Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Huyu bint inawezekana kabisa nikaachana naye so soon kama hatokuja na majibu sahihi.

Tume date muda kiasi na nlimwambia misimamo yangu toka mwanzo. Anafanya kazi nami nafanya kazi. Hakuna issue ya kupeana pesa. We share. Mimi sihongi hata siku moja. Tunapendana basi tunakubaliana kupeana mapenzi. Siuzi , Sinunui.

Sasa kwenye mahari ndo ananiambia baba yake alimuoza dada yake kwa tsh Mil 4.5 yeye alisema bila mil 6 hamwachii. Nikamwambia itakuwa baba yake alikuwa anatania mzazi mwenye akili timamu hawezi hata waza hilo neno. Akakasirika kuwa namwambia baba yake hana akili timamu.

Ilileta shida. Mimi nlisisitiza kuwa baba yake hawezi dai mahari hiyo sababu nahisi atakuwa mzee mwenye akili. Wapumbavu ndo huwa wana hizo tabia. Akakomaa sana kuwa huo ndo ukweli na baba yake ana akili sana tu.

Muda ukaenda imefika seriously kwenda jitambulisha. Now in a serious tone anasema niandae kama Mil 6.hivi ili hata akishusha basi iwe 5.4

Nlimuuliza hiyo Mil 5 nalipia nini kwake? Je nimemkuta bikra? Akainamisha kichwa chini. Je mashine yake ina regulate joto au ni adjustable? Yaani ana nini ambacho ni special kwangu. Akaanza ugomvi nimemdharau sababu nimeshakaa naye sana kuna ambao wanamwona dhahabu.

Basi nikamwambia its ok akaolewe na hao wanaomwona dhahabu. Akanichunia siku 3. nikapanga nguo zake akija azichukue aondoke. Siku hiyo kaja amefura sana. Nikajua kaja kubeba mizigo yake. Wala. Anataka tuzungumze nilimwambia mimi kiukweli siendi kutoa mahari kwao. Sioni sababu. Kama yupo tayari kuwa nami nitaenda jitambulisha na zawadi nitabeba ila mahari siendi toa. Kama hakubaliani na hilo abebe mizigo yake tu aende.

SITOI mahari hilo nimekataa. Mtu nimemkuta amesha chakatwa sana tu. Namtolea mahari iweje? Halafu acha hilo jambo yaani why nikalipe pesa kwao wanawake ambao wapo tayari niwalete home tuishi wengi tu? Yeye ana nini maalum? Nampenda ni kweli ila siendi mimi mlipia pesa ili kuendelea kulana naye.

Nitatoa zawadi kwa wazazi na ndugu zake. Zawadi si lazima na haina kiwango. But mahari No. Si yeye yu hata mwingine akija. Akitaka tukubaliane kuishi hataki akatafute mwingine.



Wewe ni mwanaume dhaifu
 
Ungetafuta watu ukaenda kwao,huko ndio ungejua ukweli,sasa unaanza kugombana na binti,ambae hata mahali hapangi
Hayo anayoyaongea ndiyo ambayo kaambiwa na baba yake. Huwezi enda kwa binti kwao bila kupata dodoso. Maana huwa siyo siri kwao. Wanaongea wanamwambi.... Wewe mwanetu bila kiasi hiki hakuoi mtu.
 
Ungejua nafasi yako kama mwanaume unayetegemea kuanzisha familia itakayokutegema kama mkuu wa kaya kuna vitu ungevitazama kwa jicho la tofauti sana.

Yaani umemchambua binti watu kiasi hicho!? Hapo kisa sio mahari tuu! Hayo maneno yameonyesha ulivyo na roho chungu na mbinafsi.

Kama hakufai si umwache? Au ukiambiwa umwoe bila mahari ndio unamwona mwanamke bora??

Tafuta wakubwa wakueleze maana ya mahari watakuambia Mahari ni kipimo cha kujua kama mwanaume yuko tayari kubeba jukumu la ndoa na familia.

Halafu ukiwa mwanaume ukapangiwa mahari kitendo cha kuikubali tuu ni alama tosha kwamba wewe ni mwanaume mwenye kujielewa, mpambanaji na mpiganaji. Mahari unaweza kulipa yote mahari unaweza lipa kwa awamu.

Halafu, Kama mahari imekushinda utaweza kulea mke na watoto?
Kaka yangu Kiranga naomba usome hapa. The real meaning of mahari na sio kukaa mnawaharibu vijana eti wakimbie mahari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani tokea waarabu wawekeze Tz, Basi kila mtanzania ni mfanya biashara.

huyo binti na baba yake ni wafanya biashara. 😀😀😀😀😀😀
 
Nenda kwao kwanza wazazi wakuone halafu mpige mimba watashusha bei. Ila mkakati wako wa ndoa ni wa kibabe sijui vijana wa siku hizi hamfundishwi maana ya kuwa mwanaume
Mwanaume ni kuwa na msimamo. Ndo maana siku hizi mnavuliwa ubingwa sababu mnakosa msimamo.
 
Isitoshe kuna room ya kuomba punguzo la mahari. Wengi tumeoa na mahari tumelipa kwa instalment. Huyo ni mzinzi tu kama alivyo huyo mchumba wake. Binti makini asingekubali kumegwa na mhuni huyo tena nje ya ndoa.
Nitafutie Binti Bikra humu nakupa Milion 6.
 
Aliekwambia wa kishua wanalipiwa mahali kubwa nani?? Dogo mbona huna akili aisee.

Mahali wanapanga wazazi/mtoto waala sio kulingana na kipato chao bali kila mahali kulingana na mila zake. Ndio maana nikakwambia inabidi ujue maana ya mahali kwanza sio kupayuka tu.
Mahari
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Wewe si unataka kujimilikisha
Si lazima. Miaka yote tunatiana akiamuana analala akiamua anaenda kwake. Na ilikuwa vizuri tu. Mi sikuwa nataka hata azoee kwangu. Basi tu akaanza na mwishowe akaweka kambi. Tunapendana na kama tunapendana basi awe tayari kuoana nami siyo kununuliwa nami. Sioni cha kulipia kwake.
 
Huyu atakuwa mtani wangu mpare huyu. Bro mahari haiishagi lakin pia jitahd wakati mwingine umsikilize mkeo mkuu. Neno msaidizi ni zaid ya tunavyolichukulia. Kuwa karibu na mkeo na jitahd usikilize umbea wake wote ili uwe mtu wake wa kwanza na uuteke moyo wake. Lakin mahari ni lazima ni mila sio fadhila japo ckubaliani na wazee wanaotaja zaid ya ml 1. Usisahau kakusomeshea mkeo bro
Hajanisomeshea. Kamsomesha kwa manufaa yake. Elimu ni ya mwanae. Hainihusu. Nami nimesoma pia. Na kumsomesha ni wajibu wake. Sikusema amsomeshe nije nimuoe.
 
Ndio maana sisi sio wazungu
Na ndio maana wazungu wanaotuoa wanaulizia taratibu na wanalipa mahari
Hukunielewa kwa vile sikujieleza sana. Hao ni ghali kuliko mahari tunayotoza hapa kwetu. Ila kusema za ukweli kutoza mahari kubwa si halali. Kwani mahari inamaliza umaskini wa familia.

Nazungumza hili kwa vile bado nina mabinti na nishaozesha. Kwangu mahari ni chini ya TSh. 10,000 tu ambazo na mimi ndizo nilizotozwa wakati nikioa mama yao. Kwani unauza mtoto? Je, kijana naye hakuzaliwa kama huyo binti yako?

Ila huo ni msimamo wangu si lazima kila mzazi afanye hivyo
 
Hajamtukana baba mkwe,
sijaona sehemu amemtukana baba mkwe.

Ameongea ukweli..Wewe unafikiri kudai M6 kama mahari ili kumuoza binti ni wazo linaloweza kutoka kwenye kichwa cha mzazi mwenye akili timamu???

Mtoa mada yupo sahihi tu sijaona kosa lake hapo.
Kabisa. Mimi sijamtukana mkwe popote pale. Nimesema tu mzazi mwenye akili timamu hawezi fikiria hilo. So siamini baba yake anaamini kuwa anatakiwa alipwe tsh mil 6.
 
Mahari kubwa ni swala la kwanza Ila maneno yako yanareflect perception yako kwa mwanamke ni swala la pili ambalo ni hatari zaidi huyo mwanamke atakaekubaliana na wewe tuanze kumuombea mapema.
Perception yao ndo mbaya. Ya kutaka kuuza watoto wa kike. Yangu ni kuwa tunazungumzia usawa na haki sawa. Ndo usawa wenyewe huu.
 
Back
Top Bottom