Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Dr Myles Monroe kwenye moja speach zake about purpose of life alisema usipojua your purpose of living ndio maana kijana Ako tayari kuua ili "anunue Nike shoes"
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamshikilia Selemani Haruna maarufu Kwata (24), Mkazi wa Kimara Temboni mtaa wa Amani, kwa tuhuma za kumuua Editha Charles (22) Mkerewe, Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili huo katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro amesema “Uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa tarehe 06/07/2022 asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi Binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa kuweka Balbu, alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali Binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Tsh 1,800,000 na kutoweka”

“Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

“Aliweza pia kuonesha kiasi cha pesa alizoziiba eneo hilo na pesa nyingine alidai mara baada ya tukio siku iliyofuata alinunua vitu mbalimbali zikiwemo simu mpya, viatu vya mpira pea 2, na begi la mgongoni lenye nguo mbalimbali mpya ambavyo navyo vimepatikana, kitendo alichofanya Mtuhumiwa ni cha ukatili ulipita kiasi, uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na atafikishwa katika mifumo ya kisheria ikiwemo Mahakamani haraka”
inavyoonesha mtu ukishatekeleza tendo la kuua tu, kuna akili Mungu anakuondolea. kweli unaficha mwili Store unafunika funika na vifaa vya store kwa kujua hautoonekana.!
 
Ninapokaa ni nyumba ya 7 kutoka kwetu dada wa kazi alikuwa na mahusiano apo mwili wake ulikutwa uchi mtuhumiwa alisema kuwa walipomlz tendo alimuomb aibe dada akakataa akaamua amue
Uwiiii jamani weeee
Sasa mbona Ana akili ndogo huyo??
 
Umeona eeh
Ukivielekeza tayari midomo itavutwa siku nzima au mwezi ukiisha tu akipata chake utaskia dada me nataka niende nyumbani...
Woiii wakwendree
Uishi kwangu nikuogope hata kukuelekeza kitu?
Una nyodo sana
 
Uwiiii jamani weeee
Sasa mbona Ana akili ndogo huyo??
Nyumba mnakaa wawili tu mama mwenye nyumba anaondok sa 11 anarud sa4usiku nan angetuhumiw kuiba kama sio yeye apo tu hyo mama alijua dada wa kaz katoroka alijua na yeye alipew hela maan tokea hyo tar 6 hyo mtuhumiwa kukamatwa akusema kama ameua maan jirani alimuona kaingia so alipouliza walimuambia walimuona flan kaingia mpaka harufu iposikika ndan jumapili ndo akapigwa kipigo aeleze mkasa mzima.
 
Huyo jamaa afungwe apewe kazi ngumu na kila siku ainamishwe.
Wangese hao wanaharibu image ya nchi.
 
🤣😂😅
Niacheni nicheke mie
Watu humu tunaomboleza kuondokewa kikatili kwa beki tatu wewe unaomba uachwe ucheke.

Haya tumekuwacha, Cheka sasa!

Kaamoonn!

1644838175268.png


wa kupuliza Mr Q
 
Muuaji inaonesha alikuwa anaijua hiyo nyumba vizuri, bahati mbaya madada wa kazi hata uwaelekeze vipi kuhusu wageni wasioelekezwa wasiwape ruksa ndio hawaelewi...
 
Ushawahi kuibiwa wakati hamna mtu ndani ya nyumba? Ukiingia chumbani utakuta nguo zote chini,godoro limefunuliwa hadi foronya,masanduku yote wametoa kila kitu yote hio wanatafuta hela(hawajui umeacha hela ndani au la wanabahatisha).
Mimi watasikitika sana baada ya hiyo kazi... maana sikai kabisa na pesa ndani
 
Nyumba mnakaa wawili tu mama mwenye nyumba anaondok sa 11 anarud sa4usiku nan angetuhumiw kuiba kama sio yeye apo tu hyo mama alijua dada wa kaz katoroka alijua na yeye alipew hela maan tokea hyo tar 6 hyo mtuhumiwa kukamatwa akusema kama ameua maan jirani alimuona kaingia so alipouliza walimuambia walimuona flan kaingia mpaka harufu iposikika ndan jumapili ndo akapigwa kipigo aeleze mkasa mzima.
Duh so wamegundua ameshaozaaa
 
Back
Top Bottom