1.Hatoi matamko kama kiongozi mkuu wa nchi.
Kuna issue ya watu kupotea katika mazingira tata but majibu anayoyatoa ni kama mtu mlevi vile anapokua anatoa maelekezo kwa wahudumu wa bar.
2 Hachukui maamuzi magumu kuinusuru nchi yetu,tangu aingie madarakani suala la rushwa limekua ni kaa la moto,kila report ya CAG inapotoka inakuja na madudu meengi lkn kama kiongozi mkuu wa nchi haoneshi usiriazi wowote kupambana na hilo tatizo kama watangulizi wake.
3. Uwajibikaji wa watumishi wa umma ni sawa na zero kwa sasa lkn Raisi hata hakemei hiyo tabia.
4. Nchi imepasuka vipande viwili coz hakuna ile tunaita umoja wa kitaifa na yeye kama kiongozi mkuu wa nchi hajishughulishi wala kuliunganisha taifa,ndio kwanza daily ni kutoa vitisho kwa wananchi.
5. Watu wake wa karibu kutuhumiwa kuwa na ukwasi ambao sio wa kawaida,mfano mmoja wa watu wake wa karibu ambae yuko nae kila kona ya ziara yake anatuhumiwa kuwa na ukwasi usiokua na maelezo lkn Yeye kama kiongozi mkuu wa nchi bado kaendelea kumkumbatia.
6. Ziara zake kukosa hamasa kwa wananchi.
7. Kugawa vyeo kwa upendeleo.
Hayo na mengine mengi yamenifanya niwaze huyu Mheshimiwa amejikatia tamaa na kuizira nchi yetu au vipi,na kama ni ndio kwa nini asiachie ngazi mapema tu akatoa fursa kwa wenye moyo na ari ya kuwatumikia wananchi wakachukua nafasi yake?