🙂🙂 namshukuru Mungu kwamba sipo labelled hivi na jamii inayonizunguka. Hata wewe tukikutana leo utabadilisha msimamo huu. Bado naamini nilifanya jambo jema, kosa ni kuniacha bila kukaa chini na kujadili kwa pamoja then anarudi anataka mimi niombe msamaha kwao.ujue maisha ni safari ndefu sana!
Mleta uzi ni type ya wale watu wana overconfidence
watu wenye kujiskia flani hivi kwamba maisha wameyapatia kwahiyo huyo mwanamke ni kama kuwa nae ulikua unamsaidia tu. ( ndio mana maamuzi yako ni sheria)
Wewe ndo wewe yani ...
matendo ya huyo dada yanakuongezea utukufu zaidi...[emoji1]
ni jamii ya watu wenye shida kwenye makuzi yao, inayopelekea upungufu wa Busara
MshengaKwani uliahidi kutoa mahali Kwa mshenga na wazazi wake Au uliongea na huyo mchumba ako wawili tu?
Rejea references zako tena na uje kwa justifications zilizoshiba.kwenye maisha inatakiwa emotional quotient (EQ) mtu asie na EQ basi IQ haina maana
Nimelelewa kwaa baba na mama. Washika dini hasa. From a lovely family,,,Mkuu kuna. watu hawajui kuomba samahani hata kidogo,yani anaona akiomba msamaha ni ujinga ndo type ya huyu Sasa,yani anaona kila a na achofanya yupo sahihi,lakini pengine hata malezi yanachangia,yawwzekana huyu ni wale waliolelewa upande mmoja,sidhani kama angetoka kwenye familia inayoelewka angefanya hivyo,kwani hata wazee wake wangemshauri.
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.
Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.
Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.
Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Tuwe wakweli tu mkuu unadhani angekuwa na jamaa anaemwona anamwelekeo angerudi? Mater fact kashajaribisha mahusiano mengine kaona hayafanyi kazi sasa atarudije kwa mwana inambidi aombe msamaha na sababu mahusiano ya watanzania wengi yanaendeshwa na ndugu ni wazi ndugu ndio walimwambia ampige chini jamaa hafai atafute mtu mwingine sasa ili waweze justustify kwamba wamerudiana kwenye mahusiano jamaa inabid awaombe ndugu msamaha...mbona hesabu rahisi hizi.. Mwanamke kashindwa kwingine kaamua kurud sababu wewe ndio last resort basi. Watakuja wanawake hapa watapondea hii ishue ila nimesoma koment zao nyingi wao ndio wakwanza kumshangaa mwanamke mwenzao anawezaje kufanya alichokifanya meaning kwamba wanakuaga na option nyingi mwanamke mwenzao anakosaje mtu mwingine kama wewe umefanya kosa kama hilo wanamshangaa karudije kwako sasa basi jibu lake hawawez kukupa mimi nakupa jibu AMESHINDWA KWINGINE WEWE NDIO OPTION YA MWISHO, na ishue ya wanawake na desperation ya ndoa huwa nashindwa kuielewa...soma kwa makini sana comments za toughlendon_1
wengine hao wanakupoteza uyakanyage, huyo mwanamke karudi sababu hana options nyingine
Jamii forums ni jukwaa huru. Si kwa ajili ya wakomavu pekee. Hata sisi ambao hatujakomaa kupitia mawazo ya wengine tunajifunza. Kuwa mwanaume hakunifungi kusikia hoja za wengine.Mwanaume kuomba omba ushauri hata Kwa mambo madogo ni dalili ya kuwa hajakomaa.
Ukisha-cancel kitu au aki-cancel MTU kitu huna haja ya kukirejesha
Vyema sana..Wote mnaomponda mshkaji kwa kumsaidia jamaa yake hamna akili, kuna baadhi ya marafiki ni bora kuliko ndugu hata mimi ingetokea situation kama hiyo kwa jamaa flani ningefanya ivo ivo, mnaosema mke atakusaidia siku unamatatizo inamaana hamjui kuwa kuna wanawqke hukimbia familia kipindi cha shida?
Jamii forums ni jukwaa huru. Si kwa ajili ya wakomavu pekee. Hata sisi ambao hatujakomaa kupitia mawazo ya wengine tunajifunza. Kuwa mwanaume hakunifungi kusikia hoja za wengine.
nakaziaKama Jambo Dogo kama hilo linakushinda mpaka uombe ushauri, ni bora usubiri Akili ikomae ndio uingie ndoani, maana Kwa Akili hizi ndoa itakushinda mapema Mno.
Mtu unashindwa kujua kipi kitangulie kipi kifuate,
Kwa sababu ya ubinafsi wako ndio maana ukamkatili huyo mtoto wa Watu Kwa kisingizio cha rafiki yako sijui anamatatizo gani.
Tafsiri yake ni kuwa hata ukioa utatanguliza mambo ya marafiki kuliko Familia yako(Mkeo na watoto),
Hata huyo Mchumba wako ni hamnazo, yaani Bora ungetoa sababu ya mzazi anaumwa lakini kumbe ni matatizo ya rafiki yako.
Mkuu nafikiri bado hujajiandaa kuwa na Familia.
Wazee hutumwa kwa wasichana waliojitunza wenye bikra zaoKawadharau sana wazazi wa binti. Halafu kakosa busara, kawaida jambo kama hilo humwambii binti, unatuma wazee. Mahari huwa haimalizwi. Unatuma wazee hata na elfu hamsini wazee wanajua namna ya kuhandle haya mambo na wangemshauri nn cha kufanya. Bora wasioe tu.
1. Nisubiri nikomae 2. Sijui kipi kitangulie 3. Nina ubinafsi 4. mchumba wangu ni hamnazo 5. sijajiandaa kuwa na familia 6. jambo dogo kama hilo linanishindaKama Jambo Dogo kama hilo linakushinda mpaka uombe ushauri, ni bora usubiri Akili ikomae ndio uingie ndoani, maana Kwa Akili hizi ndoa itakushinda mapema Mno.
Mtu unashindwa kujua kipi kitangulie kipi kifuate,
Kwa sababu ya ubinafsi wako ndio maana ukamkatili huyo mtoto wa Watu Kwa kisingizio cha rafiki yako sijui anamatatizo gani.
Tafsiri yake ni kuwa hata ukioa utatanguliza mambo ya marafiki kuliko Familia yako(Mkeo na watoto),
Hata huyo Mchumba wako ni hamnazo, yaani Bora ungetoa sababu ya mzazi anaumwa lakini kumbe ni matatizo ya rafiki yako.
Mkuu nafikiri bado hujajiandaa kuwa na Familia.
nakazia
Kama ulitoa ahadi lakini ulipobadili mawazo haukutoa taarifa, wanakuona haupo serious. Kama hukutoa taarifa ulikosea.Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.
Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.
Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.
Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Wazee hawatumwi kwa wasichana. Wanatumwa kwa wazazi wa msichana. Hakuna sababu yoyote ya kuwakosea heshima wazazi kwa sababu binti yao hana bikra. Kama unahitaji mwenye bikra tafuta mwenye bikra.Wazee hutumwa kwa wasichana waliojitunza wenye bikra zao
Busara ni kujenga hoja zenye mantiki katika mada iliyowekwa. Kufikiria mambo mengine nje ya mada na kujenga mitazamo hasi ambayo haipo ni kupoteza muda na kujitwika mambo yasiyo na tija. Kama elites, tushauriane kwa staha. Mambo unayoyaona madogo na yasiyohitaji kujadiliwa, kwa wengine ni inshu kubwa. Tuendelee kushauriana!Alafu ATI mpaka ashauriwe akaombe Msamaha ni kwamba hajui kuwa amefanya Makosa, hajali, na bila Shaka hampendi huyo Binti WA Watu.
Ashamtia aibu Binti wa Watu Huko kwao, lakini Hilo kwake halioni Kwa vile hajafanyiwa yeye.
Alafu angefanyiwa yeye angekuja hapa kupiga mayowe Wanawake ni wabaya.
Tabia za ubinafsi, kutojali hisia za wengine ni moja ya tabia Mbaya zinazotesa wengi katika jamii.
Kwa Sisi tusioweza kuvumilia huwaga hatuchelewi kujibu mapigo.
Ndio maana nikiwaambia Wanawake watafute Pesa wajitegemee waachane na kuhudumiwa naonekana mchawi na Mchukia Wanawake wakati tayari nimeshasoma Gap na kujua jamii yetu ni yanamna gani.