Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Hakuna kutengua baki uko uko
 
Kwa vile wasomi wetu ni wahitimu wa elimu iitwayo elimu kwa UONGO 1 TIM 6:20, kujenga Nchi, wanacho kijua ni miundo mbinu kuboreshwa -miradi ya wazungu. Kwani vitendea kazi vyote shopping ni ulaya na brics.

Muda ifike kizazi kingine kije, chenye kutaka nasi tuwe na vyetu.

Kwa hiyo Leo tunamnyoshea Samia kidole, lakini ungekuwa wewe pahala pake, ungefanya nini? Si ajabu ni Yale Yale, au ikawa mbaya zaidi.

Naomba tuje na hoja kwamba, tumekosea wapi na ni nini kifanyike. Kisiki tulipo jikwaa, tukione; tuking'oe na tuchore plan ya jinsi tunavyotakiwa kwenda tufikie kufaulu.
 
Nasema samia achomoi

Njia zilezile za mtangulizi wake, il

Yeye ameenda mbali zaidi kukamua Ng'ombe asiye na ndama anaongeza tu makodi!

Kubebesha mizigo walala hoi na kuumiza wapinzania wake.

Hakika kwa anayeona mbali Samia achomoi.
 
Kwa vile wasomi wetu ni wahitimu wa elimu iitwayo elimu kwa UONGO 1 TIM 6:20, kujenga Nchi, wanacho kijua ni miundo mbinu kuboreshwa -miradi ya wazungu. Kwani vitendea kazi vyote shopping ni ulaya na brics.
We jamaa hii ilitakiwa iwe topic/uzi. Aisee nakussuport 100%
KAti ya comment nilizokua nazisubiria ni hizi
 
We jamaa hii ilitakiwa iwe topic/uzi. Aisee nakussuport 100%..
KAti ya comment nilizokua nazisubiria ni hizi
ELIMU IITWAYO ELIMU KWA UONGO:

1- Tunayo wizara ya ELIMU gagari.

Ee! Kwa kiingereza, tuna MINISTRY OF EDUCATION. Kwa kiswahili, hii ni WIZARA YA MALEZI.

Lakini wao, wameturithisha MINISTRY OF KNOWLEDGE. Yaani WIZARA YA ELIMU.

WAZIRI NDALICHAKO NA KAMATI ZAKE, wajiongeze. Miaka sitini baada ya uhuru wa bendera, Wizara mbona haijitathimini.

Kila mwaka wahitimu wanaongezeka mitaani. Miaka 15 iliyopita kuna mhitimu mmoja alikata tamaa, akajirusha kutoka juu ghorofani na akafa. No body cared.

2- Tunachotakiwa kuwa nacho ni Ministry of Education. Yaani Wizara ya MALEZI. Watoto mashuleni na vyuoni waleleke kukimu mazingira wanayoishi kwa kuboresha Yale wahenga wao, waliyokuwa wakiyaenzi. Hali ya kuwa wanaweza kufyonza mambo mapya na mageni yenye kuwafaa wao vizazi na vizazi. Na sio kukopi mitaala ya kigeni yenye mazingira tofauti na yetu.

Kwa mfano, mazingira yetu tuna ardhi, misitu, wanyama pori, samaki n.k. Pia tuna madini ya kila namna, gesi, mafuta na mawingu yenye mvua tele. Inakuwa ni aibu Waziri mwenye dhamani karne hii ana simamia mitaala tuliyo kopi au kuiga kutoka ulaya. Nchi ambazo mazingira yao ni ya kifukara -umasikini wa kutupwa. Nusu mwaka kwao ni barafu. Wengine nchi zaho miezi mitatu kila mwaka jua halionekani. Bahari zao hawana samaki. Wanyama pori kwao ni simulizi. Mafuta, gesi, madini kwao ni tamaa tu. Elimu yao ni kuwatayarisha vijana wao kuwa waajiriwa. Ndio maana walikuwa na Mapinduzi ya viwanda. Hii ina maana, kama mtu alitengeza viatu vitano kwa siku, akiwa kiwandani atatengeza viatu mia tano na au alfu tano kwa siku.

Kwa idadi hiyo SOKO alipate wapi?

Afrika!!!!! Ndio dumping ground.
Kwa hiyo nia ya kutupumbaza ikawepo, na ikatimizwa -rejea mkutano wa Berlin.

Hilo walifanikisha vipi?

Ni kwa kutushikisha ELIMU (bioloji, kemistre, historia, hesabu, n.k) IITWAYO ELIMU KWA UONGO. Tulipo ikiri elimu hii tumekosa IMANI 1 Tim 6:20.

TUNATANGAZA ~ Usichanganye dini siasa.

Serikali, chama, katiba, ikulu; havina dini. Download kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II mwaka 1953. Aliapishwa kuwa kiongozi wa kanisa na taifa.

SCOLARSHIP:

Ndio, kwa ELIMU YAKE YA BURE (SCOLARSHIP), wametuteka. Skolashipu ni madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya binadamu ....rejea wakolosai 2:8 (download hotuba ya Lord Macauley ya mwaka 1835, aliyoitoa bungeni uingereza.

Hakika wamefanikiwa kufuta UTATU MTAKATIFU -
1) MILA,
2) DESTURI na
3) JADI
uliokuwa rafiki kwa MAZINGIRA, na Leo tumekumbatia MIHIMILI MITATU YA NCHI isiyo na dini-
1) BUNGE
2) MAHAKAMA na
3) SERIKALI (katiba),
Faraka na ikhtilafu ndio wazungu wanatushajiisha tudumishe. Hali ya kuwa demokrasia-
1) serikali ya wasomi,
2) kwa ajili ya wasomi na
3) ikisimamiwa na wasomi -elimu ya Bure (elimu ya mateka [watumwa]), ndio kipao mbele cha jumba angamizi la UN NEW YORK {kiini kipya} Q14:28.

3- mh Ndalichako, jua kwa AFRIKA ni jina lililo toholewa, lenye maana ya KIPANDO CHA BURE ~A FREE CAR.

Sio shule tu, bali umma wa watu wetu, umepotoshwa mno; HATUJITAMBUI.

KWA HIYO MALEZI NI KWA WATU WETU WOTE, UPYA. NA HASA WASOMI- wsjitambue, wabadilike na waache mazoea.
Ili Raisat Samia ATUVUE UTU WA KITWANA NA TUVAE UTU MPYA - wakolosai 3:5-15- {Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katka nchi: uasherati, uchafu (kupiga ramli, kuomba kaburi), tamaa mbaya (upinzani), mawazo mbaya (njia ya wengi wapewe), na kutamani; ndiyo ibada ya sanamu; ...................}
 
OMBI LA SPIKA NDUNGAI, KUONYESHWA NJIA MBADALA YA KUKUSANYA FEDHA ZA KULETA MAENDELEO TUJENGE NCHI KATIKA KIPINDI KISICHO ZIDI MIAKA MITATU:

Ni rahisi kusema, lakini kutenda ni ngumu, pindi bado kujitambua kuwa serikali zetu tuliokuwa tumetawaliwa na Wazungu watawala, ni MIRADI YA WAZUNGU WAKOLONI.

Ndugu Spika, kila mwezi wa sita na wa saba, wewe, wasaidizi wako na wabunge; mnakaa Dodoma kwa vikao vya bunge na kutunga sheria na kugawa pato LA taifa trilioni 36 kwa WIZARA HEWA MJI MKUU, ili hali watu wako kwa DIWANI VIJIJINI. Makatibu wa Wizara wakizipata fedha hizi zimegawanywa kuwa ni za matumizi ya ndani na za maendeleo. Zote zinaishia kununulia vifaa kutoka kwa wafanya biashara wa ulaya. Miaka 60 baada ya uhuru hata ni wafanyi biashara wa ulaya ndio walichangia mamilioni ya fedha za uchaguzi. Magufuli serikali yake ikawakataa. Akajikita kwenye viwanda, tutengeze vifaa tunavyo vihitaji.

Oh! Wazungu wakahaha. Watawala wao bila shaka hawakulala. Magufuli yuko mavumbini. Watanzania wengi na siri nyingi hawazijui. Kumbe vifaa na bidhaa tunazo zinunua kutoka kwao, zenyewe ni vile vyenye kuliwa na kutu. Kila baada ya miaka michache vimeoza, ni kurepea au kununua vingine vipya. Barabara za lami ndizo usiseme. Ni matundu na matobo kila msimu ukibadilika.

Ndio maana wakitupa uhuru wa bendera walituchomekea mihimili mitatu ya nchi dhulumaji-
1) SERIKALI ISIYO NA DINI - Wizara 23 Mji mkuu na idara sake kurejelewa mikoani na wilayani. Mgao wa bajeti haufiki kwa Diwani WATU WALIPO.
2) BUNGE LISILO NA MENO- kutunga sheria na kuidhinisha utajiri wetu kuhamishiwa ulaya, marikani na sasa brics, kupitia makapu yenye matobo chini (Wizara na idara zake -idara za manunuzi).
3)MAHAKAMA- Udhalimu na ufisadi ulipojificha.
a) polisi,
b) mahakama na
c) jela
Ni utatu fisidi..........
Kwa khofu tumekaa kimya usije pelekwa jela, kupitia polisi na mahakama.

Kwa mihimili hii mitatu na wewe ukiwa ni mkuu wa muhimili wa bunge, ndio uchochoro wa zile trilioni 36, humwagikia kwa wazungu, miaka nenda rudi. Na hata Magufuli Alipotaka tuchukue hatua ya kupeleka unga badala ya mahindi KENYA, BUNGE lako mbona halijatunga sheria?

JUA!

Ndugu Spika, jua kwamba MFUMO HUU - serikali, BUNGE na mahakama, ni BATILI.

Unatakiwa ubadilishwe kabisa.

Kwa mfumo huu hata tozo likawa 20%, hatuchomoki.

Na Rais Hayati Nyerere kwenye kitabu chake MADARAKA MIKOANI, ibara ima ya 40 au 44, alisema Serikali ibadilishwe kabisa. Ña BUNGE LAKO pia kwa hilo, HAMKUTUNGA SHERIA.

SERIKALI YA WATU:

Ni muhimu Spika kutambua kuwa tuna SERIKALI ya wasomi wa elimu ya akidunia.

Tunahitaji SERIKALI YA WATU. Na hii usizembee, sheria ITUNGWE. Najua uko kwenye makamba uliyofungwafungwa na BUNGE LA EA na CW.

...... Watakushangaa

........itaendelezwa........
 
UMANGI MEZA BASI:

1- Serikali ya watu MJI MKUU DODOMA ina taasisi nne tu -
1) ikulu alipo rais wa kudumu. Hapigiwi kura ya ndio bali ni MTEULE. SERIKALI ni yake ndiye mwenye MAONO na kila mwaka Mara moja hulihutubia bunge pamoja na madiwani mipango mikakati ya taifa na ustawi wa jamii, vikundi hadi mtu mmoja mmoja. Malezi ya watoto, vijana na RAIA nishughuli ya IKULU. Idara ya mahakama na sharia (sio sheria) ikulu ndio chimbuko lilipo. Bajeti yake itatokana na Wizara ya hazina kwa kila nchi husika ya muungano. Na fungu LA kumi kutoka Wizara ya madini, gesi, mafuta na biashara.

2) jumba LA bunge alipo Waziri Mkuu. Yeye kapatikana kutokana na wabunge bungeni kwa kura za ndio na kuidhinishwa na Rais. Chini mitaani yeye ni MTAWALA. Amri 10 za Mungu kufuatwa na RAIA, ni ILANI ya Uongozi wa Ikulu. Na NJIA YA SAWA NA KUNYOOKA 1 Sam 12:23 Q 5:12, 6:151-153 kufuatwa, ni ILANI ya Jumba LA Bunge.

3) Wizara ya madini, gesi. Mafuta, viwanda na biashara kwa kila nchi miongoni mwa jumuiya.

4) Wizara ya Hazina- mkisanyo wa mapato yake yatatokana tozo za mazao ya mashambani (kwa mfano mtu akivuna gunia 10, atatozwa gunia moja), misitu, wanyama pori, mifugo, utalii n.k

Mji mkuu wa JMT na miji mikuu ya nchi za jumuia hapatakuwa na Wizara zingine. Umangi meza mji mkuu, mikoani na Wilayani, byebye.

Tukitoka Ikulu, next utamkuta DIWANI. Hakuna wakuu wa mikoa wala wa wilaya na ofisi zao. Wala halimashauri za wilaya n.k.

Je! Kwa namba hii hela tunayo, au la?

Tukitoka kwa Waziri mkuu next ni TARAFA (MBUNGE WA JIMBO). Hakuna wakurugenzi wa mikoa au wilaya na ofisi zao; ila HALIMADHAURI za miji.

Hela tunayo baba, tr 36-

Bungeni ni MBUNGE WA JIMBO anaye jibu maswali vipi atatumia fedha alizo omba kwa ajili ya vijiji, kata au tarafa, WATU WALIPO.

ONA!

Ndugu Spika, unaona MFUMO HUU? Una mihimili mitatu-
1) Taasii ya Rais mwenye Amri,
2) Hekima na
3) Katiba iheshimiwayo ufu 5:1, 6, 12; Q41:41
Kwa MFUMO HUU trilioni hizi 36, moja kwa moja zitafika kwa Watu Walengwa. Ni kwa muda mfupi Tutauepuka umasikini wa mavumbini, umasikini wa kutupa na imadikini wa utumwa wa kikoloni na wasomi wetu kuwa WAJASIRIA MALI.

UMEONA? Inaingia akilini au la? Hela nyingi unazo na kusaza.

Kule Watu walipo, mgao wa Mbunge na Tarafa pale kwa DIWANI utakuwa hivi-


Itaendelezwa
 

Kwamba mwendazake aliwafanya wazungu wakahaha 😂😂😂? Acheni kufuru kwa kutetea matumbo yenu kwa njaa zenu uchwara.

Huyo unayemsifia hapo alituaminisha Corona ni vita vya kiuchumi dhidi ya Tanzania, akujiita EA economic power house. Akatuaminisha barakoa, sanitizers, chanjo, PPE nk ni biashara za mabeberu!

Leo hii tuko maji ya shingo tunapumulia mashine ugonjwa umetuzidi kimo kwingine ni mwendo wa misiba misiba tu.

Sasa beberu tuliyekuwa tukimzodoa katuletea chanjo kumbe ni bure. Tumeshaumwa na nyoka sasa wanaogaha ni sisi kutafuta namna ya kuwabadili watu mitizimo yao iliyoathirika vilivyo na porojo za huyo bwana.

Kama ni legacy ya huyo mwenye faili lake mirembe, labda kama ni kukumbushana ukichaa wake?


Kwamba Ndugai anauliza wapi pa kupata pesa mbona hayo wameambiwa sana?

1.Kila mtu wakiwamo wao wabunge, Mawaziri, na vigogo wote wawe wazalendo tu kwa kulipa kodi ambazo hawazilipi.
2. Vipi pesa zinazoorodheshwa na CAG kuibiwa serikalini kila leo bila ya kuchukuliwa hatua zozote?
3. Vipi makampuni yanayozalisha hasara kila uchao?
4. Vipi pesa za kuwasafirisha washitakiwa feki kwenye chartered planes back and forth? Nani analipa pesa hizi na kwa faida gani?

Tumekuwa tukiwashauri wasisahau pia:

1. Kuziangalia upya kodi na tozo zote kuhusiana na uwepo wa janga la Corona. Uzalishaji umeshuka kodi na tozo kwa watu zinapanda vipi?
2. Vipi sisi tunajigharamia wenyewe kwa matibabu ya ugonjwa wa Corona mahospitalini wakati wao hayawahusu?

Au wewe unaonaje ndugu yangu?
 
Reactions: BAK
Kaka brazaj, ni kweli Magufuli aliwafanya wazungu kuhaha biashara zao, madini waliyokuwa wanajizolea kiholela, licha ya makenikia. Sina maana nyingine. Hilo tu, sina budi kuliona. Hakuna mtu aliye perfect na hakuna mtu ambaye hana jema. Tuepuke kusema mtu ubaya wake hasa akiwa mbele ya haki. Tambua kuwa IKULU ni taasisi. Kwa hiyo Raisat Samia siku 100 na hata Leo, tukimlaumu inaonyesha tusivyo makini kuelewa dunia ilivyo, kwetu sisi wenye kupokea UHURU WA BENDERA.

Wazungu, wazungu, wazungu hee!

CORONA - Magufuli alitoa angalizo kufuata ushauri wa kuvaa barakoa, kunawa n.k, n.k. Juu ya hivyo tujikinge kwa kutumia malimao, tangawizi na fusho. Kuna ubaya gani?

Leo Waziri wa afya anatuhimiza kuvaa barakoa bila kutupa agiza kudumisha kinga zile. Mambo yanaanza kulipuka. Nani alaumiwe? Magufuli alitunasihi tuvae barakoa zetu wenyewe, Leo ugonjwa unadaiwa kulipuka na wakuu wamejifunika na barakoa za kuagizwa nje.

Jamani tuwe wakweli wa NIA, MANENO na VITENDO.

Taifa la JMT linahitaji Mtawala kama Huseni Mwinyi. Mbowe la. Hapana tena na tena. Kuwekwa ndani kwake kwa vile tumesikia upande mmoja wa chadema, na serikali bado, sina hoja. Ila aachiwe bila masharti au afikishwe mahakamani, kieleweke. Ule uzungumzaji wake kwa waandishi wa habari kwa jeuri, dharau na matusi, kulidhihirisha Mbowe alikuwa na nia awekwe ndani ili vilio viweze kupokelewa nje.

KATIBA.

Kaka Braza J! Elewa kuwa katiba ni kama instructional manual book. Muundaji wa kifaa ndiye atoe kitabu.

Sisi watu mtengezaji wetu ni Mungu. Kwa hiyo, Mungu ndiye tutake kwake IMBOOK (KATIBA).

KATIBA IPO:

Nayo katiba alipewa Yesu katiba MAMA. Ibara saba (mihuri saba) ufu 5:1, 6, 12-
1) Uweza,
2) Utajiri
3) Hukumu,
4) Nguvu,
5) Heshima,
6) Utukufu na
7) Baraka;
Na Muhammad Katiba mwenza - elimu ya uraia Juz'u ya 30, 29, 28; ina jumla ya ibara 1132.

Katiba hii ni vitabu viwili katika kimoja.

Jumla ina Sura 58. Wazungu wameificha Q2:159 kwenye vyuo vya madrasa kuwa ni kitabu cha mwanafunzi kwa jina LA kanuni na juz'u amma.

Tuwe makini jamani. Tuko vitani, vita vya uchumi. Sio muda wa kunyosheana vidole.

Tusome jamani. Tulimnyoshea vidole Magufuli weeee, hadi wamemfikia na kusoma. What next, Samia?

Samia HOYE! TUMZINGIRE NA SI KUMKATISHA TAMAA. mimi akanipa nafsi yake, sikubali, labda ushauri. Lakini najua hapakaliki.

Ni moto wa kuotea mbali. Tunatakiwa tusome, Japan, Korea kisini, Singapore na sasa Vietnam na Dubai; kulikoni? Walifanyaje wakachomoka?
 
Suala la kupata mafanikio kuzijenga nchi zetu afrika, sio suala LA kimalumbano kati ya vyama tawala na upinzani. Ni JAMBO KUBWA zaidi ya vyama.
 
Wazungu, kamusi imefasiri neno hili kuwa ni WATU WENYE MBINU. Wao, kazi walishamaliza, wametuacha kupambana sisi kwa sisi, huku wakila uroda kwa gharama zetu.

Muhimu tutafute common ground.

Na hili haliwezekani kwani tuko mapote ya makundi lukuki ya kisiasa, kidini, kidhehebu, kiutaasisi na kimashirika. Na vyote hivi, utakutaa makao makuu yako nje ughaibuni.

THUS, FROM WHERE SHALL WE BEGIN?

Ewe Baba yangu, ulikuwa ukisema hata gombe gonjwa lililoachwa nyuma, nalo linatimua vumbi.

Nchi yetu tulishapotezwa njia.

TUANZIE WAPI?
 
Anatuvutuga tu yule mama. Ameapa kufuata na kusimamia katiba lakini sasa snasimamia akili zake. Vurugu zote hizi na Chadema ni kutokana na yeye kukiuka misingi ya katiba na sheria
 
Tumeingizwa cha walemavu bila kupenda Tu ataka katiba mpya na tume hulu ya uchaguzi
TUANZIE WAPI?
Hoja: Tuanzie kwenye KATIBA MPYA. Sawa, bali tujiulize; hiyo ya zamani ni IPI? Kwani katiba ya nchi tuliyo nayo, si yetu. Ilitayarishwa London mwaka 1959 kwa kusimamiwa na waziri wa mambo ya ndani wa uingereza wa wakati huo, wajumbe wetu walikuwa 9 au 11 wakiongozwa na Kambona.

Kwa hiyo, UPYA tutakaouzungumza ni UPI? Ukijua kwamba hii katiba ya nchi Toleo LA 1977 ni kisu wakoloni walitushikisha ili tujichinje wenyewe. Hali wao kwa raha zao wanavuna kupitia migongoni mwetu, usiku na mchana.

Wao kama nchi hawana katiba iliyoandikwa kwa mikono ya watu, ila biblia iliyonukuliwa na Mwafrika mwenzetu King James (gogo king James alikuwa mwafrika?). Ndivyo babu zetu kabla ya wazungu kutuvamia nchini mwetu, nao hawakuwa na katiba iliyo andikwa kwa mikono ya watu bali DESTURI. Sisi wazee wetu walidumisha UTATU MTAKATIFU WA KWELI-
1) MILA YA BABA WA IMANI NABII IBRAHIMU,
2) DESTURI (KATIBA IHESHIMIWAYO) na
3) JADI (BABU MKUBWA KATIKA UKOO, AU MFALME KATIKA TAIFA).

Kwa hiyo tukizungumzia KATIBA mpya, ni kutokana na KATIBA hii ya nchi au ile ya babu zetu weusi (DESTURI)?

Kutokana na ufafanuzi huu, tukubaliane kwamba, KATIBA ya nchi tuliyo nayo, SIYO.

KWANZA TUKUBALIANE HILO.

.......itaendelezwa
 
Sina mengi wakuu ila nauliza tu.

Naona karibia watanzania wote hawakubali namna serikali inayoendeshwa.

°Gharama za maisha kupanda... Hili limewagusa wananchi wote wa hali ya chini!

°Chanjo ya Corona pamoja na hatua mbalimbali zitakazochukuliwa kuhusu huu ugonjwa ambao nguvu kubwa ipo kwenye media huku wananchi wakishangaa tu.


°Anayotendewa mwenyekiti wa CHADEMA na mengineyo ambapo kuna kundi halipendezwi, pia tutaanza kumulikwa vibaya na wahisani/mabeberu pamoja na wakomunisti ambao tumeshaamua kuwafurahisha kupitia hatua mbalimbali za kicovid19

Nimeuliza hivyo sababu rais tuliye nae sio mvumilivu kuongoza watu wenye malalamiko na manung'uniko.

Nini kitaendelea endapo akijiuzulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…