We jamaa hii ilitakiwa iwe topic/uzi. Aisee nakussuport 100%..
KAti ya comment nilizokua nazisubiria ni hizi
ELIMU IITWAYO ELIMU KWA UONGO:
1- Tunayo wizara ya ELIMU gagari.
Ee! Kwa kiingereza, tuna MINISTRY OF EDUCATION. Kwa kiswahili, hii ni WIZARA YA MALEZI.
Lakini wao, wameturithisha MINISTRY OF KNOWLEDGE. Yaani WIZARA YA ELIMU.
WAZIRI NDALICHAKO NA KAMATI ZAKE, wajiongeze. Miaka sitini baada ya uhuru wa bendera, Wizara mbona haijitathimini.
Kila mwaka wahitimu wanaongezeka mitaani. Miaka 15 iliyopita kuna mhitimu mmoja alikata tamaa, akajirusha kutoka juu ghorofani na akafa. No body cared.
2- Tunachotakiwa kuwa nacho ni Ministry of Education. Yaani Wizara ya MALEZI. Watoto mashuleni na vyuoni waleleke kukimu mazingira wanayoishi kwa kuboresha Yale wahenga wao, waliyokuwa wakiyaenzi. Hali ya kuwa wanaweza kufyonza mambo mapya na mageni yenye kuwafaa wao vizazi na vizazi. Na sio kukopi mitaala ya kigeni yenye mazingira tofauti na yetu.
Kwa mfano, mazingira yetu tuna ardhi, misitu, wanyama pori, samaki n.k. Pia tuna madini ya kila namna, gesi, mafuta na mawingu yenye mvua tele. Inakuwa ni aibu Waziri mwenye dhamani karne hii ana simamia mitaala tuliyo kopi au kuiga kutoka ulaya. Nchi ambazo mazingira yao ni ya kifukara -umasikini wa kutupwa. Nusu mwaka kwao ni barafu. Wengine nchi zaho miezi mitatu kila mwaka jua halionekani. Bahari zao hawana samaki. Wanyama pori kwao ni simulizi. Mafuta, gesi, madini kwao ni tamaa tu. Elimu yao ni kuwatayarisha vijana wao kuwa waajiriwa. Ndio maana walikuwa na Mapinduzi ya viwanda. Hii ina maana, kama mtu alitengeza viatu vitano kwa siku, akiwa kiwandani atatengeza viatu mia tano na au alfu tano kwa siku.
Kwa idadi hiyo SOKO alipate wapi?
Afrika!!!!! Ndio dumping ground.
Kwa hiyo nia ya kutupumbaza ikawepo, na ikatimizwa -rejea mkutano wa Berlin.
Hilo walifanikisha vipi?
Ni kwa kutushikisha ELIMU (bioloji, kemistre, historia, hesabu, n.k) IITWAYO ELIMU KWA UONGO. Tulipo ikiri elimu hii tumekosa IMANI 1 Tim 6:20.
TUNATANGAZA ~ Usichanganye dini siasa.
Serikali, chama, katiba, ikulu; havina dini. Download kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II mwaka 1953. Aliapishwa kuwa kiongozi wa kanisa na taifa.
SCOLARSHIP:
Ndio, kwa ELIMU YAKE YA BURE (SCOLARSHIP), wametuteka. Skolashipu ni madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya binadamu ....rejea wakolosai 2:8 (download hotuba ya Lord Macauley ya mwaka 1835, aliyoitoa bungeni uingereza.
Hakika wamefanikiwa kufuta UTATU MTAKATIFU -
1) MILA,
2) DESTURI na
3) JADI
uliokuwa rafiki kwa MAZINGIRA, na Leo tumekumbatia MIHIMILI MITATU YA NCHI isiyo na dini-
1) BUNGE
2) MAHAKAMA na
3) SERIKALI (katiba),
Faraka na ikhtilafu ndio wazungu wanatushajiisha tudumishe. Hali ya kuwa demokrasia-
1) serikali ya wasomi,
2) kwa ajili ya wasomi na
3) ikisimamiwa na wasomi -elimu ya Bure (elimu ya mateka [watumwa]), ndio kipao mbele cha jumba angamizi la UN NEW YORK {kiini kipya} Q14:28.
3- mh Ndalichako, jua kwa AFRIKA ni jina lililo toholewa, lenye maana ya KIPANDO CHA BURE ~A FREE CAR.
Sio shule tu, bali umma wa watu wetu, umepotoshwa mno; HATUJITAMBUI.
KWA HIYO MALEZI NI KWA WATU WETU WOTE, UPYA. NA HASA WASOMI- wsjitambue, wabadilike na waache mazoea.
Ili Raisat Samia ATUVUE UTU WA KITWANA NA TUVAE UTU MPYA - wakolosai 3:5-15- {Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katka nchi: uasherati, uchafu (kupiga ramli, kuomba kaburi), tamaa mbaya (upinzani), mawazo mbaya (njia ya wengi wapewe), na kutamani; ndiyo ibada ya sanamu; ...................}