Anataka kuacha ajira ya kudumu ajikite kwenye kilimo

Aisee na mimi nimefikiria kama wewe na ninachofikiria huenda ni hadithi ya kufikirika. Hilo suala lilikua sio la kufikiria mara mbili bali au kuja kuuliza uliza hapa bali ni kuchukua maamuzi tuu kama msomi
 
Mkuu naomba nkuchek Pm
 
Nina haya ya kumshauri;

1. Aachane kabisa na mahesabu ya akina Inspirational speakers. Kwamba nilianza na punje moja ya mchele, sasa ninamiliki magunia laki mbili ya mchele. Hawapo realistic sana. Hawazungumziagi changamoto za shughuri husika.

2. Kama mwaka jana amelima na akapata kiasi alichopa, NA AMEFANYA HAYO AKIWA MFANYAKAZI, kwanini asiendelee na kazi huku akifanya kilimo? Akishazowea au akishajua faida na hasara za kilimo huku akiwa ameshapata uzoefu mkubwa ndo aache kazi na kujikita mazima kwenye kilimo.

3. Kwa sasa anasema eneo analolima halina shida ya mvua, ameshajiandaa na cha kufanya endapo mvua itasuasua..?
 
Aendelee na kazi mpaka atpostaafu, maana ndio ilionfikisha alipo,asubiri tuu kustaafu kwa raha
 
Kama mm ningekua yeye kwanza hiyo mil 180 ningeitupia Utt mfuko wa liquid then nikaenda bank nikachukua mkopo wa hiyo hela ambapo wangenipa 80% ya mil 180 ambayo ni kama mil 140 nikaacha utt na bank walipane marejesho huku nikijua wakimaliza pesa yangu mil 180 ipo palepale.sasa basi huo mkopo wa mil 140 ningehakikisha nahakikisha nawekeza ktk maji kupatikana shamban sabab nikiwa na trekta + maji nakua sina hofu tena so kama kisima ningechimba au kuvuna maji ningevuna.then nikalima ekari 100 na ekar 100 zingine ningekodisha pesa ya kukodisha ndo ingesaidia kuhudumia shamba ninalolima
So sabab nina maji ningekua nalima mara2 kwa mwaka mazao tofauti tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapa ndipo wahindi wanapotuzidi! Hata angeuza akapata 100m ingetosha kuacha ualimu
 
Asiache kazi kwanza.
Kilimo hakitabiriki.
Unajua Milioni 180 Kuna laki 6 ngapi? Kuna laki 6 mara 300! Yaani hiyo pesa +assets hata msimu uwe mbaya akivuna akauza akapata 40m ukitoa gharama faida ikabaki 20m ni nyingi kwa mwaka ambapo kwenye ualimu kwa mwaka anapata 6m
 
Kimsingi huyu jamaa ni tajiri, I wish ningekuwa yeye Wala nisingeomba ushauri kwa yeyote! Kesho ningewasilisha barua ya kuacha kazi 24hrs
 
Aache ualimu. Hio ni pesa nyingi sana, akiwekeza anafika mbali sana.
Afanye ualimu kama hauathiri shughuri zake binafsi.
 
Acha uongo wako hivi unafikiri kulima ekari 200 ni mchezo?
 
Ujue kilim0 kina msimu kuna wakati kinakukubali kuna wakati kinakukataaa....Mimi nimelima sana ila kwasasa kimenikataa napanda vizuri natumia garama kubwa ila kimenikataa kabisaa...nimekaa na wakulima wengi wameniambia pia wa0 walikuwa wakulima wakubwa ila kwasasa hata wapande nini hawapati waliv0tarajia...Mwambie asiache ualimu ajigawe huku na huku...kilim0 si0 chakujivunia...
 
Jf mambo mengi sana,yaan mtu anapata mill 180 ambayo ukigawa kwa take-home ya 640k unapata miaka 23+ plus ya kufundisha....afu huyo huyo mtu anaomba ushauri kama aache kazi au aendelee....kama unashindwa kufanya maamuzi ya 640k je hiyo 180mill amewezaje kuipata,
Sina ushauri ila mjitahidi kuleta story zenye uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…