Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Muachieni Mbowe

Sio mnatesa watu halafu mnajifanya kumlilia Mungu
 
Mama Samia ana dhambi kubwa mbele za Mungu kwa kuutweza utu wake.

Binadamu wote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Anayemtweza binadamu mwenzake, anajitweza mwenyewe, na anamtweza Mungu Muumba wetu aliyetufanya tuwe tofauti na chochote, na akatushirikisha katika ukuu wake.

Ameutweza utu wa baadhi ya watu, kwa kuruhusu watu wabambikiwe kesi za uwongo. Aliishia tu kuwalaumu polisi bila ya kuchukua hatua. Ameutweza utu wa watu wengi, vijana kwa wazee, watu wa kawaida mpaka maaskofu na mashekhe, akaruhusu wawekwe mahabusu kwa sababu tu walikuwa wamejiandaa kuhudhuria kongamano la katiba. Watu hao hawakuwa na hatia yoyote.

Ukipewa mamlaka yanayokupa haki ya kuzuia watu kuonewa, lakini ukakaa kimya kwa kusingizio kuwa siyo wewe, ilihali umepewa wajibu, ni sawa na kuyabariki na kuyakubali matendo yale maovu.

Ukiwa kiongozi una wajibu ulio mkubwa kuliko watu wengine. Na wajibu huo usipoutimiza kikamilifu, huwi tofauti na mhalifu.

Kama unataka utu wako uheshimiwe, anza na kuheshimu utu wa watu wengine, hata kama dhamira yako haifurahiwi na yale wasemayo au watendayo, alimradi hawavunji sheria.

Viongozi wote watambue kuwa wana wajibu kwa wanaowaongoza. Na wajibu huo, maadamu umeyakubali mamlaka ya kuwa kiongozi, hauwi tena ni takwa la hiari, bali ni wajibu wa lazima.

Lazima Rais Samia atambue ana wajibu:

1) kuhakikisha watanzania wote wanatendewa haki. Polisi hawawabambikii watu kesi. Wateule wake hawawapori watu mali zao wala kuwatendea watu isivyostahili. Hao wote, iwe polisi, TIS, magereza, maDC, maRC, mawaziri, wakitenda maovu, ni sawa ametenda yeye. Au la awachukulie hatua madhubuti hasa ambazo zinapeleka ujumbe kwa watu kuwa hawa wayatendayo, siyo niliyowaagiza. Polisi wakiwabambikia watu kesi, Rais akawa kimya, maana yake watu hao wamebambikiziwa kesi na Rais. Watu hawakuwachagua Polisi, walimchagua Rais. Yeye ndiye aliyewaajiri Polisi.

2) kuhakikisha Watanzania wanapata huduma zao muhimu, pamoja na matibabu, umeme, maji, n.k. Kutokuhakikisha hayo, na kuridhika, ni kutotimiza wajibu.

3) kuhakikisha wananchi wanatengenezewa mazingira ya haki ya kuongoza nchi na jamii zao kwa haki, uhuru na usawa. Asipohakikisha hayo, kwa nafasi yake, anakuwa ametenda uovu.

4) kuhakikisha haki na uhuru wa watu unalindwa, alimradi uhuru huo haukiuki sheria. Asipofanya hivyo hastahili kuwa kiongozi. Na watu wakinyimwa haki na uhuru wao na chombo chochote, yeye ndiye anakuwa mwovu mkuu maana hao wote ni wateule wake. Anaposhindwa kuchukua hatua dhidi yao maana yake ameridhia na kubariki uovu ule.

Wananchi, wakati wote tusipotendewa haki, mtu wa kumbana ni Rais. Huyo ndiye zao la matakwa ya wananchi, hata kama tunafahamu uchaguzi wa 2020 ulivurugwa. Sisi hatukumchagua waziri, IGP, Mkuu wa Magereza wala majaji. Wakivurunda majaji, polisi, mawaziri, maRC, maDC, wakurugenzi, aliye halali yetu, kwa lawama zetu zote na hatua nyingine zozote, ni Rais.

Hao wengine atajuana nao yeye. Uovu wa polisi, ni uovu wa Rais. Uovu wa majaji ni uovu wa Rais, uovu wa mawaziri, ni uovu wa Rais, uovu wa maDC na maRC, ni uovu wa Rais. Tuliye na haki naye kumwajibisha ni yule tuliyempa mamlaka, na siyo mtu mwingine. Polisi wakiwabambikizia kesi Raia na majaji wakala njama za kutengeneza mashahidi bandia, lawama zetu ni kwa Rais maana ndiye anayeteua makamanda na majaji wote.

Mkitaka kupambana na anayewaonea, msitawanye mishale.
 
Nilijuwa unaandika kitu cha maana kumbe unaharisha tu hapa gaidi unataka asihukumiwe kunyongwa mwizi asihukumiwe ? Acha ujinga mwache rais afanye kazi yake tena unamuhusisha na mambo yasiyo mhusu liacheni tu hil gaidi lenu liadhirike limeua limetesa limepoteza watu halifai muulize sumaye alponea chupuchupu uenyekiti unamfanya aue wenzie kama ataishi milele mbowe hafai kuishi duniani
 
Uzuri ni kuwa Rais anafahamu kuwa ndani ya Taifa hawakosekane wendawazimu na majuha. Nawe atakusoma, na kukudharau, maana anajua ushauri toka kwa mwendawazimu, hauna maana zaidi ya kuwa kipimo cha kufahamu mwendawazimu yupo kwenye hatua gani.

Acha walio wazima wajadili hoja.
 
HAAA yaani huo uharo hapo juu mtu kajipinda kuandika kama katoka kirabuni nani anataka?
 
Binadamu hatukuumbwa kwa mfano wa mungu. Sisi waislamu tunafundishwa mwenyezimungu hafanani na chochote.

Labda kama unamaanisha mungu mwingine lakini si yule mmoja ambae hakuzaa na wala hakuzaliwa
 
Niujinga na upumbavu mkubwa mmmno kusema ama kuwaza eti binadamu anamdhalilisha/anamtweza Muumba.

Hakuna binadamu anaweza kufanya hayo! Wewe sema tuu anamkosea inatosha.

Tuchunge ndimi zetu zisiwendeeefu sana.
 
Niujinga na upumbavu mkubwa mmmno kusema ama kuwaza eti binadamu anamdhalilisha/anamtweza Muumba.
Hakuna binadamu anaweza kufanya hayo!!! Wewe sema tuu anamkosea inatosha.
Tuchunge ndimi zetu zisiwendeeefu sana...
Siifahamu imani yako, lakini yangu mimi, kuna andiko linasema:

Mathew 25
34“Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, ‘Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

35Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha; 36nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’ 37Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji? 38Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? 39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’ 40Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’

Hivyo, kila uletendalo dhidi ya mwanadamu mwenzako, liqe jema au zuri, umemtendea Mungu mwenyewe.
 
Reactions: PNC
Tulia kamanda, mahakama iko huru. Mama anaupiga mwingi.
 
Usiwe mvivu kutafakari neno pia omba hekima ya kulielewa neno!

Ukiua/ukimpiga mtu unakuwa umeee?

Watu wangu wanaangamia.
 
Tuache kujifariji,Kwa kweli huku mitaani kuna kelele nyingi za wananchi juu ya mambo mengi.

Wanalalamika juu ya vitu kupanda bei, shida ya umeme, maji nk. Ni kweli serikali yetu inafanya maendeleo mengi na bado kuna miradi mingi inayoendelezwa,lakini bila kujibu malalamiko ya watu, haya mengine yote hayatatuliza mioyo ya watu.

Kwa mfano kuna hili la bei juu ya mbolea, limewachanganya wakulima na kiukweli wanajiuliza maswali mengi sana bila majibu ya uhakika.watu wanaponung'unika juu ya serikali yao si jambo la kufumbia macho.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Tunatumia muda mwingi kupromote na kutetea mambo ya hovyo kwenye jamii.

Yani asiyefuata maadili anaenda kuchanganywa na wanaofuata maadili baada ya miaka 10 wote unakuta wameoza.

Wamemwandaa nani wa kuacha shughuli zake alee hao watoto watakao zaliwa na kuachwa na wazazi wao? Maana baba ataenda jela miaka 30 na mama atarudi shule.

Muda si mrefu na haki ya vilainishi itaruhusiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…