Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Atuachie Tanganyika yetu. Atoke. Atoke.
 
Hata mwanaye amethibitisha na anajua Mama yake hapendwi

 
Hu uzi utafutwa kama wilaya ya Ngorongoro, ngoja mods bado wanapata breakfast.
hivi hao mods huwa wanapatikana wapi.

mwanzoni huu Uzi nilikuwa sijaelewa sana, sasa nimekuelewa. ni swali zuri sana kujiuliza maana hali sio kabisa!
 
Katika mambo ambayo CCM 2025 hawapaswi kamwe kukosea ni kumrejesha Rais huyu madarakani
1. Kwanza Tanzania bado tunatawaliwa na mfumo dume kiasi kwamba hata ndani ya CCM wenyewe hawapo tayari kumwongezea miaka na wapo wengi tayari kumchagua hata upinzani maadamu ni jinsia ya kiume .

2. Wengi wanaona kwamba hayupo tayari kulinda Raia wake, kumekuwa na ajari, Ngorongoro wafugaji wanatumia yeye ameamua kuwa kimya
3. Issue ya bandari inamtafuna maana hata kanisa Katoliki ambalo limeota mizizi mpaka kijijini mashauri yao yamepuuzwa na kumbuka wapo watu ambao hawawezi kudharau kauli ya viongozi wao
4. Kikokotoo na nyongeza za mishahara kwa wafanyakazi imepuuzwa.
5. Utekaji umekithiri bado kama amiri jeshi Mkuu mfariji wa raia mlinzi wa uhai wa wananchi yeye amenyamaza kimya.
CCM mnapaswa kufanya maamuzi magumu sana uchaguzi wa 2025
 
Hakika anaupiga mwingi
 
1. Kwanza Tanzania bado tunatawaliwa na mfumo dume kiasi kwamba hata ndani ya CCM wenyewe hawapo tayari kumwongezea miaka na wapo wengi tayari kumchagua hata upinzani maadamu ni jinsia ya kiume
Tusibague Mtu kwa Jinsia yake Rangi yake Dini yake Kabila lake nk.

Ubaguzi wa aina yoyote haufai tuchague Mtu kutokana na uwezo wake.
 
Well said✌️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…