Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Amuua binti wa kazi kisha kuvunja chumba na kuiba pesa

Hii walifanyaga hostel kwangu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nililiaga sana khaaa

wezi wanarudisha maendeleo nyuma jamani [emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Sasa km n hostel, si room mate hao.
 
Ninapokaa ni nyumba ya 7 kutoka kwetu dada wa kazi alikuwa na mahusiano apo mwili wake ulikutwa uchi mtuhumiwa alisema kuwa walipomlz tendo alimuomb aibe dada akakataa akaamua amue
Sasa angemziba mdomo na nguo, angemfunga kamba miguu na mikono, ili asipige kelele na angemfungia kwa ndani, yeye angeiba hela na kutoka.
 
Umenikumbusha mwaka flan nyuma nilimtembelea Dada yangu na yeye hapo kwake alikuwa anaishi na mfanyakazi tu Mumewe alikuwa kasafiri nje ya nchi, na mimi nilienda kwa kustukiza tu wala sikufanya appointment. Nilicho kikuta Geti kubwa lilikuwa wazi kwa maana lilirudishiwa tu wala halikufungwa na komeo au funguo geti la kuingia ndani lilikuwa wazi na mda huo yalikuwa majira ya saa 6 mchana nilipoingia mpka seblen nikamkuta jamaa kajilaza kwenye makochi yupo tumbo wazi [emoji3][emoji3] sasa ktk kutafakari huyu ni nani nikawa natamfuta yule dada wa kazi kumwita anaitikia akiwa jikoni kusogea mpaka jikoni alipo namkuta anakaanga mayai sasa mwenyewe akaanza kujistukia kwa aibu na hofu mara ashike kikombe aache mara ajiongeleshe vp umegonga sana mlango[emoji1787][emoji1787] narudi tena sebleni yule jamaa sijamkuta alishakimbia. Kumbe yule jamaa alikuwa ni bodaboda na alikuwa mpenzi wake na ilikuwa ni kawaida kwao Sister akiondoka kwenda kazin yule jamaa uingia pale nyumbani kama kwake na ata yale mayai alikuwa anamkaangia jamaa[emoji3][emoji3]. Wafanyakazi wa ndani ni wa kuishi nao kwa makini jamani wengi wao vitendo wanavyofanya majumbani wakiwa peke yao ni vya hatari ambavyo vinaweza kuleta madhara makubwa. Wezi majambazi sometimes upata michoro ya nyumba na kujua kilichomo ndani kupitia wafanyakazi wa ndani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka hadi machozi, sasa jamaa analala kwa kochi km kwake?? Tena tumbo wazi??

Khaaaaah
 
Umeona eeh

Ukivielekeza tayari midomo itavutwa siku nzima au mwezi ukiisha tu akipata chake utaskia dada me nataka niende nyumbani.

Woiii wakwendree

Uishi kwangu nikuogope hata kukuelekeza kitu?
Na mbaya zaidi watu wana mentality kua wadada hua wananyanyaswa ukimkaripia tu anazunguka nyuma anaanza kulia mara asile chakula siku nzima urudi home na mastress tena uanze bembeleza mdada. Mimi nimefika hatua sitaki ujinga nao tena huezi kukaa vyema kwangu niekee nauli yangu mezani amsha kwenu
 
Huyu kijana kuna jirani alimuona alipoingia na muda alokaa,inasemekana kuna kijana walikuwa wanamdhania ndo jirani akawaambia sio huyo ni huyu ila kapigika hapo polisi acha
Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

Jeshi letu lapolisi liko vizuri Sana kwenye kufuatilia watuhumiw
 
Kuna ukazima gani kuua binti ili kuiba, mbona angeweza kumfunga kamba tu na kuiba kisha akasepa
 
Au huko mtaani ana kiboda boda chake au mhuni flani ukiwa haupo basi analetwa hadi home mazingira yanasomwa...mwisho wa siku matukio ya wizi au mauaji... Kwa hali hii jamani kweli watakuwa salama..?
Hili lilishawahi kunitokea. Binti alikuwa anamleta bwana wake dereva wa boda boda ndani kila siku. Ilikuwa anakuja asubuhi anapikiwa chai, mchana anakula lunch na mida ya saa 10 anakuja kuchukuwa container ya supper.

Aliekuja kusanua mchezo wote ni mwanangu mdogo ambae kuna kipindi alikaa kama wiki mbili nyumbani sababu ya kuumwa. Nilipishana na jamaa wa bodaboda njiani nikiwa na dogo, dogo akamchangamkia uncle na kumuuliza kama leo atakuja kunywa chai pia. Jamaa akaanza kupotezea ikabidi kumuhoji mwanangu vizuri ndio nikaambiwa kila kitu.
Kwenda kumuuliza dada kwa ukali ndio akafichua siri yote.

Kwa kifupi hawa madada huwa ni rahisi sana kughilibiwa na vijana wakware na mengi ya matukio hufanywa baada ya kudanganywa na wanaodhani ni wenza wao kumbe vibaka tu.
Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu.
 
Na mbaya zaidi watu wana mentality kua wadada hua wananyanyaswa ukimkaripia tu anazunguka nyuma anaanza kulia mara asile chakula siku nzima urudi home na mastress tena uanze bembeleza mdada. Mimi nimefika hatua sitaki ujinga nao tena huezi kukaa vyema kwangu niekee nauli yangu mezani amsha kwenu
Asee sinaga huo umama wa kubembeza mdada
Yani watu wenyewe wawili halafu tununiane humo ndani itakuwajee
 
Inaitwa Scientific Investigation...ni source kuu ys ushahidi mahakamani
Ana kosa sana unazinije na mtu umuingize kwenye nyumba ya mtu ? Si umesikia huyo mkaka ni kibwana chake
 
Binti wa kaz amepumzishwa uko mloganzila awawez kusafirisha mwili umeharibik vibaya
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamshikilia Selemani Haruna maarufu Kwata (24), Mkazi wa Kimara Temboni mtaa wa Amani, kwa tuhuma za kumuua Editha Charles (22) Mkerewe, Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili huo katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro amesema “Uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa tarehe 06/07/2022 asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi Binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa kuweka Balbu, alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali Binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Tsh 1,800,000 na kutoweka”

“Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

“Aliweza pia kuonesha kiasi cha pesa alizoziiba eneo hilo na pesa nyingine alidai mara baada ya tukio siku iliyofuata alinunua vitu mbalimbali zikiwemo simu mpya, viatu vya mpira pea 2, na begi la mgongoni lenye nguo mbalimbali mpya ambavyo navyo vimepatikana, kitendo alichofanya Mtuhumiwa ni cha ukatili ulipita kiasi, uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na atafikishwa katika mifumo ya kisheria ikiwemo Mahakamani haraka”
...Nawaza huyo atakayepewa Kazi ya kuwapia simu Wazazi wa Marehemu na kuwaamba Mtoto Wenu amefariki! Inasikitisha...
 
Mwizi alikuwa na insider information.... inawezekana vipi ajue hiyo nyumba ina hela?
Ukute ni Mchepuko wa huyo muuali na Nadi alimpa Taarifa kwamba ndani Kuna Hela!
Ila Kuna Watu Wana Roho Ngumu! Umeua Mtu na Siku hiyo hiyo unakwenda kununua simu na Pesa ulizoiba??
 
Umenikumbusha mwaka flan nyuma nilimtembelea Dada yangu na yeye hapo kwake alikuwa anaishi na mfanyakazi tu Mumewe alikuwa kasafiri nje ya nchi, na mimi nilienda kwa kustukiza tu wala sikufanya appointment. Nilicho kikuta Geti kubwa lilikuwa wazi kwa maana lilirudishiwa tu wala halikufungwa na komeo au funguo geti la kuingia ndani lilikuwa wazi na mda huo yalikuwa majira ya saa 6 mchana nilipoingia mpka seblen nikamkuta jamaa kajilaza kwenye makochi yupo tumbo wazi [emoji3][emoji3] sasa ktk kutafakari huyu ni nani nikawa natamfuta yule dada wa kazi kumwita anaitikia akiwa jikoni kusogea mpaka jikoni alipo namkuta anakaanga mayai sasa mwenyewe akaanza kujistukia kwa aibu na hofu mara ashike kikombe aache mara ajiongeleshe vp umegonga sana mlango[emoji1787][emoji1787] narudi tena sebleni yule jamaa sijamkuta alishakimbia. Kumbe yule jamaa alikuwa ni bodaboda na alikuwa mpenzi wake na ilikuwa ni kawaida kwao Sister akiondoka kwenda kazin yule jamaa uingia pale nyumbani kama kwake na ata yale mayai alikuwa anamkaangia jamaa[emoji3][emoji3]. Wafanyakazi wa ndani ni wa kuishi nao kwa makini jamani wengi wao vitendo wanavyofanya majumbani wakiwa peke yao ni vya hatari ambavyo vinaweza kuleta madhara makubwa. Wezi majambazi sometimes upata michoro ya nyumba na kujua kilichomo ndani kupitia wafanyakazi wa ndani.

Ulimuelezea sister yako ikawaje?
Mim ndio maana huwa nafunga hata iweje sikai mlango wazi
 
Kila ukiuliza mbona mayai yanaisha haraka unaambiwa hata sijui kumbe boda nae ana share yake hapo.
Kaaz kweli kweli

Kuna mkaka na mkewe waliweka bulb za taa zenye camera sebulen hawakumuambia mdada wa kzi
Siku moja yupo kazin akaona aangalie kwa simu kinachoendelea home [emoji23][emoji23][emoji23] akaona kijana wa boda kaingia ndani kafika sebulen kavua tisheti kabaki kifua wazi miguu kaweka juu ya meza
Dada wa kazi anaanda supu kamletea jamaa akala halaf akamaliza wakaendelea kupiga stori
Akampigia mkewe wakaenda kufika mwanaume akaruka geti akaingia ndani walishtuka wakampeleka police na dada wakamtimua
Wasichana nao hutamani kuwa na maisha hayo sasa wanaona muda unaenda inabidi wafanye siri hivyo hivyo na wadada wa kzi na boda wanapendana haooo
 
🤣🤣🤣🤣
 
Ninapokaa ni nyumba ya 7 kutoka kwetu dada wa kazi alikuwa na mahusiano apo mwili wake ulikutwa uchi mtuhumiwa alisema kuwa walipomlz tendo alimuomb aibe dada akakataa akaamua amue
Na unaweza kuta pia hawakuwa na mahusiano, Marehemu pengine alibakwa au ilishindikana kubakwa.

Kwa haraka haraka inaelekea kulikuwa na varangati kubwa la kujitetea kabla Marehemu kuuawa
 
Back
Top Bottom