Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada

kwa hati fungani ya miaka 20 atapata kila baada ya miezi 6 karibu mil 6, ambayo kwa mwezi ni kama laki 8 na zaidi.
Nimejaribu kufuatilia kumbe kuna kubid..so kumbe unaweza kuwa na hela lakini ukakosa hizo bonds?
 
Achukue milioni 3 tu awekeze kwenye kilimo cha tikiti. Kila baada ya siku 75 anavuna. Net profit sio chini ya milioni 8 akilima eka 3 (za kuhenyeka hasa)

Faida yake ni kubwa sana akijitoa
 
Hamna benk inyoweza kumpa hiyo, hata ile kuu
Bro akili yako ni kubwa
Bora uhamie kule kwenye jukwaa la vipanga
Hiyo hela hawatoi hata ufanyaje sikuzidi maana ni 4mil kwa mwaka
 
Achukue milioni 3 tu awekeze kwenye kilimo cha tikiti. Kila baada ya siku 75 anavuna. Net profit sio chini ya milioni 8 akilima eka 3 (za kuhenyeka hasa)

Faida yake ni kubwa sana akijitoa
Huku kuna vijana wamelima tikiti kwa Mavi ya popo
Tikiti lina ushindani sokoni hatare
 
Awekeze kwenye hati fungani za serikali za miaka 20 au miaka 25 awe anakula interest ya 15% au zaid kwa mwaka.
Yap, kwa mstaafu hii ndio inamfaa. Aachane na benki, wanaweza kumpata good rate sasa, lakini mwaka ukiisha wanashusha rate. Bonds rate zake zipo fixed kwa term yote ya miaka 10/15/20/25
 
Mkuu hebu tuambie hiyo bank gani maana nimeuliza bank nyingi asilimia 6 ndiyo wengi wanayoa kwa hiyo 100 m
 
Mkuu hebu tuambie hiyo bank gani maana nimeuliza bank nyingi asilimia 6 ndiyo wengi wanayoa kwa hiyo 100 mY

Mkuu hebu tuambie hiyo bank gani maana nimeuliza bank nyingi asilimia 6 ndiyo wengi wanayoa kwa hiyo 100 m
Ya posta mkuu,wanatoa 13% kwa mwaka na wanakupa pesa yako ukitaka kwa mwezi,miezi mitatu,sita,tisa au mwaka
 
Haki yake, unaweza kukuta watoto aliwasomesha na wanamaisha yao, sasa unataka awagawie tu?
 
*Anunue nyumba mbili,moja iwe guest house na nyingine aipangishe aidha awe na guest mbili mbona atapata mpaka 3mil.(chakuzingatia ni locations tu) na hapo sishauri labda kwa malipo KIDOGO...

Umemshauri Vizuri Sanaaa....

Huyu mama ahakikishe kabisa hatoki nnje ya fixed assets zinazo ongezeka thamani.

Chonde Chode

ASITOKE NNJE YA MSTARI WA FIXED ASSETS ZINAZO ONGEZEKA THAMANI

1. Anunue hata nyumba aiboreshe afanye lodge / guest house tena asimamie mwenyewe

2. Anunue maeneo makubwa karibu ya mji kama acre au ngap akate kate auze viwanja vidogo vidogo

Hyo namba moja ndio yenyewe

Asifungue biashara sijui za kuuza au kununua, asinunue sijui daladala, lorry, sijui boda boda achane na huo uchafu ACHEZE NA NYUMBA ZA BIASHARA TU. Atanikumbuka.

Hzo hapotei njia mtu akishoboka anamuuzia hela ndefu. Asikubali kuyumbishwa na ndugu, jamaa au marafiki. Simjui Hanijui ushauri wangu wa dhati mbele ya Mungu shahidi afanye navyomuambia kama hawezi aiche hyo hela bank asiitumie.

Hao watoto kakosea sana kuwapa hyo amount. Kama anao wa 4 angewanunulia viwanja vya milion 5 each = 20 M kuliko kuwapa hard cash. Kama ni wengi angewanunulia vipande vya mashamba..asiwape hela. Mtaani nakujua watapoteza kila kitu.
 
Mimi. Ni mstaafu ninajua , simshauri ajenge , kama hakujenga kipind cha ujana akojeo akalale tu,
 
Neelewa kwamba anataka aweke hela bank alafu bank iwe ina mruhusu kutoa laki saba tu kwa mwezi!!

Hakuna bank yenye huduma hiyo!! Ushauri kama anakiwanja cha ziada, bora ajenge apartment za kawaida za laki moja na 20 chumba na sebule ziwe tano atakazo pangisha na kupata laki sita sita kila mwezi iwa wapangaji wake
 
UPO VIZURI SANA WENYE ASSETS NDIO MATAJIRI,AND NOT HARD CASH,
kuwapa watoto hela sometimes its bad,BAADHI watafavya vyema baadhi wataziharibu na kuonja utamu wa fedha,hao waliofanya vibaya na hela wataanza maombi mabaya, (**bora afe, afii tuuu... and so so...).
 
Pamoja na hayo huwezi kuhalalisha kuwa alikosea kukataa kukukopesha. Lile lilikuwa jasho lake. Ulipaswa kwenda benki kama ulitaka mkopo. Alikutunza na kukusomesha ulipokuwa mdogo hivyo sasa hivi unarudisha deni.
 
Ajiandae kupokea maelezo kutoka kwa watu ambao hawajawahi kuuza hata karanga
 
Mkuu naomba unitoe tongotongo. Hivi ukisema ''bond za miaka 20'' maana yake ni kuwa unaingia mkataba wa kuwaachia fedha zako kwa miaka 20 huku ukichukuwa ''faida'' tu?
 
Na kuwa mtaafu kote huko na kupewa mil 100 Bado anakuja kutuomba msaada
 
Mkuu umemalizaa yanii..UZI UFUNGWEEE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…