Anayejua Rais Samia anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Nimeuliza tu jaman msinishambulie sana, maana mimi nimeona kuna ubinafsi mkubwa sana kwenye hii tabia , lakini nimebaini kiongozi huyo hana uchungu wala upendo wa dhati kabisa na watu wake anao waongoza na mengine yafananayo.
Sasa najiuliza huyu kiongozi yupo hapo kwa ajili yanani?
Kama uliisikia hotuba yake ya juzi ,huna haja ya kuuliza hayo maswali
 
Ukiona Hivyo ujue hatuna kiongozi Bali tunakivuli tu Cha kiongozi
 
Duniani kote ufisadi ni adui wa maendeleo, nyinyi mna Raisi anayewaambia viongozi kuleni urefu wa kamba zenu.
CAG anatoa ripoti ya ubadhirifu wa pesa nyingi Serikalini, Raisi anaishia kusema shenzi.

Bado kuna wajinga wanaona wana kiongozi ambaye ataifikisha Tz sehemu? Hizo nguvu, vijembe zingeelekezwa kwenye maendeleo hakuna mtu angefungua mdomo wake, maana karibu vya kupiga kelele vingekuwa vimefanywa na Serikali.

Siku ya Watanzania kuamka, watalia kilio cha kusaga meno, itafika hiyo siku nasema. Unataka kwenda mbugani unaambiwa kumeuzwa ni mali ya watu, misitu ya watu itakuwa too late. Acha watu wajichotee mabilioni, ndiyo maana nguvu kubwa inatumika. Usimuamshe aliyelala, utalala wewe.
 
Nimeuliza tu jaman msinishambulie sana, maana mimi nimeona kuna ubinafsi mkubwa sana kwenye hii tabia , lakini nimebaini kiongozi huyo hana uchungu wala upendo wa dhati kabisa na watu wake anao waongoza na mengine yafananayo.
Sasa najiuliza huyu kiongozi yupo hapo kwa ajili yanani?
Kwa ajili yake, familia yake na kunguni wake.. Nyie kwakwe ni vinyamkera tuuu
 
Ukitaka kuskia akiongelea Rushwa nenda youtube ukasikilize mada za rushwa kila mkutano na mada zake
 
Nimeuliza tu jaman msinishambulie sana, maana mimi nimeona kuna ubinafsi mkubwa sana kwenye hii tabia , lakini nimebaini kiongozi huyo hana uchungu wala upendo wa dhati kabisa na watu wake anao waongoza na mengine yafananayo.
Sasa najiuliza huyu kiongozi yupo hapo kwa ajili yanani?
Hapa huwezi kuona Mwashambwa, chiembe, tlaatlaah wakiongea chochote cha maana
 
Nimeuliza tu jaman msinishambulie sana, maana mimi nimeona kuna ubinafsi mkubwa sana kwenye hii tabia , lakini nimebaini kiongozi huyo hana uchungu wala upendo wa dhati kabisa na watu wake anao waongoza na mengine yafananayo.
Sasa najiuliza huyu kiongozi yupo hapo kwa ajili yanani?
Tume za kuchunguza ufisadi zitaundwa nyuma ya mikamera majibu ya hizo tume nyuma ya pazia
 
hakuna mbwa atakemea ukimtupia nyama ila ukishampa jaribu kumsogelea uone.
 
Ukitaka kuskia akiongelea Rushwa nenda youtube ukasikilize mada za rushwa kila mkutano na mada zake
Mbona wote tunamsikiliza huongea kwa ukali kama alivyo kemea wanaharakati? Au kwa vile unahofu wanaharakati wanahatarisha ugali wake ndio maana anakuwa makali kuliko kukemea ufisadi. Huoni huu ni ubinafsi?
 
Kwahiyo unataka asiongee kwa ukali akubembeleze
 
Tukajifanya tunaoujasiri wakuonja sumu , dadadeek Kizimkadzi anatunyorosha kinyambisi , na sijui tutamchomoaje.

Paka kashaonja panya mwenye chumvi ...tuliombee tu Taifa
 
Paka kashaonja panya mwenye chumvi ...tuliombee tu Taifa
FB_IMG_1748143380375.jpg
 
Tukajifanya tunaoujasiri wakuonja sumu , dadadeek Kizimkadzi anatunyorosha kinyambisi , na sijui tutamchomoaje dadaddeeeki.

Paka kashaonja panya mwenye chumvi ...tuliombee tu Taifa
Chumvi umemwekea ndugu?
 
Jambo moja ambalo nimeliona kuwa dhahiri ni kwamba raisi wetu hapendi kukosolewa, na hata zaidi anakuwa na hasira sana pale anapoona kama watu wanamkashifu au kile kinachoonwa kumtukana. Watu wamepigwa sana, wametekwa na hata kuuwawa, na hadi sasa wengine hawajulikani walipo kwa kile kilichoonekana kuwa kwenda dhidi ya raisi au serikali, au tu kujionyesha yeye ni nani na hachezewi.

Uongozi wa Raisi umekuwa kwa kiasi kikubwa wa visasi na hasira zinazodhidi na kupita kiasi juu ya mambo madogo madogo sana. Mara nyingi raisi ameamua kuua mbu kwa kutumia rungu kwa vitu ambavyo alipaswa tu kuviacha vipite na upepo.

Sasa najiuliza, iwapo raisi anafanya hivi katika awamu yake hii ya kwanza, akichaguliwa awamu ya pili itakuwaje? Nachelea kutakuwa na kampeni kubwa kutafuta wale wote walioonekana kuwa dhidi yake na wataumizwa sana. Kuna watu wengi wanaweza kuja kuumizwa sana, na si wao tu, bali kama awamu hii tumeona ukali na hasira ya kupita kiasi ya raisi, basi tufunge mikanda maana akipita tutanyooshwa kwelikweli. Kuna kila dalili kwamba katika awamu ya mwisho, ukikohoa tu utatekwa, utapigwa, utafungwa jela na hata utauwawa.
 
Hebu fikiria. Wakenya wamekuja nchini kwa ajili tu ya kumuunga mkono Lissu, kuhudhuria tu mahakamani. Hawajatamka neno lolote wala kufanya jambo lolote dhidi ya serikali, na wala haikutarajiwa wangesema lolote. Kesi ingeahirishwa warudi kwao. Lakini bado raisi amewashughulikia utafikiri walikuja wakakutwa na silaha za kuipindua serikali, na hotuba za hasira kutolewa.

Mtu kachoma picha, akahukumiwa faini tu kuonyesha ni jambo dogo, lakini leo haijulikani yuko wapi. Ndani ya miaka minne mara mbili tuna kesi za uhaini kwa tafsiri tu ya sentesi iliyotolewa kisiasa.

Ni kiongozi wa namna gani huyu? Atakuwaje akipewa madaraka awamu ya mwisho?
 
Kitakacho kuwa wacha kiwe. Tumechoka sasa basi. Hatuogopi kuuwawa. Kifo ni kifo tu kama alivyosema. Kwani yeye/wao wataishi milele ? Tanzania inakwenda kwenye point of no return. CCM wanajua muziki 2025 sio wa kitoto.
 
Back
Top Bottom