Anayejua kuhusu huyu Roboti wa Tanzania anisimulie vizuri. Naona mitandaoni amekua gumzo

Anayejua kuhusu huyu Roboti wa Tanzania anisimulie vizuri. Naona mitandaoni amekua gumzo

Mimi leo nimeshacheka hadi basi, bora angekuwa robot wa mtaani ila sio wa kwenda kupelekwa hadi bungeni.
Hii nchi sijui tunaweza kufanya nini kwa usahihi, sanamu ya Nyerere tu ilitushinda!
Tunaweza kupitisha wabunge bila kupigwa mkuu.
 
😂😂

Jana condester bungeni alikuwa anampiga SPANA nape kuhusu roboti “Eunice”

Nasikia tenda wamepewa vijana kutoka South Africa kutengeneza hicho kitu, na wanasema kuna operator ambaye anafanya kazi ya kujibu kwa remote maalumu. Kwa maana kwamba kazi iliyofanyika bado haina ufanisi.

Na wameishia kumuita mdoli wa Nape.

Mimi nipo hapa kuuliza kwa ndugu zangu Watanzania.

Huyu roboti anamsaidia vipi raia ambaye huduma za kijamii kama zahanati vijijini, barabara mbovu, maji na mengineyo kuyatatua?

Jamani Kaka yangu Pascal Mayalla naomba unisaidie nijifunze kitu.najua unashinda sana bungeni.

Nisaidie faida za huyu roboti katika maendeleo ya taifa.
Mada yako ingekuwa na facts if ungeacha neno “nasikia” hivi “nasikia” vile. Means hata wewe huna correct informations
 
Mada yako ingekuwa na facts if ungeacha neno “nasikia” hivi “nasikia” vile. Means hata wewe huna correct informations
Mkuu wangu.

Kamsikilize mbunge condester hiyo nikutokana na maneno yake.

Hivyo mimi ninahisi tu kama ni ya kweli au laah ndio maana nikasema nasikia.

Ahsante pia kwa ushauri.
 
Miaka kumi iliyopita kuna jamaa mnazi mmoja alikuwa anachezesha mdoli maarufu kama joyce wowowo, kuna mzungu aliununua na kuondoka nao, miaka kumi baadae tunaletewa bungeni humanoid,
 
Hadi mbunge mwenzake jana alimwambia wazi kwamba katupiga changa la macho ,kuna mtu alikuwa pembeni pale anafeed swali then anatoa jibu then Robot "YUNISI" anajibu ,yaani AI ya nape ni Zero kabisa , robot anaongelea tumboni hahaaaa ,robot mdomo hauchezi kabisa ,wajifunze kwa walioweza ,inatakiwa kusiwe na humani interaction ,robot ukiliuliza inatakiwa likujibu lenyewe ,kama BOT linavyojibu ukiliuliza.
 
Miaka kumi iliyopita kuna jamaa mnazi mmoja alikuwa anachezesha mdoli maarufu kama joyce wowowo, kuna mzungu aliununua na kuondoka nao, miaka kumi baadae tunaletewa bungeni humanoid,
Joyce wowowo ana zaidi ya miaka 30 mkuu ,ameanzia 90s.
 
Hadi mbunge mwenzake jana alimwambia wazi kwamba katupiga changa la macho ,kuna mtu alikuwa pembeni pale anafeed swali then anatoa jibu then Robot "YUNISI" anajibu ,yaani AI ya nape ni Zero kabisa , robot anaongelea tumboni hahaaaa ,robot mdomo hauchezi kabisa ,wajifunze kwa walioweza ,inatakiwa kusiwe na humani interaction ,robot ukiliuliza inatakiwa likujibu lenyewe ,kama BOT linavyojibu ukiliuliza.
Huyu ni joyce wowowo tu
 
Back
Top Bottom