Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Lakini mnasemaga bora demokrasia kuliko uchumi/maendeleo ya vitu. Kwamba gadafi aliwapa walibya kila kitu kasoro demokrasia hivyo wakamtoa. Sasa basi kuleni demokrasia itumieni kutolea pesa kwenye miamala yenu ya tigo na mpesa.
Hii kauli pana sana hadi uwe mwanafalsafa ndo utaielewa. Kwa kifupi ni hv. Uchumi wa nchi unajengwa na wananchi. Jukumu la raisi ni kusimamia haki basi. Akishindwa wananchi wanamtoa na kumuweka mwingine awawakilishe
 
Nadhani sasa mmeshajua mama anatupeleka wapi! Tusitishane..
 
SOMO KWA MAMA YETU MPENDWA RAISAT SAMIA:

Serikali yetu ni mfumo tuliorithi kwa wakoloni wetu. Bado kuwa HURU. Mama Raisat Samia amerithi tu. Tusitegemee maajabu. Ukipanda mgomba, utavuna ndizi. Mkoloni alipanda utawala huu ili avune bila jasho kwake.

Kwa hiyo msitegemee eti serikali itakuwa na jipya. LA! Kazi inaenda mbele, mpaka kije kizazi kitakacho ukataa UMANGI MEZA.

UMANGI MEZA.

Kila msomi akihitimu, ajira ndio tegemeo lake. Uzalishaji ni kile wakulima na wafugaji masikini walio mavumbini wazalishe. Sasa, huyu mhitimu wa vyuo vyenye mlengo wa kibepari, mtaalamu waziri wa fedha; atakuwa na akili gani nyingine?

Wenzake walikuwa wanavuta kwenye bia na vilevi. Yeye ameona a a! Hapa hapa kwenye mawasiliano. Kwenye vilevi angekusanya shs xxxx kwa mwezi. Sasa atakusanya xxxx mara7 wa 70. Tena asubuhi na mapema. Pesa bwana! Kila mbunge akimaliza kipindi hatakua ni wa kupewa gari na shs 350,000,000/-, bali na Jumba la kifahari kama marais wastaafu wanavyotunukiwa.

NINI?

Kesha maliza kazi ya huyu Muajiriwa namba Moja, raisi wetu. E e, tujiulize. Rais wetu ni muajiriwa namba 1, ni nami MUAJIRI WAKE?

Msilalamike sana jamani kwa sababu hii serikali ni ya Wasomi kwa ajili ya wasomi ikisimamiwa na wasomi. Ni MRADI WA WAZUNGU WAKOLONI. Wao wazingu ndio wametuwekea mitaala shuleni na vyuoni. Kwa hiyo serikali yetu sio -
1) Serikali ya Watu
2) Kwa ajili ya Watu na
3) Ikisimamiwa na Watu.
Ndio maana Mbunge muwakilishi wa watu, akiapishwa tu, anahongwa shangingi. Kwa mwezi atakusanya milioni 12. Hii ina maada kwa muhula wake atakuwa aneti shs 12,000,000x12x5.

Si hayo tu. Bali huyu muasisi wa mfumo huu wenye makengeza-
1) bunge,
2) serikali na
3) mahakama
ana wapigapiga mabegani wabunge WAKE, anaWambia: msijali. Ukimaliza kipindi utasainiwa milioni 500 take home.

Unafikiri atakuwa tena muwakilishi wa watu au kikaragosi cha mdude -SIWA {HESHIMA YA MALKIA}?

EE MASIKINI TULIO MAVUMBINI:

Kilio chetu sasa basi. Makosa ni yetu. Tukishamchagua rais na wabunge, hapo tunarudi vyumbani kuvuta blanketi. Kukoroma ndio kunako fuatia.

Hatuna utaratibu wakuona nini kinachoendelea. Eti tunasubiri maendeleo. Mnuka MAVUMBI MWENZETU hayati JPM, alikusudia kujaribu. Yuko MAVUMBINI tayari. Na roho yake bila shaka IKO PAHALA PAZURI HUKO KWA MUNGU. Na kaburi lake ni pana, lina taa na harufu nzuri. Kwenye kona kuna kichungu cha maji baridi na glasi. Kila pakiadhiniwa, hutembelewa na wageni wapya wapya, wazuri na wamebeba zawadi Humuambia usiwe na shaka, makazi yako peponi yaliandaliwa tangu hujazaliwa. Naye huwaambia asanteni. Nataka kuwaona baba na Babu zangu. Wanamjibu, twende.

Baada ya safari ya kutalii kuonana na wapendwa wake, pia aliwaona baadhi ya viongozi walio mtangulia mbele ya HAKI. Wako pahala poa, pana migomba iliyopangiliwa vizuri. Makondoo makubwa yaliyonona. Ah! Ni Patrice Lumumba, Abubakar Tafawa Balewa, Jumbe, Sokoine, Sankara, Gaddafi n.k, kuna wengine hakuwaona. Wakamwambia kesho.

Wakati wa kurudi, wanamwambia: hutaki kuwaona WATU wako (yaani Watanzania)?

Anamuona Sabaya wakimdhalilidha. Hayawi hayawi mbona yamekuwa. Basi akafunga macho ili asione mama ntilie kule wa Moro wakibanguliwa. DC na mhasibu wake wakapoteza ajira Oh! Soko LA Kariakoo likiwaka moto.


........JPM........Akawaza oh!
Dada SAMIA ...... Kazi iendelezwe: lakini si kihivi!
..........bila udikteta hatufiki.....
Wazungu ndio waalimu wa udikteta. Bila UDIKTETA MADINI YETU , PEMBE ZA NDOVU, GESI NA MAFUTA YETU WANGEVIPATA?
KILA KONA YA DUNIA WAMEEGESHA MAJEDHI YAO. HUU NI UDIKTETA, TENA WA MABAVU.

.........itaendelezwa.
 
KWA MAMA SAMIA:

Nchi hii inataka MTAWALA na sio MWANASIASA.

Siasa ilitufikisha kwenye SERIKALI YA WASOMI, kwa ajili ya WASOMI na ikisimamiwa na WASOMI.

WASOMI.wetu wanachojua ni AJIRA, na sio KUJENGA NCHI.

Wanachotaka ni MAISHA KAMA WAZUNGU na sio kuishi KAMA WATU.

RAIA 96% ni sisi WALALA hoi Mijini na vijijini. Katiba iliyopo haitufai, hata ile pendekezo LA WARIOBA, kwani ni ya WASOMI. Kazi yao ni kuproses njia ya Utajiri na Mali zetu kuvushwa kwenda Ulaya kupitia madirisha ya IDARA ZA UNUNUZI kwa kila WIZARA. Na kuagiza vitu vinavyo liwa na kutu kutoka ulaya, marikani na hivi sasa BRICS.

MAMA TUPE NAFASI SISI TULIOKO NG'AMBO YA BARABARA KUONYESHA KITU.

Asante.
 
Habari!
Naomba uzi huu na nyuzi zingine mithili ya hizi zinazopinga dhuluma kwa wananchi ziendelee kuwepo mpaka serikali itakapojibu hoja za wananchi.

Tulikuwa tukiambiwa kuwa kuna tozo za line za simu kulingana na kiasi cha vocha tunazoweka.
Huku tukilalamikia dhuluma hizi kabla ya kuanza utekelezaji wake tumepigwa kwa kodi ya miamala ambayo ni kubwa zaidi.
Hii ni dhulma. Kama mmeshindwa kukusanya fedha muombe ushauri kwa wananchi au muwapishe wengine. Sio dhambi kukubali kushindwa.
 
Tulia wewe libavicha! Mama anawakomesha mataga, sukuma gang na marehemu!

Anakusanya hela azimwage mtaani ili nyie mibavicha muwe mnaziokota!

Mwambie pia bavicha mwenzio Malisa aenendelee kuandika zile makala zake uchwara kwamba maama anaupiga mwingi!
 
Tulia wewe libavicha! Mama anawakomesha mataga, sukuma gang na marehemu!

Anakusanya hela azimwage mtaani ili nyie mibavicha muwe mnaziokota!

Mwambie pia bavicha mwenzio Malisa aenendelee kuandika zile makala zake uchwara kwamba maama anaupiga mwingi!
Yaani anawapora wananchi kidogo walichonacho ili awamwagie mabilioni na matirioni!!!
Ina make sense kwa akili yako ya ki UV CCM?
 
Tukila ugali tushibe vizuri alafu simu iwe na bundle la kutosha, hatudaiwi kodi nje tunayo Vitz tumepaki. Tunalipwa na serikali. Hela ya bia haipigi chenga alafu tunalo limchepuko la maana hapo limetuli. Kiujumla we have No stress😊😊😊

Kazi kubwa ambayo hua imebaki hapo ni kuilaumu serikali tuu.😀😀😀😀
Serikali ya Magufuli na Samia ilichukua tozo kwa walio jilimbikizia fedha za wananchi kiholela kwa sababu mbalimbali. Moja wapo ikiwa ni uzembe wa taasisi ya Urais. Kwa katiba ya nchi ilivyo, RAIS ni MTAWALA. Magufuli alipokaa kwenye hiyo nafasi, ikulu ikaonekana kwa watu wa kawaida. Maendeleo ya huduma na vitu tukaviona.

Serikali ya Samia na Nchemba (Magu alimtema), wao; wale Masharobaro wapigaji wakuu wa fedha za umma na wakwepaji wa kodi, wanakodishiwa ndege kwenda ng'ambo utalii wa biashara hewa. Magufuli alichosema biashara ya mahindi kwenda Kenya hapana. Bali tuwapelekee UNGA. Ni aibu tunawapelekea mahindi, wao wanayakoboa na pumba na viini wanatengeza chakula cha mifugo na kutuuzia kwa bei ya juu Mara tatu ya bei tuliyo wauzia mahindi. Hata Raisat SAMIA kwenye hotuba yake bungeni Nairobi, wabunge wakichekelea kuwa yeye SAMIA ni SULUHU (bure) na KENYATA ni UHURU (afanye atakavyo).

TUSIILAUMU SERIKALI BALI TUJIANGALIE UPYA KWA KUJIPANGA.

1) Tunahitaji KATIBA. Katiba IPO. Ni ya kale, sio mpya. Ina vitabu viwili.
a- KATIBA MAMA -Alipewa nabii Isa / Yesu ina Ibara 7 ufu 5:1, 6, 12. Ibara hizi saba zimefichwa kwenye kitabu cha mwanafunzi wa Madrasa Q1:1-7, kiitwacho Kanuni na Juz'u Amma. Hapo mwanzo kilikuwa kinaitwa KANUNI YA IHSANI (yaani kanuni ya kupiga kura ya ndio). Ndani yake kuna sehemu tatu-
i) kanuni ya MAISHA ya miji,
ii) katiba mama na
iii) elimu ya Uraia (juz'u tatu za sehemu ya kumi ya mwisho ya Msahafu uliotwaharika [maarufu siku hizi kwa jina la Qur'ani Tukufu]).

b) KATIBA MWENZA -Alipewa Muhammad. Ni elimu ya uraia (civics). Juz'u ya 30 (mambo yaweje), juz'u 29 (tubarikiwe) na juz' u ya 28 (watu tuwe wasikivu). Ina Ibara 1132

HII KATIBA INA SURA 58.

Ni kweli KATIBA ya nchi yetu haikidhi mahitaji; hasa ikiwa Rais atakuwa Mwana siasa. Ndio maana ulaya yote nchi nyingi zina wafalme. Na nchi zenye Rais, waziri mkuu ndiye mtawala. Japan kuna mfalme. Uchina rais ni wa kudumu. India wazir mkuu ni mtawala n.k.

Tumzingire Raisat Samia na tumuombe Mbowe na Chadema waone mbali na sio nyayoni mwao.

Wazungu wametukamia. Miaka 400 iliyopita walishajipanga. Download Lord Macauley, ripoti yake bungeni uingereza ya mwaka 1835, utachoka.

Mwaka 1884-5 mkutano wa Berlin wakajikatia maeneo barani mwetu bila kutushirikisha. Mwaka 1917, makampuni makubwa wakajikita kwenye mikataba baina yao jinsi ya kula keki (utajiri na Mali barani mwetu) bila kuzozana.
Mwaka 1949 wakahamisha miji mikuu ya dunia, badala ya kuwa Makka na Jerusalem, wakazua New york na Brussels.

Mwaka 2019 covid, walilenga itumalize watu weusi Afrika. Mbowe, Tundu, na MIMI; Tuwe macho. Siasa ni uongo.

Tutumie AKILI. Ndio maana wamefanikiwa kutupa uhuru wa Bendera kwa akili yao. Mpaka Leo tunalumbana kwa tamaa ya madaraka. Uh!

Lini tujenge nchi?

AKILI YAO:

Tumerithi mfumo wao wa utawala, wizara 23 Mji mkuu. Ndugu Ndungai anaomba apewe mpango mbadala wa tozo wabunge waliyoipitisha. Kwa fikra hiyo nampa dole. Hilo tutalifanya Mungu atujalie uhai.

Malezi, Mafunzo, Ulinzi, Biashara, Elimu, Kilimo, Michezo n.k, vyote ni replika. Tumewaiga. Kwa kuwaiga, Mungu wetu watu weusi, tukamuepuka. Naye Mungu wetu Amekaa kando anatuangalis. Mvua za msimu hakuna. Zikija ni fupi au zina madhara. Wanawake hawaolewi. Watoto hawana mashiko. Wakubwa hatujui tena kitu ila AJIRA. HII ni kwa sababu usomi ndio sifa ya kuajiriwa bila kujali kuwa ulicho soma ndicho au sicho. Njia ya sawa na kunyooka marufuku, ila njia ya demokrasia.

LEO NJIA YA DEMOKRADIA ni nini?

Ni utawala wa wasomi wa akisekyula, kwa ajili yao hao wasomi wa akisekyula, na ikisimamiwa na wao hao hao wasomi wa akisekyula. Na wabunge wetu ni kundi hilo hilo, labda tuondoe wachache Mkulima, Kishimba n.k.......

Waalimu wao ni Wazungu. Washauri wao ni Wazungu.

Jamani kuna haja watu tukae chini. Kwani hata hilo bunge LA Ndungai, ni mithli yao WAZUNGU. Ndivyo Macauley alivyo shauri, watubadilishie mfumo wetu wa malezi, tuione vile vyetu ni vibaya na vile vyao ndio vizuri.

Ah!
 
Ndugu watanzania imefahamika kwamba kumbe lengo la kushusha gharama za kuingiza umeme lengo lake ilikuwa ni kuongeza gharama kwenye matumizi ya unit kumbe kuanzia mwezi huu au ujao usishangae ukiweka Tshs 9000 unapata unit 25 tofauti na hapo mwanzo ambapo ktk Tshs 9000 ulipata unit 73.8kwh.hzo ndio akili za waziri wa fedha na viongozi wake.
 
Uchochezi Doti Com. Labda kushusha lakini si kuongeza. Narudia tena ni uchochezi.com
 
Ndugu watanzania imefahamika kwamba kumbe lengo la kushusha gharama za kuingiza umeme lengo lake ilikuwa ni kuongeza gharama kwenye matumizi ya unit kumbe kuanzia mwezi huu au ujao usishangae ukiweka Tshs 9000 unapata unit 25 tofauti na hapo mwanzo ambapo ktk Tshs 9000 ulipata unit 73.8kwh.hzo ndio akili za waziri wa fedha na viongozi wake.
Hii ni aina fulani ya umbea
 
Ndugu watanzania imefahamika kwamba kumbe lengo la kushusha gharama za kuingiza umeme lengo lake ilikuwa ni kuongeza gharama kwenye matumizi ya unit kumbe kuanzia mwezi huu au ujao usishangae ukiweka Tshs 9000 unapata unit 25 tofauti na hapo mwanzo ambapo ktk Tshs 9000 ulipata unit 73.8kwh.hzo ndio akili za waziri wa fedha na viongozi wake.
Sasa mkuu yaan elfu 9 unapata unit73 una lalamika wakati wengine elf 10 wanapata units 28.
 
Naandaa waraka kwa ndugu zangu wote ambaye atakuwa ccm mm na yeye tusjuane kuazia wazaz..lazma niwambie hiki sio chama ni kikundi cha wachache wahuni waliopo kwa maslahi yao na familiar zako over
Hilo mimi nilishamalizana nalo tangu awamu ya Magufuli na hasa baada ya oktoba 2020
 
Back
Top Bottom