Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Sasa unafikiri nani atakukomboa? Twendeni na Samia tu hamna namna.
 
Wale usiende mbali, nenda njia ya Banana tu kuelekea Kitunda ukaona show, kuna mahandaki kama sio nyuma tu ya Airport.

CCM OYEEEEEEEEEEEEE
Ccm mbereee kwa mbeeeeeeee, au nadanganya ndugu zangu?
 
Huyo mama anatuvusha wapi .
Hata ukiweka jiwe hapo ,CCM itakuambia twende na jiwe litatuvusha.
 
Nasikia na barabara zenu zote zimepigwa lami na maji yanamwagika
Hahahahaa.

Barabara ya lami ni inayounganisha mkoa na mkoa mwingine tu kama ilivyo Morogoro road tu
 
Lawama zielekezwe kwa CCM, wanapeana vyeo na madaaraka kishikaji, wameyaweka majeshi yote mfukoni, demokrasia wameiweka mfukoni, Mahakama na bunge vipo Chini yao,

CCM ndo adui mkubwa wa nchi hii
 

Tanzania 2025 elections: Why Magufuli legacy persists despite Samia's political reforms.​


Source: The East African Online Newspaper

Hakuna Gazeti ambalo GENTAMYCINE naliheshimu kwa Uweledi wake uliotukuka kama la The East African kwani lina si tu Waandishi Nguli na Wabobezi bali pia lina Waandishi ambao ni very Intelligent na hawakurupuki kuja na Taarifa zao ambazo zimefanyiwa kila aina ya Utafiti na Uhakiki ndiyo maana zikawekwa kwa Sisi Walaji Werevu tuzisome.

Rais Samia nitaanza Kumpima na Kumuelewa kama akipita tena 2025 ila kwa sasa najua anatambaa na Chaki kwa Kufuata na kuyafanyia Kazi yale yote ambaye aliyekuwa Boss wake Hayati Magufuli aliyaandaa na mengine kuanza Kuyatekleza hivyo tusidanganyane kuwa kuna alilofanya Yeye kama Yeye.

Rest In Peace Mwamba na Mthubutu wa Kweli katika Maamuzi na Mtu ambaye hukuwa Mnafiki na Muoga Late John Pombe Magufuli ( JPM )
 
Samia reforms are aimed at turnishing Mwendazake 's legacy.Walinda Ligacy mnahangaika sana.
 

Subili utupiwe mawe na wale Wadudu wa nguo chafu. Oooh walinda legacy oooh mwashita ooooh push gang Yaani jamaa wa Kizimkazi ukweli ulioandika hawataki kuusoma kabsaa
 
Madiwani na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wanakiri kuwa rais Samia yupo na nia thabiti kusaidia wananchi.

Anatoa pesa nyingi sana ili kuwezesha na kukamilisha miradi ya kusaidia maendeleo ya wananchi.

Pesa zinaliwa na kutafunwa kama njugu. Ameshindwa kusimamia rasilimali za umma.

Je, waarabu huko Ngorongoro wameuziwa nini?

Acha mwamba wa Rubambangwe akubukwe kwa kila namna

 
Utawala ni watu ,mamlaka ni majeshi ! Kibali Cha mungu ni sauti ya watu ! Rais wangu wateule wako ni WA kwako sio wa kwetu ! Usipime Imani yetu kupitia wateule wako ! Wateule wako wapo ili wakufurahishe wewe ni sio kutuhudumia sisi hili unalijua?

Aliyeshiba hamjui mwenye njaa! Juzi wametutangazia nafasi za kazi kwa mbwembwe ! Kwamba wewe umeidhinisha waajiriwe waalimu 12000!! Na wauguzi kadhaa wa kadhaa !

Tulijua shule zitafungua na waalimu wapya watakuwa kazini na tulidhani upungufu wa waalimu unaenda kutatuliwa mara Moja ! Kinyume chake shule zimefunguliwa Kila mtu yupo kimya !

Hakuna ajira kwa waalimu Wala wauguzi ! Vijana wetu waliposikia mbwembwe za waziri wa tamisemi walianza kumeza mate ya matumaini lakini wameanza kupaliwa kwa ukimya wa wizara ya elimu pamoja na tamisemi !! Ninini ambacho kilifanya mtangaze ajira ambazo Bado hazijawa tayari ?

Rais wangu watanzania huku vijiweni wanaongea vitu tofauti na unavyoambiwa na wateule wako !huku mtaani Hali ni ngumu !! Narudia Tena hali ni ngumu !! Weka utaratibu wa kutusikiliza sio Kila kitu kipitie kwa wateule wako wanakudanganya !!
 
Ameshajibadilisha na kuwa Amphibian...mpaka yafanyike mambo ya Gen Z ndiyo atasikia
 
umeskizwa hata kwa hili bandiko lako tu 🐒

kua mstahimilivu na mwenye subra...
ajira nyingi kama hizo ni mchakato. usiwe na moyo wa kukata tamaa na kulaumu hali ngumu....

fursa rasmi hivi sasa kwenye kilimo ufugaji, biashara n.k zipo nyingi tu anza nazo ukisubiri hizo za ajira...

serikali sikivu ya CCM itamkiza kila mTanzania mwenye maoni na mtazamo wa kujenga ili kama Taifa tusonge mbele Pamoja 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…