Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Daah hatari sana kwa kweli matukio mengine mpaka unashangaa kama yametokea Tanzania...ukatili wa kiwango cha juu sana haya matukio tunasikia Mexico,USA na SA..
 
Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

Jeshi letu lapolisi liko vizuri Sana kwenye kufuatilia watuhumiwa.
 
Ili shetani akuangamize lazima akutoe ufahamu kwanza,sasa kwanini hata asingemfungia tu stoo na kuchukua hizo hela badala ya kumuua huyo dada!na kwakuwa kashakamatwa sasa ndio ufahamu umeachiwa,atakuwa anajiuliza maswali yasio na majibu.Salama yetu ngugu zangu ni kuwa karibu na Mungu vinginevyo tutaangamia...
 
Si angechukua tu pesa amwache hata amemfungia mlango kwa nje.

Ila mwezi atakuwa family member
Huyo kijana alijuaje kuna balb mbovu? Atakuwa alikuwa anamazoea, alimuua kuficha kutambulika kirahisi, inawezekama Dada alipewa mchongo akatolea nje akaona amalizane nae
 
Ushawahi kuibiwa wakati hamna mtu ndani ya nyumba? Ukiingia chumbani utakuta nguo zote chini,godoro limefunuliwa hadi foronya,masanduku yote wametoa kila kitu yote hio wanatafuta hela(hawajui umeacha hela ndani au la wanabahatisha).
Hii walifanyaga hostel kwangu 😅😅😅😅 nililiaga sana khaaa

wezi wanarudisha maendeleo nyuma jamani 🥺🥺🥺
 
Mwizi alikuwa na insider information.... inawezekana vipi ajue hiyo nyumba ina hela?
Inawezekana muuaji alishakuwa na mazoea na huyo binti walitongozana na hatimaye kupata siri za nyumbani na hatimaye kupanga shambulio.
 
Ushawahi kuibiwa wakati hamna mtu ndani ya nyumba? Ukiingia chumbani utakuta nguo zote chini,godoro limefunuliwa hadi foronya,masanduku yote wametoa kila kitu yote hio wanatafuta hela(hawajui umeacha hela ndani au la wanabahatisha).
Ni kweli kabisa, lazima wasachi kwanza. Wakikosa pesa ndio huchukua vilivyopo.
 
Asee wadada wa kazi wamekuwa victim sana wa ukatili majumbani. Sema na wao huwa hawana umakini na wakieleweshwa huwa hawasikii. Unamwambia dada ukiwa ndani funga geti na mlango wa kuingilia ndani kwa funguo ila walaaaa hajali Unafika home unapita getini hadi unaingia ndani hadi room kwake wala hana habari anafanya kustuka ....

Au huko mtaani ana kiboda boda chake au mhuni flani ukiwa haupo basi analetwa hadi home mazingira yanasomwa...mwisho wa siku matukio ya wizi au mauaji... Kwa hali hii jamani kweli watakuwa salama..?
Ninapokaa ni nyumba ya 7 kutoka kwetu dada wa kazi alikuwa na mahusiano apo mwili wake ulikutwa uchi mtuhumiwa alisema kuwa walipomlz tendo alimuomb aibe dada akakataa akaamua amue
 
Back
Top Bottom