JPM wewe unaumia nimi mkuu.
 
Back
Top Bottom