Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anaekubalika ni nani?
 
Kwa sisi tuliopitia machungu ya mwendazake direct, kwakweli tunampenda
 
Vipi kuhusu hili la kuwavalisha madera na vijora haters wake wote?
 
Mambo aliyoyafanya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni ngumu Sana kuyamaliza hapa, Hivyo nitajitahidi kuyaelezea kwa kadri nitakavyoweza,

Wakulima. Hapa mh Rais wetu mpendwa amewagusa wakulima ambalo Ni kundi kubwa Sana, Hapa mh Rais wetu ametoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa laki na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70, Hali hii imewagusa Sana wakulima na kukonga nyoyo zetu wakulima Hadi tunatamani uchaguzi uwe Leo ili Tumlipe kwa kumpigia kura za kutosha Kama asanteeeeeee,

Pili mh Rais wetu mpendwa mama Samia amewagusa Sana watanzania hasa wanaotoka familia masikini na familia nyonge kwa uamuzi wake wa kutoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita na gharama zake kubebwa na serikali yetu sikivu, hapa kiukweli Rais wetu amezigusa nyoyo za watanzania wanyonge, Jambo hili limetoa nuru na mwanga kwa watanzania wanyonge

Katika Afya. mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania Amechukua hatua za kujenga vituo vya Afya kila Kona ya nchi hii, mfano majuzi tu hapa vituo vya Afya takribani 234 vimejengwa hapa nchini, hii imegusa maisha ya watanzania wanyonge kwani hii imerahisisha upatikanaji wa huduma karibu na mwananchi na kupunguza safari za kutembea umbali mrefu kutafuta na kupata huduma, Jambo hili limegusa Sana mioyo ya watanzania wanaoendelea kumshukuru mh Rais na Kuendelea kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania

Nitaendelea
 
ametoa ajira 50+ kwa watoto wa maskini

kayafa au kwa jina lingine mfalme juha alifanya nini cha kuwagusa wananchi wa chini zaidi ya kutengeneza maskini wengi?
 
Swala kubwa alilofanya katika awamu yake ni Kuanzisha tozo basi.....
 
Elimu bure=Mwendazake alisimamia hili sio yeye
Hajapandisha chochote ilikua ni uhuni tu nasema wananchi wa chini sisemei watumishi ambao ni kundi la wanaofaidi nchi sijui unaelewa nilichouliza na unachojibu??Hapa nazungumzia wananchi sio watumishi ww ni wa wapi?
Kodi ndo wananchi wanazifaidi??Toa hoja acha uongo?Nilichouliza ni tofauti na ulichojibu
Ajira zipi wewe unataka makofi au kwanini unaongopa kumpamba huyo bibi uwongo?
Mabarabara ni ajenda ya mwendazake na Jk tokea huko zake ni zipi

Madarasa yanajengwa tokea enz za jk na shule za kata wala hajaleta yeye
 
Vituo vya afya ilikua ni ajenda ya mwendazake na sio yeye

Suala la mbolea siyo yeye acheni utapeli hakuna mbolea iliyoshuka
 
Elimu bure ililetwa tokea mwaka 2015 na sio yeye ililetwa na mwendazake na ndo alisimamia hili yeye samia hajaja na sera ya elimu bure wacha kudanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…