Anayefahamu kijijini wanakouzwa mashamba Kati ya laki 2 Hadi 5 anijuze popote Tanzania

Wilaya zote ni karibu vijiji vyote,isipokuwa kuna Kijiji Kimoja kinaiwa wotta_Mpwapwa wagumu kuuza.Bei ni kuanzia laki na nusu inategemea na muuzaji.Huko wotta ni watu waliohamia Toka Iringa kutokana na vita vya wajerumani na Wanyalukolo!
Nashukuru sana wadau Kwa kufunguka basi KAZI imebaki kwangu kuamua pa kuelekea nishapata mwanga. This is the reason I like JF
 
Ni mengi mno.

Kuanzia, Sumbawanga, Namanyere hadi Mpanda vijiji vya Senta Maria, Kasekese, Kagunga hadi Katuma.

Kama unataka kanda ya Shinyanga, Maeneo ya Kahama vijiji vya Senta Chale, Segese, Lugunga hadi Kalumwa.

Tanzania bado ina maeneo mengi sana mazuri tu bei ya chini, ni wewe kuchagua tu.
 
senta maria na kasekese mkuu kupata kwa bei iyo ngumu maana pale ni mbuga sana, labda maeneo ya nyagantambo, mwali, katondo,bugwe, uzuri wa maeneo hayo ardhi bado nzuri mnooo na ni jirani na makao makuu ya wilaya Tanganyika
 
senta maria na kasekese mkuu kupata kwa bei iyo ngumu maana pale ni mbuga sana, labda maeneo ya nyagantambo, mwali, katondo,bugwe, uzuri wa maeneo hayo ardhi bado nzuri mnooo na ni jirani na makao makuu ya wilaya Tanganyika
Nilikuwepo huko mwaka 2020, bei ilikuwa chini, sijui sasa hivi labda.

Hiyo barabara ya Mwese kupita Kapanga, maeneo yalikuwa bei sawa na bure.
 
Siyo mbaya atapata namna bora ya kuingia shambani huko mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…