Anafanya majukumu yote ya ndani lakini si pesa ya urembo wangu

Anafanya majukumu yote ya ndani lakini si pesa ya urembo wangu

Najua unamsemea mwanamke mmoja mjinga asiejielewa. Not you
Majukumu yote ya ndani anayafanya hata kunyoa watoto wa kiume nywele J’mosi ni jukumu lake. Ananunua chakula, umeme, ada za shule, nguo za watoto.

Kusuka nywele zangu amesema ni jukumu langu na pia kupendeza. Hataki nimuaibishe tukipata mialiko niwe nadhifu. Haulizi mshahara wangu ni kiasi gani wala haombi pesa yangu.

nimfundishe vipi kutunza mke?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii post imenikasirisha na kuniboa sana! Kila nikitaka ku comment najawa na miasira ngoja niache tuu nipige gambe kidogo [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Siyo mume bali baba yako, ndiyo anaweza kukupa huduma zooote bila hata ya kujiongeza kidogo.
 
Mimi ni mke wa mtu ninahitaji kuhudumiwa
Siku zote kwenye ndoa mwanamke hapewagi hela ya kusuka na shopping, ila ivyo vitu nilivyo vitaja wanawake wengi wanavipata ndani ya hela ya matumiz ya kila siku, mfano mume wako hanakugaiya hela ya matumiz ya mwezi mzima mfano chakula, bill ya umeme maji, nguo za watoto, mkaa, kwaiyo nawewe unatakiwa uingize mambo yako ndani ya bajeti ya mwez mzima, husisubili mume hakupe hela ya kusuka, kunua viatu, lotion, nguo, Ningumu sana mume kukumbuka kila baada ya Siku tatu unatakiwa husuke nywele.

🙏🏾
 
Majukumu yote ya ndani anayafanya hata kunyoa watoto wa kiume nywele J’mosi ni jukumu lake. Ananunua chakula, umeme, ada za shule, nguo za watoto.

Kusuka nywele zangu amesema ni jukumu langu na pia kupendeza. Hataki nimuaibishe tukipata mialiko niwe nadhifu. Haulizi mshahara wangu ni kiasi gani wala haombi pesa yangu.

nimfundishe vipi kutunza mke?

Sasa wee mshahara wako unapeleka wapi... Yaani unashindwa kujiweka sexy for ur husband wakati yeye anatimiza majukumu ha msingi
 
Majukumu yote ya ndani anayafanya hata kunyoa watoto wa kiume nywele J’mosi ni jukumu lake. Ananunua chakula, umeme, ada za shule, nguo za watoto.

Kusuka nywele zangu amesema ni jukumu langu na pia kupendeza. Hataki nimuaibishe tukipata mialiko niwe nadhifu. Haulizi mshahara wangu ni kiasi gani wala haombi pesa yangu.

nimfundishe vipi kutunza mke?
Kwani majukumu yote
huliyo sema anayafanya, je anayafanya kwa mfumo upi? je kwakukupa pesa wewe mkoni au kwa kufanya yeye kama yeye bila kukupa hela ukafanye wewe malipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wakati mwingine mwanaume anatamani kuona mchango wa mkewe kwenye maendeleo ya familia kwa wale wenye kipato

Sent using Jamii Forums mobile app
You have made my day, seriously. Hata kama utachangia 50,000 Tsh. kati ya 1,000,000Tsh. aliyotoa baba, ataithamini sana kwani unamoyo wa kumsaidia mwenzako ila uwezo wako ndo unaishia hapo.

Ukiona mwanaume anajitoa sana kwa mke wake basi ujue huyo mkewe kwa asilimia nyingi sana sio mbinafsi.
 
Mwanamke ni kiumbe cha ajabu
tapatalk_1574542475299.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe mchango wako kwenye familia ni nini?
Maana unatumia muda wa familia kwenda kazini na hautoi mchango wowote kwa muda wa familia unaotumia kukaa kazini.
Nikiwa na mke kama wewe nitakushauri ukae nyumbani ili watoto wetu wapate malezi mazuri maana hatuwezi kusacrifice malezi mazuri kwa watoto wetu kwa wewe kwenda kushinda kazini ukiwaacha watoto na dada wa kazi na familia hainufaiki chochote na kazi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na wakati mwingine mwanamke kama huyu hata kulea watoto hajui.
 
Back
Top Bottom