Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

 
ukishaona mtu yuko ccm usitegemee sana kauli zake kwani hata angekuwa malaika kuna fisi wengi wenye ushetani wamemzingira na hawapendi shauri zenye akili
 
Taifa limekabidhi roho yake kwa mabeberu na wanalichezea wanavyotaka. Leo hii tunapinduliwa na kugeuzwa kadri mabeberu wanavyotaka. Wanatulazimisha kupata mikopo kupitia chanjo za Kovidi 19. Watanzania nao wamezigomea.

Watanzania wanakamuliwa kodi za kila aina ambazo hazijabadilisha uelekeo wa maisha yao hata kiduchu. Ukiongea kodi, ukicheka kodi ukimtumia bibi yako hela ya ugolo anakatwa kodi. Lakini huduma za kijamii kama afya na upatatikanaji wa maji safi hakuna.

Ccm ya mama Samia haijajitanabaisha kuwa inataka nini juu wananchi wa kawaida. Maana matatizo yao ya kila siku yanaongezeka. Hawana uhakika wa kula, huduma za afya ni tabu tubu, ajira ni tabu tupu. Lakini hawajasikia mama Samia akisema ana mpango gani kuwanusuru.

Taifa letu kama watanzania limetwaliwa na wapigaji wachache. Tutumbue macho.
 
Kwa hiyo kwenda kuhudhuria MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA(UNGA) ni kuchezewa na mabeberu?!!!

Iko hivi.......

AJIRA
*******
Ilipita zaidi ya miaka 6 bila ya serikali kuajiri WATUMISHI wengi kwa mpigo...Awamu ya 6 imeanza kuajiri vijana zaidi ya 8000 (Tamisemi+Wizara ya afya)....

WATUMISHI NA MADARAJA
YA KAZI
********

Ni takribani miaka 6 watumishi wa UMMA walikosa kupandishwa MADARAJA YA KAZI...Serikali ya AWAMU YA 6 imewapandisha madaraja na kuwaahidi KUWAONGEZEA MISHAHARA ifikapo mwaka ujao wa fedha 2022/2023.

#SiempreJMT
#KaziIendelee
 
Taifa limekabidhi roho yake kwa mabeberu na wanalichezea wanavyotaka. Leo hii tunapinduliwa na kugeuzwa kadri mabeberu wanavyotaka. Wanatulazimisha kupata mikopo kupitia chanjo za Kovidi 19. Watanzania nao wamezigomea...
Ukimtazama Magufuli, Mkapa, Nyerere halafu uka-compare na huyu tuliyenaye ndo unajua nchi inapotea na iko mikokoni mwa outlier
 
Ukimtazama Magufuli, Mkapa, Nyerere halafu uka-compare na huyu tuliyenaye ndo unajua nchi inapotea na iko mikokoni mwa outlier
Nchi inapoteaje wewe jamaa?!!

Nchi ipo imara chini ya CCM.....

Waliofanya vetting iliyopelekea awe hapo alipo si "mazwazwa"....

Endelea kuufukuza upepo.....

#SiempreJMT
#NchiKwanzaKablaYaMaslahiKoko
 
Taifa limekabidhi roho yake kwa mabeberu na wanalichezea wanavyotaka. Leo hii tunapinduliwa na kugeuzwa kadri mabeberu wanavyotaka. Wanatulazimisha kupata mikopo kupitia chanjo za Kovidi 19. Watanzania nao wamezigomea...
Mzee wa legacy utahangaika Sana,irudishe kwenye muelekeo basi.

Kwamba wewe huoni viongozi kila siku wakitatua matatizo ya wananchi?

Lini hayo matatizo uliyoyataja yaliwahi pungua?

Kwa taarifa yako tuu sio Kazi ya Rais kukutafutia chakula,Wewe huoni vituo vya afya vikijengwa kila kona? Huoni miradi ya maji ikizinduliwa? Huoni mashule yakijengwa? Wewe uko nchi gani?

Mtoa mada acha upumbavu,Rais kamwe hatokuja mtaani kupandisha mabega kama yule mtu wenu,majigambo ndio mlizoea sasa hamyaoni yanawapa tabu.

Namba tuu ndio zinaongea 👇





 
Pale tumeingia cha kike.

Wa kulaumiwa ni ccm, kuweka viongozi kwa fadhila ama kufanya masihala na uongozi wa nchi hii.

Chini ya ccm hatutafika mahala popote. Yule mama hakuna kitu, hajielewi, hajitambui na wala hajui anafanya nini.

Tanzania sijui tunakosea wapi.
 
Mkuu,usimpigie Gitaa Mbuzi,hawezi kucheza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…