Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Namkubali rais samia kwa kila hali,,kutokana na utendaji wake wa kuendeleza alipoachia mtangulizi wake.
 
Kutoa ajira 8000 kwa vijana(TAMISEMI+ WIZARA YA AFYA) baada ya miaka 6 kupita bila ya ajira nyingi kiasi hicho.....mimi kijana wa KUPINGA HOVYO kutoka PINGA PINGA FC hapa "makao" Kinondoni nimempinga sana tena sana kwani HAIWEZEKANI ATUPORE HOJA YETU YA KUWA SERIKALI HAITAKI KUAJIRI VIJANA KABISA....yaani Rais SSH AMEIPORA HOJA YETU KABISAAAAA......


#PingaPingaFC
 
Hili la kufuta TASK FORCE za TRA na kuwakumbusha TRA kukusanya KODI kwa akili nyingi bila ya MAGUVU MENGI....hakika hili limenifanya nimpinge sana mh.Rais SSH kwani SISI PINGA PINGA FC ametupora hoja zetu za KUILALAMIKIA SERIKALI JUU YA HAYO......

#PingaPingaFC Member
 
Kupandishwa MADARAJA WATUMISHI WA UMMA......

Haiwezekani hawa WATUMISHI wa umma wapandishwe madaraja....bora wangebaki vilevile tu kama miaka 5 iliyopita.....

HAPA MH.RAIS SSH "ameniangusha mnoooo"

NDIMI PINGA PINGA FC MEMBA
 
HuweI kuwa ccm halafu usiwe katili , haijawahi kutokea
Huwezi kuwa CHADEMA halafu ukakosa kuwa "MSUKULE "wa mh.Mbowe.....kwa mwanachadema Mbowe hakosei lolote lile.... ni zaidi ya waasisi wa taifa hili......
 
Nampinga mh.Rais SSH KUENDELEZA UJENZI WA BWAWA LA UMEME MWALIMU NYERERE....

Haiwezekani mh.Tundu Lissu alipinge bwawa hilo kwa "kulobby" wabunge wa CDU kule BUNDESTAG(ujerumani) marafiki zake David Mc Alister kwa hoja za UHARIBIFU WA MAZINGIRA halafu mimi "msukule" hapa "makao Kinondoni" nisimuunge mkono....HAIWEZEKANI.....

Yaani Tanzania iwe na umeme wa uhakika MEGAWATI 2200 ?!!!!

Tuendelee tu kuwa hivihivi na UMEME WA MASHAKA TU....

Napendekeza Mh.SSH ausitishe mradi huo mara moja........

NDIMI PINGA PINGA FC

NDIMI MPENDA MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO

NDIMI MTAKA KATIBA MPYA HATA KWA KUMWAGIKA DAMU YA WATANZANIA WASIO NA HATIA

NDIMI MTAKA KATIBA YENYE SERIKALI YA MAJIMBO
 
Rate ya uharifu imepanda mno,wanainchi wameanza kukabwa na kuvunjiwa nyumba zao,hajalisemea lolote hili
 
Nimempuuza Mh.Rais SSH kwa hili...

KUTOA FEDHA ZA MWENDELEZO WA MRADI WA SGR NA KUNUNUA TRENI ZA UMEME ZA SGR TOFAUTI KABISA NA TRENI ZA SGR ZILIZONUNULIWA NCHINI KENYA(Diesel powered engine).

Tanzania SGR imegharimu DOLA BILIONI 1.92...Kenya imegharimu DOLA BILIONI 3.8....

SGR ya Tanzania ni ya UMEME...
SGR ya Kenya ni ya INJINI YA MAFUTA......

SGR ya Tanzania treni la abiria litakwenda kilomita 160 kwa saa....

SGR ya Kenya treni la abiria litakwenda kilomita 120 kwa saa....

SGR ya Tanzania treni la mizigo(freight) litakwenda kilomita 120 kwa saa....

SGR ya Kenya treni la mizigo(freight) litakwenda kilomita 80 kwa saa.....

Kwanini mh.Rais wetu ASIUFUTE HUU MRADI ILI TUSIWAPITE WAKENYA....yaani tuwapite wakenya hivihivi tu?!!!🤣🤣🤣

NDIMI PINGA PINGA FC MAKAONI KINONDONI
 
Mr. Sound umetumia neno kali kidogo jaribu kuwa na Adabu na mkuu wa nchi. Mwenzio mch. Msigwa kaitwa polisi kwa tweet tu.

Mimi napenda sana mh. Mkuu wa nchi

Asimamie aliyoiita vibrant democracy kwa kusaidia Swala la la Mbowe.

Matatizo yetu mengi ya kutofuata sheria,kanuni na taratibu watu bila kuwajibishwa yanatatuliwa na Katiba mpya. Ningependa kabla mama hajamaliza miaka yake kumi awe ametuwekea kitabu kipya cha kutuongoza Tanzania sio kisiwa dunia ni kijiji na mbaya zaidi information zina transcend haraka sana yale yaliyotokea Arab spring tujiepushe nayo yanweza kuja kutokea hata hapa kwetu na kwa akili na ufahamu wa watu wetu yanaweza kuwa na outcome mbaya zaidi.

Siamini sana kwenye uwekezaji huu kama wa wachina hawa na wahindi wanaokuja kunyonya wananchi. Serikali iwezeshe zaidi wananchi waweze kuwa na mitaji riba za mikopo zipungue na utalaamu. Sekta zote haswa kilimo. Ikiwa Philipine anauza mchele ulaya mchele wa mbarali sijui unashindwaje kwenda kuuzwa hata Morroco na Tunisia tuu.

Serikali ipunguze watumishi wasio na tija bali wapo kisiasa hii yote ni kupunguza matumizi. Mkoa tulihitaki DEd tu anatosha hawa wakuu wa mikoa,wilaya, katibu sijui wote wangeenda kujiajiri mambo wanayoyahubiri wakiwa majukwaani. Too much chawaz u know.

Fedha ya serikali kuwe na ukali na ufuatiliaji wa kimfumo na kibinadamu isifujwe. Mfano sasa hivi kila siku watumishi wanatoka dodoma kuja dsm bila sababu za msingi. Kipo kisa kimoja mkoa mmoja jengo haliishi huku serikali imetoa fedha lakini mkandarasi fedha halipwi kufauatilia kumbe Mkurugenzi anazungushia hela kkoo kwenye biashara zake.

Waziri wa fedha ame underperform sana simply gharama za vitu vyote kuanzia vyakula, umeme, ujenzi,mbolea, spare,pembejeo,dawa vimependa ghafla kila wiki. Kunahitajia ultimate intervention hata ya ubabe vitu vispande hovyo. Maisha mtaani yanazidi kuwa magumu ili hali mishahara haiendani na bei ya vitu.

Bado tunapenda tusikie mara kwa mara performance ya mabalozi wetu maana wanalipwa na watoto wanasomeshwa lakini output yao bado ni storiii tuu. Na hata watanzania wanapopata matatizo mabalozi huwasikii wakitia jitihada. Kuna dogo kapigwa risasi marekani ikabidi upitishwe mchango wa nauli ya kuja kuzikwa nyumbani hii nia aibu kwa nchi. Wote tu ajua hakuna wawekezaji wazuri wenye manufaa kwenye ajira kama wazungu kuliko wachina na mataifa mengine. Balozi zetu zichangamke zilete wawekezaji. Mfano Hakuna mwekezaji aliinua wafanyakazi kama Barrick, Twiga cement lakini sio wahindi wa Tanzanite one, Sio Dangote mpopo. Wawekezaji kabobo wala wasitupotezee muda tutachosha wanachi wetu bure.
 
Sijawahi kumpuuza na sifikirii kumpuuza
 
Mbaguzi wa kijinsia wa wazi wazi. Watendaji humo serikalini anajaza wadangaji tu hakuna la maana ndo maana uchumi unadorora kila uchao na maamuzi hayaeleweki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…