Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Nyiee acheni mambo yenu, Zama za Mwendazake zimeshaisha.
Kwani JPM alijiuzulu uwaziri wakati wa Kikwete? Mbona hamkumuita mnafiki wakati anamkosoa hadharani baada ya kuwa raisi?
Msiwe ma sore looser, mipango ya mungu haiwezi shindwa na nyie wanadam.

Tuoneshe ilani ya Samia ambayo ni tofauti na ya mtangulizi wake!
 
Ni mmoja wa vyeti feki au? Hao waache wafie mbali bhana! Vyeti feki! NO! Hata kama tumempata rais mwenye vyeti vya aina hiyo, NO!

Ha ha ha ha

Shida nyie huwa mnakuwa too personal mtu akitoa maoni basi anajibeba yeye.

Waliita vyeti feki lakini hawakuwa na vyeti vya kidato Cha nne, walisoma mpaka vyuo...wengine walikuwa na vyeti 2 kwaajili ya kurudia.

It was very unfair kuwatoa bila mafao.


Mi bado nipo kazini nadunda na vyeti vyote kuanzia la saba mpaka Masters halafu viko vizuri sana....kichwa kiko vizuri.
 
Kwahiyo yeye kusema Mama Samia ndio rais wa JMT ndio hallucination???

😀😀😀😀😀😀😀😀

Mnateseka sana
Kama unashindwa hata kufatilia bora upige kimya . sasa niteseke na kitu gani au ndo mwendelezo wa maneno ya vikoba?
 
You are very shallow in analysis of issues. and putting each scenario into its right perspective. Wewe kama inawezekna kujiuzulu, mbona hapa una ID fake. Ungeliweka identity yako ukamkosoa Jiwe bila kujali watu wasiojulikana. Kwa Udikiteita wa Jiwe nani angediliki kusema ukweli wake? Kila mmoja na wewe inclusive, ulitenda usichokiamini kutetea kazi yako na maisha yako. Basi na hao mawaziri/VP walitenda hivyo kwa maslahi ya kazi zao na maisha yao! Nani Africa alijiuzulu kupingana na Boss/kiongozi wake?

Siyo kila mwenye mtazamo tofauti na wako ana maslahi binafsi serikalini. Nina miaka zaidi ya 25 tangu nitoke katika civil service!

Your reasoning is seriously handicapped. Are you saying that no one should be prosecuted and convicted for theft that one actually committed, just because there are so many people who steal every day?
 
JPM alinadi ilani tofauti na ya watangulizi wake. Ilani ya Samia ni ipi?
Kwani ilani ndio inasema kwamba usiseme madhaifu ya rais aliye pita ? Kimbuka ile ni ilan ya chama (ccm ) na sio ilani ya magufuli hivyo magufuli kama mtu ameonesha udhaifu mkubwa ambao sio ya kiilani bali ni kwa utashi wake hivyo si vibaya idhaifu wake ukiwekwa bayana maana unakiuka ilani ya chama.
 
Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi walikuwa wanahubiri na kusimamia wasichokiamini. Kitendo hicho cha kuhubiri na kusimamia wasichokiamini kilikuwa unafiki na utovu mkubwa wa nidhamu kwa wapigakura wa nchi hii. Hili limenikumbusha hata ule utovu wa nidhamu ambao VP na PM waliuonesha wiki nne zilizopita kwa kuwapa wapigakura salaam hewa kutoka kwa Hayati JPM ilhali wakijua JPM alikuwa mahututi ndani ya ICU.

Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.

VP au Waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.

Needless to say, VP au Waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.

Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!

Haya ni maoni yako. Wengine tunaona amefanya kitendo cha kijasiri kuibua, kutimua na kubadili madudu yaliyokuwa yakiendelea nyuma ya pazia. Kiongozi hutakiwi kususa na kujiuzuru kila ushauri wako unapokataliwa, mama alikuwa na maono na akasubiri wakati muafaka ambao ndio huu
 
Back
Top Bottom