Anafanya majukumu yote ya ndani lakini si pesa ya urembo wangu

Anafanya majukumu yote ya ndani lakini si pesa ya urembo wangu

Majukumu yote ya ndani anayafanya hata kunyoa watoto wa kiume nywele J’mosi ni jukumu lake. Ananunua chakula, umeme, ada za shule, nguo za watoto.

Kusuka nywele zangu amesema ni jukumu langu na pia kupendeza. Hataki nimuaibishe tukipata mialiko niwe nadhifu. Haulizi mshahara wangu ni kiasi gani wala haombi pesa yangu.


nimfundishe vipi kutunza mke?
Unatakiwa uje kwangu, umcheat jamaa halafu, tufanye aone. Akihisi na kukuuliza mwambie huyo ndiye ananijali. Akigundua kamsahau mkewe mpaka anasaidiwa, ataanza kukukumbuka.
 
Si una mshahara unataka utunzweje tena,wanawake mnakwama wapi?
 
Sio upumbavu ni vile anatamani kuufeel mchango wa mumewe ktk muonekano wake
Ndo upumbavu wenyewe huo! Mzigo wote wa majukumu ameubeba sidhani hata kama amewahi kumwambia pole na asante kwa kututunza zaidi sana anaona hapewi hela ya urembo!? Huu ni upumbavu na ukienda kwa watu wazima wanaweza kukulamba makofi
 
Sasa wewe mchango wako kwenye familia ni nini?
Maana unatumia muda wa familia kwenda kazini na hautoi mchango wowote kwa muda wa familia unaotumia kukaa kazini.
Nikiwa na mke kama wewe nitakushauri ukae nyumbani ili watoto wetu wapate malezi mazuri maana hatuwezi kusacrifice malezi mazuri kwa watoto wetu kwa wewe kwenda kushinda kazini ukiwaacha watoto na dada wa kazi na familia hainufaiki chochote na kazi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana siku hizi vijana hawataki kuoa. Na akioa ndoa haichukui round inavunjika. Bahati mbaya Sana ukikosea ukaoa mwanamke mbinafsi yaani hilo linakuwa zigo maisha yako yote. Na bahati mbaya ikukute Mambo ya kiuchumi yakayumba na mwanamke maisha yenu yote alijikita kwenye urembo wake binafsi......hakujizoeza kutoa japo kidogo kwa familia, hapo lazima akili ikae sawa. Utanyanyasika mpaka ukome.
 
[emoji3][emoji3]ofcourse kuna raha yake kuletewa hizo zawadi,sometimes si mbaya,but isiwe kama jukumu lake asipoleta unanuna na huku bills zote zingine anaclear jamani( meals,school fees nk) na sisi tuwe tunawasuprise akina baba chanja kwa vizawadi pia, wanafurahi haoo Mara leo umeona saa ya laki 3 umemchukulia, Raba kali ya 100,000 hivi, mdada salary inaruhusu(Note:hizo gharama mi siwezi kununua lkn[emoji3][emoji3]).

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo unaandika tu kununua huwezi [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majukumu yote ya ndani anayafanya hata kunyoa watoto wa kiume nywele J’mosi ni jukumu lake. Ananunua chakula, umeme, ada za shule, nguo za watoto.

Kusuka nywele zangu amesema ni jukumu langu na pia kupendeza. Hataki nimuaibishe tukipata mialiko niwe nadhifu. Haulizi mshahara wangu ni kiasi gani wala haombi pesa yangu.


Nimfundishe vipi kutunza mke?
My dear Kwanza nakupa hongera kupata kidume anaejitambua. Maana wanaume Wa siku hizi hawajui majukumu hasa pale inapotokea mkewe nae anafanya Kazi. Swala la kutokukupa HELA Za saloon Sioni kuwa ni issue kama anafanya haya majukumu ya msingi. Ninachoona Mie anakufundisha uwajibikaji kama Mke...maana akikuendekeza kuwa Kila kitu ni yeye siku hayupo.. .utapata shida sana...hivo ni bora akuwajibishe angalau kwa mambo yako binafsi akiamini kabisa Kazi yako inakutosha kujihudumia. Ndio maana hagusi HELA yako. Tena unauhuru Wa kujipara utakacho bila kusimangwaaa..maana wengine hupewa HELA kwa maelekezo ya nini cha kusuka.utasikia elf 15 inakutosha kusuka yeboyebo!
 
Hii coment imenifanye nisiendelee kusoma huu uzi tena
Ona!!! Wanawake jamani ni shida!!

MWANAUME ANAHITAJI:

1. Kupikiwa
2. Unyumba
3. Kupumzika

MWANAMKE ANAHITAJI MWANAUME WAKE UWE:-

1. Mpenzi
2. Rafiki
3. Mshikaji
4. Kaka
5. Baba
6. Mwalimu
7. Bosi
8. Mpiganaji
9. Askari
10. Mlinzi
11. Mpishi
12. Fundi umeme
13. Fundi bomba
14. Mchungaji
15. Mzee wa kanisa
16. Shehe
17. Daktari
18. Mpambaji
19. Mwana mitindo
20. Modo
21. Mnyanyua vyuma
22. Fundi magari
23. Mwanasheria
24. Mhasibu
25. Fundi seremala
26. Mcheshi
27. Mwanamuziki
28. Muigizaji
29. Shamba boi
30. Fundi ujenzi
31. Msafi
32. Unajali
33. Mzazi
34. Mlezi
35. Mvumilivu
36. Mjanja
37. Mpole
38. Mkarimu
39. Msikivu
40. Mtunza siri
41. Mkweli
42. Kiongozi
43. Tajiri
44. Mpangaji
45. Mwana Michezo
46. Mtundu
47. Tegemeo
48. Jasiri
49. Mthubutu
50. Shupavu
51. Mwerevu
52. Muungwana

HAPO HAPO UNATAKIWA:-

53. Uwe Fundi kitandani.
54. Uwe unamtoa outing.
55. Uwe unampa pesa za kutosha.
56. Usimsumbue sumbue.
57. Usiangalie wanawake wengine.

HALAFU KUNA:-

58. Kumnunulia vizawadi zawadi hapa na pale.
59. Kumsifia alivyoumbika.
60. Kumsifia alivyopendeza.
61. Kumfungulia mlango, kumshikia pochi.

PIA USISAHAU:-

62. Siku yake ya kuzaliwa.
63. Kumbukumbu ya ndoa.
64. Siku ya valentine.

MUHIMU SANA, KUWA MAKINI:-

65. Jifunze kutoulizia chenji ukimpa pesa ya shopping.
66. Usipende kubishana nae kila kitu.

(Hayo ni baadhi tu mazee, nitaongeza mengine baadae).

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha kazi uone kama hajakuhudumia hakuweki kwenye bajet coz wwe unaweza kujihudumia ila inapopatikana hela ya reserve akikuta ki2 njian atakunulia
 
Back
Top Bottom