Tukila ugali tushibe vizuri alafu simu iwe na bundle la kutosha, hatudaiwi kodi nje tunayo Vitz tumepaki. Tunalipwa na serikali. Hela ya bia haipigi chenga alafu tunalo limchepuko la maana hapo limetuli. Kiujumla we have No stressπππ
Kazi kubwa ambayo hua imebaki hapo ni kuilaumu serikali tuu.ππππ
Serikali ya Magufuli na Samia ilichukua tozo kwa walio jilimbikizia fedha za wananchi kiholela kwa sababu mbalimbali. Moja wapo ikiwa ni uzembe wa taasisi ya Urais. Kwa katiba ya nchi ilivyo, RAIS ni MTAWALA. Magufuli alipokaa kwenye hiyo nafasi, ikulu ikaonekana kwa watu wa kawaida. Maendeleo ya huduma na vitu tukaviona.
Serikali ya Samia na Nchemba (Magu alimtema), wao; wale Masharobaro wapigaji wakuu wa fedha za umma na wakwepaji wa kodi, wanakodishiwa ndege kwenda ng'ambo utalii wa biashara hewa. Magufuli alichosema biashara ya mahindi kwenda Kenya hapana. Bali tuwapelekee UNGA. Ni aibu tunawapelekea mahindi, wao wanayakoboa na pumba na viini wanatengeza chakula cha mifugo na kutuuzia kwa bei ya juu Mara tatu ya bei tuliyo wauzia mahindi. Hata Raisat SAMIA kwenye hotuba yake bungeni Nairobi, wabunge wakichekelea kuwa yeye SAMIA ni SULUHU (bure) na KENYATA ni UHURU (afanye atakavyo).
TUSIILAUMU SERIKALI BALI TUJIANGALIE UPYA KWA KUJIPANGA.
1) Tunahitaji KATIBA. Katiba IPO. Ni ya kale, sio mpya. Ina vitabu viwili.
a- KATIBA MAMA -Alipewa nabii Isa / Yesu ina Ibara 7 ufu 5:1, 6, 12. Ibara hizi saba zimefichwa kwenye kitabu cha mwanafunzi wa Madrasa Q1:1-7, kiitwacho Kanuni na Juz'u Amma. Hapo mwanzo kilikuwa kinaitwa KANUNI YA IHSANI (yaani kanuni ya kupiga kura ya ndio). Ndani yake kuna sehemu tatu-
i) kanuni ya MAISHA ya miji,
ii) katiba mama na
iii) elimu ya Uraia (juz'u tatu za sehemu ya kumi ya mwisho ya Msahafu uliotwaharika [maarufu siku hizi kwa jina la Qur'ani Tukufu]).
b) KATIBA MWENZA -Alipewa Muhammad. Ni elimu ya uraia (civics). Juz'u ya 30 (mambo yaweje), juz'u 29 (tubarikiwe) na juz' u ya 28 (watu tuwe wasikivu). Ina Ibara 1132
HII KATIBA INA SURA 58.
Ni kweli KATIBA ya nchi yetu haikidhi mahitaji; hasa ikiwa Rais atakuwa Mwana siasa. Ndio maana ulaya yote nchi nyingi zina wafalme. Na nchi zenye Rais, waziri mkuu ndiye mtawala. Japan kuna mfalme. Uchina rais ni wa kudumu. India wazir mkuu ni mtawala n.k.
Tumzingire Raisat Samia na tumuombe Mbowe na Chadema waone mbali na sio nyayoni mwao.
Wazungu wametukamia. Miaka 400 iliyopita walishajipanga. Download Lord Macauley, ripoti yake bungeni uingereza ya mwaka 1835, utachoka.
Mwaka 1884-5 mkutano wa Berlin wakajikatia maeneo barani mwetu bila kutushirikisha. Mwaka 1917, makampuni makubwa wakajikita kwenye mikataba baina yao jinsi ya kula keki (utajiri na Mali barani mwetu) bila kuzozana.
Mwaka 1949 wakahamisha miji mikuu ya dunia, badala ya kuwa Makka na Jerusalem, wakazua New york na Brussels.
Mwaka 2019 covid, walilenga itumalize watu weusi Afrika. Mbowe, Tundu, na MIMI; Tuwe macho. Siasa ni uongo.
Tutumie AKILI. Ndio maana wamefanikiwa kutupa uhuru wa Bendera kwa akili yao. Mpaka Leo tunalumbana kwa tamaa ya madaraka. Uh!
Lini tujenge nchi?
AKILI YAO:
Tumerithi mfumo wao wa utawala, wizara 23 Mji mkuu. Ndugu Ndungai anaomba apewe mpango mbadala wa tozo wabunge waliyoipitisha. Kwa fikra hiyo nampa dole. Hilo tutalifanya Mungu atujalie uhai.
Malezi, Mafunzo, Ulinzi, Biashara, Elimu, Kilimo, Michezo n.k, vyote ni replika. Tumewaiga. Kwa kuwaiga, Mungu wetu watu weusi, tukamuepuka. Naye Mungu wetu Amekaa kando anatuangalis. Mvua za msimu hakuna. Zikija ni fupi au zina madhara. Wanawake hawaolewi. Watoto hawana mashiko. Wakubwa hatujui tena kitu ila AJIRA. HII ni kwa sababu usomi ndio sifa ya kuajiriwa bila kujali kuwa ulicho soma ndicho au sicho. Njia ya sawa na kunyooka marufuku, ila njia ya demokrasia.
LEO NJIA YA DEMOKRADIA ni nini?
Ni utawala wa wasomi wa akisekyula, kwa ajili yao hao wasomi wa akisekyula, na ikisimamiwa na wao hao hao wasomi wa akisekyula. Na wabunge wetu ni kundi hilo hilo, labda tuondoe wachache Mkulima, Kishimba n.k.......
Waalimu wao ni Wazungu. Washauri wao ni Wazungu.
Jamani kuna haja watu tukae chini. Kwani hata hilo bunge LA Ndungai, ni mithli yao WAZUNGU. Ndivyo Macauley alivyo shauri, watubadilishie mfumo wetu wa malezi, tuione vile vyetu ni vibaya na vile vyao ndio vizuri.
Ah!