Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

ametoa ajira 50+ kwa watoto wa maskini

kayafa au kwa jina lingine mfalme juha alifanya nini cha kuwagusa wananchi wa chini zaidi ya kutengeneza maskini wengi?
Ajira zipi hizo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwani kayafa nae si alidanganya katoa ajira 50 elfu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mwendazake na Samia tofauti ni ndogo sana kwani huyu angalau yeye hateki wala kuuua kama lile zimwi la chato but kwenye uchumi she is good for nothing
 
Elimu bure ililetwa tokea mwaka 2015 na sio yeye ililetwa na mwendazake na ndo alisimamia hili yeye samia hajaja na sera ya elimu bure wacha kudanganya
Kwanza wewe bila Shaka huelewi masuala ya kisiasa na uongozi, Mama Samia Ni wa chama gani? Hayati Dr Magufuli alikuwa wa chama Gani? Alikuwa anatekeleza ilani ya chama gani? Elimu bure ilikuwa Hadi kidato Cha ngapi? Tanzania Kuna mgombea binafsi? Umewahi msikia mgombea binafsi? Umesoma katiba yetu? Acha kutoa aibu hapa
 
Vituo vya afya ilikua ni ajenda ya mwendazake na sio yeye

Suala la mbolea siyo yeye acheni utapeli hakuna mbolea iliyoshuka
Wewe Ni mkulima? Unajuwa mbolea kwa Sasa Ni shilingi ngapi? Unajuwa msimu uliopita ilikuwa shilingi ngapi? Kwani Hayati Magufuli alikuwa wa chama gani na alikuwa anatekeleza ilani ya chama gani? Acha kujianika ipeo wako wa kifikra hapa na kuonekana bado hujakuwa kifikra na upeo wako ni mdogo
 
mwanangu alikuwa ajapanda cheo tokea awamu ya tano, alivyoingia Samia kapanda cheo, mtoto wa mdogo wangu pia kapata ajira ya ualimu mkoani,kipindi Cha dikteta no ajira
 
Acha hasira zako hapa wewe kwani hukuona ajira za ualimu na Afya zilizotolewa na serikali ya mama Samia? Ulikuwa unaumwa wakati zinatoka? Au hupo Tanzania? Bila Shaka wewe siyo mtanzania Ndio maana huelewi yanayoendelea hapa nchini kwetu
 
Hakuna hata kimoja zaidi ya kumumiza na tozo na Kodi,fukuza wamachinga.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Tozo Ni kwa ajiri ya maendeleo ya nchi yetu, Hata mataifa ya ulaya yalipita njia hii katika kuzijenga nchi zao, walijinyima na kujibana ili kujenga nchi zao, hata sisi lazima tujibane na kujinyima ili kulijenga Taifa letu, wajibu wetu Ni lazima tuubebe katika mabega yetu, lazima tuutimize wenyewe, lazima Tufahamu kuwa hakuna mbadala wetu katika ujenzi wa Taifa letu,

Suala la machinga naona Napo unafanya upotoshaji wa kizamani, mh Rais wetu mpendwa mama Samia alikutana na viongozi wa machinga na kufanya nao mazungumzo na kutoa maagizo kwa viongozi wote nchini katika halmashauri kuhakikisha kuwa kunakuwepo na utaratibu mzuri wa kuwapanga machinga maeneo yanayofikika vizuri na yatakayokuwa salama, Ndio maana unaona namna machinga wanavyoendelea na biashara zao vizuri bila shida Wala bugudha, ndio maana hujaona vurugu zozote zilizofanywa na machinga maana vijana wameridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
 
Amefanya mengi mno

1. Ajira
2. Nyongeza ya mshahara
3. Barabara zimejengwa nyingi tu.

4. Amepanua wigo wa treni mwendokasi na mabasi ya mwendokasi.

5. Amejenga diplomasia baina ya nchi ya Tz na nchi nyinginezo.

6. Madarasa yamejengwa kwa kasi
7. Royal Tour imechangia watalii kuongezeka

Aisss yako mengi sana
 
Mnahangaika bure kwani hakuna marehemu aliyewahi kufufuka zaidi ya kristo.
Enyi wafuwasi wa Kayafa ifike mahali mkubali matokeo.
Yule dhalimu hawezi kurudi tena.
Wasalimie usukumani mkuu.
"Mwangaluka mayoo"
 
Huu ni mjadala makini, lakini najuwa hauwezi kwenda popote kwa jinsi JF ilivyo siku hizi.

Ngoja nami niache uchafu wangu hapa"

1. Kafungua nchi iliyokuwa imefungwa ili kila matakataka yanayotaka kuja yaje kuwadidimiza wananchi wa kawaida kabisa. Yeye anasema hawa wananchi watapata ajira, kwa hiyo maendeleo yatakuwepo makubwa sana.

2. Anahimiza tupeleke gesi kwa majirani, ili wakishaitumia wananchi wetu wengi watapata bidhaa zilizotengenezwa huko, kwa hiyo maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa yameguswa kwa kila njia.

3. Wachuuzi wetu sisi wenyewe, kama akina Roast, milango ya wao kuneemeka kwa ziada ipo wazi. Hawa wakishapata neema tu, mwananchi wa kawaida atakuwa amenufaika kwa kupewa viperemende vya hapa na pale.

4. Nashangaa sana mara hii tu mleta mada umekwishasahau neema inayotokana na "Royal Tour"? Binaadam kweli hamna shukrani nyie.

5. Mwisho, Zanzibar inameremeta kwa manufaa makubwa yanayotokana na juhudi za mama kuhakikisha kila fursa ipatikanayo ni haki ya Zanzibar kuchukua haki yake hata kama ni deni litakalotakiwa kulipwa na walalahoi wa linchi kubwa lisilokuwa na kitu kichwani.

Sasa, kama yote haya wewe bado huoni alichofanya cha kutikisa sana, wewe utakuwa na kipimo chako ambacho ni cha kipekee sana.
 
-Watu hawabambikiwi kesi kifalafala
-Watu hawaporwi mali zao hovyohovyo
-Watu hawauawi kijingajinga

Oops, sorry umesema kimoja tu. Nimejikuta naanza kutiririka baada ya hasira kunipanda ghafla nilipolikumbuka lile nduli liuaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…