Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Hii kauli ya mama sikuielewa kabisa!!

''KWA UAMUZI HUU NAJUA UCHUMI UTATIKISIKA LAKINI NAOMBA TUVUMILIE''

Je ni sahihi Rais kusababisha uchumi kuyumba tena kwa maksudi? Ili kimfurahisha nani? Kamwe kiongozi usiongoze ili kuwafurahisha unaowaongoza.
Huu ni wakati wa kutengeneza walipa kodi wengi wa baadaye baada ya uchumi wao kuimarika na wao kuweza kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi, kwa lugha nyepesi tuanze na maendeleo ya watu ili tuje kwenye maendeleo ya vitu.
Kiongozi mwema na mwenye hekima siku zote anatakiwa awafurahishe anaowaongoza.
 
Kama vyama vya siasa bado vinakatazwa kufanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba, na wewe hujaingilia kati kwa ishu ndogo kama hii ambayo hutapata lawama maana kipo kikatiba, Basi naanza kuwa na mashaka utawala wako.

Najua umezungukwa na wahafidhina wa CCM, lkn Kama dhamira yako, sheria na Katiba vinakupa haki katika kufanya lolote, waambie kuwa kwa hili niacheni.
 
Mkuu vyama vya upinzani kupitia wenyeviti wake kama vile Mbowe, Tundu Lisu nk, wanadai kuwa nchini kuna corona. Sasa kama kuna corona kwa mujibu wa maneno yao wenyewe. Hauoni kama wakipewa ruhusa ya kufanya mikutano watasababisha maambukizi yasio ya lazima. Usihamishie lawama kwa raisi
 
Minyumbu basi inajua ndio itajiachia muda wa kuchapa kazi huu!!!sio muda wa siasa wayabane hivyo hivyo
 
Mkuu vyama vya upinzani kupitia wenyeviti wake kama vile Mbowe, Tundu Lisu nk, wanadai kuwa nchini kuna corona. Sasa kama kuna corona kwa mujibu wao wakipewa ruhusa ya kufanya mikutano watasababisha maambukizi yasio ya lazima
Msibani kwa mwenda zake,mbona hawakuzuia watu kukusanyika?
 
Watz huwa tunashangilia mapema sana.......anewei mnasahau kuwa utawala ni uleule, chama kilekile,Polisi walewale..........kilichobadirika ni kifo cha jeipiemu tu......mabadiliko hayawezi kutokea ovanaiti tu
 
Tumpe Muda na tumwombee yale mashetani yasimzidi nguvu.
 
We subiri,subira huvuta kheri
 
Mtu hata kuteua ma RC na Ma DC bado
Mnataka kuanza kumpa demands?Hata mwezi bado?

Mbona alipokuwepo Yule jamaa mliufyata kabisa?

Mpeni mda
Kweli aisee twende polepole. Muda bado upo maana hata mwezu badi atafanya mangapi?? Nikweli serikali ile ye ibilisi mwendazake ilituumiza lakini twende taratibu tutavuka.
 
Ni mapema kumlaumu apewe muda, pia ni muhimu kutambua amechukua hatamu kwa aina gani.
 
Hakuna Kiongozi hapo. Kwa miaka mitano alikuwa kimya kuhusu udhalimu na dhuluma za dikteta. Kuna kundi kubwa linalotaka kuendelea kumuenzi dikteta na dhalimu sijui kwa lipi la kuenzi. Ngoja tuone Mkuu naona mama anacheza dansi kati ya Dodoma na Dar. Leo yuko Dar kesho yuko Dom and vice versa. Sioni jipya but time will tell.

 
Kwa Baraza la Mawaziri aliloteua na ambalo halina tofauti na lile la dikteta na dhalimu sioni mabadiliko yoyote makubwa katika uteuzi wa maRC na maDC.
AMtu hata kuteua ma RC na Ma DC bado
Mnataka kuanza kumpa demands?Hata mwezi bado?

Mbona alipokuwepo Yule jamaa mliufyata kabisa?

Mpeni mda
 
Kweli mwendazake alikua kiboko maana we all tumepata sauti zetu tena!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…