Sisi ni waafrika sio wazungu. Kuna kitu kinaitwa tamaduni, ndani yake kuna mila na desturi. Mahari sio kitendo cha kupuuzwa kinabeba ujumbe mzito sana wa kuunganisha familia mbili, kutoa mahari ni tukio la heshima na adabu kwa ukoo wa mwanaume waliokulelea binti yao hadi kawa mkeo leo.
Mahari ingekuwa ni malipo ya kumnunua binti the bei ingekuwa ni juu sana zaidi ya hata bilioni maana utalipia kila dakika iliyotumika na mzazi katika kumlea na kumkuza binti yake.
Anyways, tujifunze maudhui na maana nyuma ya matendo yetu ya kijamii ili tuweze kulinda, kutunza na kuboresha mila na desturi zetu za kiafrika.
Wazungu ni watu tofauti sana na sisi, kuna mambo tunaingiliana ila si yote tena tunatofauti kubwa sana. Kuacha mila na desturi zetu kwa kisingizio cha kistaarabika ni dalili ya udhaifu na ulegelege wa kusimamia jamii yetu. Wanaume tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda mila na desturi no matter how hard jamii za magharibi itakinzana na kutuingilia.
Sisi ni waafrika na tunaijenga Africa kwa namna yetu. Dont be laid back brother.