Mambo aliyoyafanya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni ngumu Sana kuyamaliza hapa, Hivyo nitajitahidi kuyaelezea kwa kadri nitakavyoweza,
Wakulima. Hapa mh Rais wetu mpendwa amewagusa wakulima ambalo Ni kundi kubwa Sana, Hapa mh Rais wetu ametoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa laki na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70, Hali hii imewagusa Sana wakulima na kukonga nyoyo zetu wakulima Hadi tunatamani uchaguzi uwe Leo ili Tumlipe kwa kumpigia kura za kutosha Kama asanteeeeeee,
Pili mh Rais wetu mpendwa mama Samia amewagusa Sana watanzania hasa wanaotoka familia masikini na familia nyonge kwa uamuzi wake wa kutoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita na gharama zake kubebwa na serikali yetu sikivu, hapa kiukweli Rais wetu amezigusa nyoyo za watanzania wanyonge, Jambo hili limetoa nuru na mwanga kwa watanzania wanyonge
Katika Afya. mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania Amechukua hatua za kujenga vituo vya Afya kila Kona ya nchi hii, mfano majuzi tu hapa vituo vya Afya takribani 234 vimejengwa hapa nchini, hii imegusa maisha ya watanzania wanyonge kwani hii imerahisisha upatikanaji wa huduma karibu na mwananchi na kupunguza safari za kutembea umbali mrefu kutafuta na kupata huduma, Jambo hili limegusa Sana mioyo ya watanzania wanaoendelea kumshukuru mh Rais na Kuendelea kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania
Nitaendelea